Upinzani wakwaza chaguzi za CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upinzani wakwaza chaguzi za CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 24, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 23 May 2012 20:48[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]


  Mwandishi Wetu
  UPINZANI hasa kutoka kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) unaaminika kuwa moja ya vikwazo vya kutofanikiwa kwa asilimia 100 kwa chaguzi za ngazi za mashina na matawi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Miongoni mwa maeneo ambayo yamefanya vibaya katika chaguzi hizo ni Arusha Mjini na Iringa Mjini ambako Chadema kinaaminika kuwa na wanachama wengi, kwani kilishinda viti vya ubunge katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

  Habari kutoka ndani ya CCM zimeeleza kuwa chama hicho, kimeshindwa kujaza nafasi za uongozi katika mashina na baadhi ya matawi hivyo kufanya nafasi hizo ziendelee kuwa wazi huku zikitajwa sababu mbalimbali ikiwamo migogoro ya kisiasa ya ndani kuwa chanzo.

  Taarifa ya Idara ya Oganaizesheni ya chama hicho iliyowasilishwa katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) hivi karibuni Mjini Dodoma, imeeleza kuwa migogoro hiyo imewafanya makada wa chama hicho washindwe kuhamasishana kujitokeza kuomba nafasi za uongozi.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo ambayo Mwananchi imefanikiwa kuiona, migogoro hiyo imefanya kukosekane kwa uhamasishaji wa kutosha na hivyo kufanya watu wasijitokeze kugombea uongozi.

  Imebainika kuwa CCM kimeshindwa kufanya uchaguzi katika mashina 74,748 sawa na asilimia 15.9 ya mashina yake 468,587 yaliyopo nchi nzima. Kadhalika, kimeshindwa kufanya uchaguzi kwenye matawi 6,045 sawa na asilimia 26.9 ya matawi yake 22,464 nchini.

  Taarifa hiyo ya CCM inaonyesha kuwa hali ni mbaya zaidi kwa Jumuiya yake ya Vijana (UVCCM), ambayo hadi sasa haijaweza kufanya uchaguzi kwenye mashina 101,387 sawa na asilimia 34 ya mashina yake 308,484 yaliyopo nchini.

  Kwa upande wa matawi, UVCCM hawajawasilisha taarifa yao hadi sasa, wakati Jumuiya ya Wazazi haikufanya uchaguzi kwenye matawi 5,891 sawa na asilimia 28 ya matawi yake 20,928 na Jumuiya ya Wanawake (UWT), haikufanya uchaguzi kwenye matawi 6,271 idadi ambayo ni sawa na asilimia 28.6 ya matawi yake 21,761.

  Mchakato wa uchaguzi ngazi ya shina ulifanyika kati ya Februari 4 na 29, mwaka huu kwa upande wa jumuiya za chama hicho, wakati kwa upande wa uongozi wa CCM, ulifanyika kati ya Februari 20 na Machi 31, mwaka huu.

  Mchakato wa ngazi ya tawi kwa upande wa jumuiya, ulifanyika kati ya Machi 3 na Aprili 22, wakati kwa uongozi wa jumla ulifanyika kati ya Machi 26 na Aprili 29 mwaka huu.

  Mikoani na wilayani

  Katika Mkoa wa Arusha, taarifa hiyo ilisema vijana wengi kwenye mashina walikuwa hawajaandaliwa kikamilifu, hivyo kushindwa kufanyika kwa uchaguzi huo.

  “Hata katika chaguzi zilizopita, inaonyesha mkoa huu hawakufanya uchaguzi katika ngazi ya mashina ambayo ni mapya katika Jumuiya ya Umoja wa Vijana,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza:

  “Wilaya ya Arusha Mjini haikufanya uchaguzi kwa sababu ya wanachama waliojitokeza waligundulika ni mamluki hivyo chama kikasitisha uchaguzi ili zoezi lianze upya kwa kuwapata wanachama waaminifu na wenye imani na CCM kugombea nafasi hizo.”

  Pia ilibainisha kuwa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha inaendelea na mchakato wa uchaguzi wa mashina 6,853 kutokana na kuahirishwa kwake ili kupisha uchaguzi mdogo wa ubunge ambao ulifanyika Aprili Mosi, mwaka huu.

  Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa katika Wilaya ya Ludewa, Iringa, chaguzi hazikufanyika kama ilivyokusudiwa kwa kutokujitokeza kwa wagombea katika baadhi ya mashina.

  “Iringa Mjini ni wilaya iliyopo nyuma kwa ratiba kwani haijafanya uchaguzi wa mashina wala matawi kutokana na tatizo la ulegevu wa usimamizi wa kazi wa watendaji wa wilaya,” ilisema sehemu nyingine ya taarifa hiyo.

  Taarifa hiyo imetaja mikoa ambayo chaguzi zake ngazi ya mashina zilizofanyika kwa kati ya asilimia 50 na 60 kuwa ni Tabora na Kigoma na Mikoa ya Shinyanga, Morogoro, Mbeya, Mtwara, Kaskazini Pemba na Arusha katika ngazi ya matawi ambako uchaguzi ulifanyika kwa kati ya asilimia 50 na 69.

  Mikoa ya Rukwa, Iringa, Kagera, Arusha na Dodoma chaguzi zake zilifanyika na hazikuwa na ushindani kwani zilikuwa chini ya asilimia 50.

  Ilisema Mkoa wa Rukwa katika Wilaya ya Sumbawanga wanachama walikosa hamasa ya kujitokeza katika uchaguzi mara baada ya kesi ya Ubunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini iliyosababisha CCM kutopeza jimbo hilo na kuwafanya wanachama hao kutojitokeza.

  “Baadhi ya maeneo wanachama wengi hawakujitokeza kwa utashi wao kuomba uongozi, hivyo uongozi wa matawi umelazimika kuwateua mabalozi pasipo kufanyika uchaguzi katika ngazi hiyo mfano Mikoa ya Mjini Magharibi, Dar es Salaam, Kilimanjaro na Kigoma,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza:

  “Watendaji na wajumbe wa vikao vya uchujaji na uteuzi wa wagombea hawana uelewa wa kutosha juu ya matumizi ya alama za sifa zinazotolewa kwa waombaji wa uongozi kwa mujibu wa kanuni.”

  Uchunguzi wa gazeti hili katika mikoa mbalimbali, umebaini kuwa makada wengi wa CCM walikwepa kugombea nafasi hiyo jambo lililofanya walazimishane na kuleta wakati mgumu kupata warithi.

  Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, mabalozi au wajumbe wa shina ndiyo ngazi ya kwanza ya uongozi ndani ya chama hicho pia ni kiungo muhimu kati ya chama na wananchi katika maeneo wanayoishi.

  Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Augustino Mbogo alinukuliwa na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita akikiri kwamba kazi ya kuchagua mabalozi wa nyumba kumi iliingia dosari na kufanya baadhi ya watu kususa.

  Hata hivyo, aliwatupia lawama baadhi ya watendaji ndani ya chama hicho kwa ngazi ya kata na matawi kuwa walikuwa kikwazo kwa kukwamisha mchakato huo na kuwafanya baadhi ya wanachama kususa.

  Wakati katibu huyo akieleza mchakato huo, uchunguzi uliofanywa katika baadhi ya maeneo umebainisha kuwa kwa baadhi ya sehemu, nafasi hizo hazikutangazwa kabisa, hivyo kufanya mabalozi waliokuwa madarakani waendelee kuongoza hata kama muda wao umepita.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Ukiona mtu anaipenda ccm ujue akili zake kama lusinde(mavi).;:;(;(;(;(;(;(;(;(;(
   
 3. p

  pstar01884 Senior Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Njia ya Kaburini haikwepeki.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  nimependa sana analysis yako na hasa hayo ma percentage ..yamenifurahisha sana na nimeelewa sana mimi...kweli JK mungu akubariki kwa maana bila wewe CCM isingekufa kifo hiki....mungu akutiee maguvu umalize kazi yako ya kuweza historia ya ccm kuwa chama cha upinzani 2015...
   
 5. k

  kijiichake JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ccm kwisha.
   
 6. a

  annalolo JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  komba anajianda kutunga nyimbo mpya kwa ajili ya kuizika ccm
   
 7. K

  Kalimanzira Senior Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Aug 15, 2007
  Messages: 100
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa taarifa hii, hata wale wanojipa moyo nadhani sasa ni wakati wa kuona mbivu na mbichi. Kwa mtu anayefahamu siasa anatakiwa kujua kabisa kuwa 'mtaji mkuu wa chama ni wananchi/wanachama, tena wa kawaida' ukiona chama kinakimbiwa na wanachama au wanachi hawatki hata kujihusisha nacho ujue ndi mwisho wake. CCM kwa miaka mingi ime nufaika sana na kukubalika kwake, na sasa kama wanchi hawataki hata kuomba uongozi ujue safari yake inafikia ukingoni.
   
 8. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  itachukua muda mrefu sana kwa CCM kuanza kujipanga upya. Na hii ni hata kama kitakuwa tayari chama cha upinzani. bado itachukua muda sana kuonekana kama chama cha siasa. hang over ya kupoteza madaraka, kutapelekea kurumbana na kutukanana na kutafuta mchawi. baada ya hapo, wengi wataachana nacho na kuanza kufanya shughuli nyingine au kuhangaika 'kufua' mitaji michafu walioipata walipokuwa madarakani. mpaka kije kujipanga kuwa kikundi cha kisiasa kitakuwa kimeachwa mbali sana. nadhani vyama vingine vya upinzani vitaweza ibuka nakuwa vyama vya siasa bora na makini kuliko CCM.
   
 9. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kumbe CCM Wanamashina mengi kiasi hicho 468, 500 mengi namna hiyo na pia matawi elf 22 na ushehe.

  Ebu wenye records watuambie CDM wana mashina na matawi mangapi?
   
Loading...