chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,968
Wabunge wa Upinzani wamesema wao walikuwa hawasaini posho kama naibu spika anavyodai na wanataka posho hizo kufutwa kabisa kama serikali ya JPM inataka kubana matumizi kweli
Mheshimiwa Spika, kabla sijatoa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu bajeti ya Serikali ya 2016/17, napenda kuweka rekodi sawa kuhusu upotoshaji unaofanywa na Wabunge wa CCM kwamba Wabunge wa Upinzani wanaisaini mahudhurio bungeni na kuchukua posho bila kufanya kazi.
Napenda mkumbuke kwamba, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikisisitiza kufutwa kwa posho za vikao kwa maana ya “Sitting allowance”, lakini serikali imekuwa ikipata kigugumizi, hivyo basi Kambi Rasmi inasema kama kweli Serikali ya Rais John Pombe Magufuli inania thabiti ya kubana matumizi ya Serikali basi inoneshe uthabiti huo kwa kuifuta posho ya vikao na fedha hizo zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo hususani kuwapatia Watanzania maji safi na salama.
Hata hivyo, tunashauri, wale wanaokaa bungeni bila kuchangia hata kwa maandishi na kuchukua posho, wafuatiliwe na wakatwe mishahara yao, kwa kuwa hawajafanya kazi na hansard itumike kuwabaini.