econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 22,138
- 32,715
Vyama vya upinzani vya Tanzania ukiondoa chama cha CHADEMA Vimeonesha wazi ya kwamba havipo kwaajili ya kuiondoa CCM madarakani bali vipo kwaajili ya kukifanya chama mapinduzi kuendelea kuwa madarakani.
Vyama vya upinzani vilikuwa na nafasi adhimu ya kukibana chama Cha CCM kikae pamoja nao na kufanya mabadiliko makubwa kabla ya kuingia kwenye uchaguzi kwa vyama vyote vya upinzani Kugoma kusign kanuni za maadili ya uchaguzi. Kitendo Cha vyama vya upinzani kukataa kusaini hizo kanuni kungepelekea CCM kushiriki uchaguzi pekee yake kitu ambacho kingekuwa kigumu kwao hivyo wangeingia kwenye mtego wa aidha CCM waende wenyewe kwenye uchaguzi au wasitishe mchakato wa uchaguzi mpaka reforms zifanyike.
Ila jambo la kushangaza wapinzani wakasema mhuni hasusiwi au wengine wakasema watalinda kura. Sasa unahangaika kulinda kura wakati ulikuwa na fursa ya Kugoma kusaini hizo kanuni ili uweke mazingira mazuri yasiyo kalazimisha kulinda hizo kura?. Wengine baada ya kusaini zile Kanuni wakaanza kulia kwamba zifanyiwe marekebisho. Kwakweli upinzani mmetuangusha wananchi.
Niseme tu kitendo Cha vyama vya upinzani kusaini kanuni za uchaguzi kimetoa ruhusa kwa CCM kuendelea na uchakakuaji wake maana Vyama vyote vimeridhia kanuni hazina shida. Yeyote anayesema atapambana huko huko ulingoni ni mwongo. Kwanini upambane wakati fursa ya kuweka mazingira sahihi ulikuwa nayo ila ukaiacha? Kwanini ulinde kura wakati fursa ya kuweka mazingira bora ya kisheria ulikuwa nayo? Shame on you upinzani.
Vyama vya upinzani isipokuwa CHADEMA, vimeonesha unafiki na uoga kwa CCM. Nakipongeza chama Cha CHADEMA Kwa kukataa kushiriki uchaguzi huu maana historia itawakumbuka kama chama kilichokataa kuwa mtumwa wa CCM .