assadsyria3
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 6,909
- 4,057
Kama unapenda ukweli hii ni habari njema lakini kama unapenda propaganda hapa hutoelewa. chadema imeenda Ukawa baada ya kuona chama kimepoteza mvuto hivo ili kujificha ikaamua kujificha kwa vyama ambazo awali vilijulikana kama ccm B, vingine vikiitwa Pandikizi la ccm.
Hio haimaniishi kuwa mapungufu yameisha chama sasa kinapumulia ICU. Imagine wabunge hawa majimbo yao huenda yasirudi tena Chadema, Arfi, mh Zito, mh Shibuda, mh Lema.
Bila shaka octoba 2015 CHADEMA hata nafasi ya kuwa chama kikuu cha upinzani itakosa.
Hio haimaniishi kuwa mapungufu yameisha chama sasa kinapumulia ICU. Imagine wabunge hawa majimbo yao huenda yasirudi tena Chadema, Arfi, mh Zito, mh Shibuda, mh Lema.
Bila shaka octoba 2015 CHADEMA hata nafasi ya kuwa chama kikuu cha upinzani itakosa.
Wadau, amani iwe kwenu.
Ni chini ya saa 48 zimebaki kufikia muda wa Watanzania kufanya maamuzi juu ya mustakabali wao pale watakaposimama kwenye mistari ili kupiga kura kuwachagua viongozi wao ikiwa ni pamoja na Rais, Wabunge na Madiwani.
Ni dhahiri kwamba yapo mengi yamesemwa wakati wa kampeni na wapo wanasiasa waliojigamba kuwa wataibuka washindi. Pamoja na majigambo hayo, ni ukweli usiopingika kuwa CCM imefanya chaguo sahihi kuanzia Mgombea Urais, Mgombea Mwenza, Wabunge na Madiwani. Wagombea wengi walioteuliwa na CCM ni mtaji tosha kwa vile wanakubalika na wananchi walio wengi.
Jambo jingine ambalo Wapinzani hawalijui ni mtaji mkubwa wa wanachama wa CCM. Tangu mwaka 2010, CCM imefanya kazi kubwa ya kurecruit potential CCM members ambao ni mtaji tosha wa wapiga kura. CCM ina zaidi ya wanachama 14,000,000 ambao imehakikisha kuwa wanajiandikisha na inahakikisha pia kuwa wanapiga kura. Hawa wenzetu wanategemea watu wanaopita barabarani kama ndo mtaji wao wa kisiasa ambao hata hivyo Magufuli amebadilisha upepo wao kutokana na jinsi alivyojinadi.
Jambo jingine ni mapungufu yaliyojitokeza ndani ya UKAWA. Si siri kwamba mchakato wa kumpata mgombea Urais kwa tiketi ya UKAWA uligubikwa na sintofahamu kubwa hali iliyopelekea baadhi ya waasisi wa umoja huo, Prof Lipumba na Dr Slaa kuachia ngazi kwenye vyama vyao na umoja huo. Wapo wanachama na wafuasi wengi wa CHADEMA, CUF na NCCR ambano nina hakika kuwa kura yao itakuwa kwa Magufuli. Tena hawa ni wengi kuliko wale wanaozingusha mikono kuashiria ni mabadiliko. Si siri kwamba UKAWA wamekurupuka katika mchakato wa kumpata mgombea Urais.
Kwa upande wa wagombea Ubunge, UKAWA nao hawako sawa. Ijapokuwa wamefanikiwa kukubaliana katika majimbo mengi, tena yaliyo mengi ni yale ambayo yanachukuliwa na CCM, kushindwa kukubaliana katika baadhi ya majimbo kumetoa mwanya kwa CCM kushinda kwa kishindo. Wao wakati wanalumbana, CCM inapita katikati yao kwa mwendo kasi na kuwaacha wakiduwaa.
Kwa haya na mengineyo ambayo sijayaeleza, ni dhahiri kwamba UKAWA wamechemsha. Baada ya uchaguzi, nataraji mambo yafuatayo kujitokeza.
1. LOwasa atakubali matokeo na kuachana na siasa. Kwa hali hiyo, Lowasa hatakuwa tena mtaji kwa wapinzani. Tayari mwanasiasa huyo ametangaza kurudi Monduli na kuchunga ng'ombe baada ya uchaguzi.
2. CHADEMA kitasambaratika vibaya mno. Ka vile kitakuwa na wabunge wachache sana tofauti na 2010, wafuasi wengi wa chama hicho watahama chama na kujiunga ama na CCM ama ACT.
3. ACT kitakuwa chama mbadala wa CHADEMA ijapokuwa hakitakuwa na ushawishi mkubwa kwa vile hakitakuwa na wabunge wengi bungeni
4. Kutakuwa na ugumu wa kuunda kambi ya upinzani bungeni. Je CHADEMA na ACT wataunda kambi moja ya upinzani?
5. CUF itakuwa imefutika kwenye ramani ya siasa Tanzania Bara. Itabaki Pemba tu na baadhi ya majimbo ya Unguja.
6. NCCR Mageuzi itafutika rasmi kwenye ramani ya siasa nchini. Kigoma haitakuwa ngombe yao tena. Natabiri NCCR hawatakuwa na jimbo hata moja mwaka huu.
7. Wananchi watakata tamaa na upinzani na wengi watarejea CCM baada ya Dr Magufuli kuanza kwa kasi huku akishughulikia matatizo ya wananchi kwa kasi ya ajabu.
8. Wazee waliotoroka CCM na kujiunga na UKAWA kama Kingunge, Mwapachu, Msindai, Mgeja Sumaye na wengineo waapoteza mwelekeo. Upinzani hawatatakiwa tena na CCM hawataruhusiwa kurejea.
9. Kuna wengi watakimbia nchi wakiwemo watendaji wa Serikali ambao walizoea kuishi kwa ufisadi.
Ka haya na mengineyo mengi, ni dhahiri kuwa kuanzia wiki ijayo, Tanzania itakuwa na chama kimoja tu chenye nguvu.