MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Kua na mfumo wa vyama vingi nchini fursa na bahati ya kipekee sana tusitoitumia vyema kwa sababu ya uchu wa madaraka na roho mbaya kwa baadhi yetu.Hatuna bahati kabisa,wenzetu walioitumia bahati hii tayari wako mbali sana kimaendeleo, walishaamini kua bila kukosolewa huwezi kua perfect.
Hili suala la mtu kujiaminisha kua anayo guarantee ya kuongoza taifa miaka 10 mfululizo huwafanya kua na viburi sana na kuahidi ahadi zisizotekelezeka,wengine huweka viporo huku wakiamini kua watamalizia awamu zijazo.
Kwa sababu Leo hii UKAWA ungechukua dola CCM wangeumia sana, na UKAWA nao wasingekibali kushindwa ili kupoteza heshima zao 2020! Kwa namna yeyote ile wangepigana kwa hali na mali ili kuhakikisha kua wanaaminiwa na umma tena 2020.Hivyo ushindani huu ungekua na manufaa makubwa sana kwa umma.
Tujifunze, mchawi wa maendeleo yetu ni wale wanaong'ang'ania madaraka upande mmoja kwa kutumia nguvu kubwa. Siku tutakapoamini katika demokrasia ya kweli ndivyo tutakavyojenga historia kubwa ya taifa letu lililonyuma kimaendeleo pamoja na Ukubwa wake.