Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Amani iwe kwenu.
Kwa mara ya kwanza nchi imekuwa na kambi ya upinzani iliyoshindwa kutekeleza majukumu yake sijui kwa umbumbumbu ama makusudi.
Hivi kususa kutoa mpango mbadala kunaboresha vipi upinzani? ama kunaathiri vipi serikali? Hotuba nyingi hasa zile zilizowasilishwa na Wabunge wa Chadema hazina mpango mbadala wala namba. Zimejaa vijembe na kushambulia watu. Huwezi kufanya ulinganisho wa mpango wa serikali na upinzani.
Mbunge anavunja kanuni za bunge ili kupata "attention" ya media kueleza upotoshwaji. Mfano hotuba ya Lema imeingiza mambo ya uuzwaji wa nyumba za serikali ambayo kimsingi ni wizara nyingine, Mambo ya Lugumi ambayo yanachunguzwa na kamati ya bunge hivyo kikanuni na kisheria hayapaswi kujadiliwa bungeni. Anaambiwa kuyatoa na Kamati ya Kanuni anazira kwa sababu kufanya hivyo hotuba yake itakuwa imekwisha. Hivi mpango mbadala uko wapi? Kwanini mnaruhusu upumbavu na ulofa kutamalaki hapo Chadema?
Hivi kwanini mnasusia vikao vya bunge siku wake/vimada wenu wakiwa hapo dodoma? manake Lema hakuona la maana la kuongea zaidi ya kumsifia mkewe. Aibu yenu.
Kwa vijana wadogo, Mh. Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Temeke miaka ya mwishoni 90. Aliiwajibisha serikali na mawaziri kujiuzuru bila ya Bunge kuwa "Live"... Ndio walijiuzulu... Prof.Mbilinyi (Fedha), Dr. Hans Kitime nk. Alitoa hoja ambazo hata wabunge wa CCM walimuunga mkono. Kambi rasmi ya upinzani isipobadilika mtakiona cha mtema kuni.
Kwa siasa za nyakati hizi mtapotea; kususa, matusi, selfie, bunge live havileti barabara, maji, umeme, afya nk kwa wananchi.
Nilikuwa pia napendekeza CAG atukagulie elimu za wabunge wa kambi ya upinzani hususani Lema, Msigwa, Kubenea, Sugu na Lijuakali na iwe wazi kama ya ATCL na TTCL.
Nawasilisha.