FredKavishe
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 1,090
- 318
Niweke wazi mimi ni mwanachama hai wa Chadema.
Turudi kwenye mada tunaelekea uchaguzi wa wabunge wa East Africa week ijao lakini upinzani huu tulionao wote unaenda kwenye uchaguzi ukiwa haueleweki.
Sheria zilizolipotia zinasema Chadema 2 CUF 1 CCM 6(Wabunge wa kwenda bungeni East Africa),Ndugu Zitto aka raise hoja kwamba wabunge wa upinzani wote wanaweza gombea kutokana na chama kikiwa na uwakilishi Bungeni,Akamuandikia Spika barua ambayo bado haijapata majibu mpaka sasa.
Turudi historia nyuma kidogo mwaka 2015 kulikua na muungano wa Ukawa(NCCR,CUF,CHADEMA,NLD) Huku ACT ilisimama wenyewe.Lakini kwenye huu Ukawa kuna wagombea wengi waliacha kusimama kwenye udiwani ama ubunge kisa hii Ukawa lengo likiwa ni moja kumtoa CCM.
Sote hatuwezi kataa haswa kwa Kigoma,ACT iligawa kura nyingi na kufanya majimbo mengi yaliyokuwa chini ya NCCR kupotea,inawezekana kuhama kwa kina Zitto,Kitila na wenzake kulisababishwa na kupishana kimawazo wakati wakiwa Chadema,Lakini yaliyopita si ndwele tugange yajayo.Ndio maana tulimuona Ndugu Lema(Mb Arusha) kwenye mkutano wa ACT akisema upinzani unahitaji sauti moja.
Tukirudi kwenye mada tukubali asilimia 18 ya wabunge wa CHADEMA ilichangiwa na UKAWA maana kuna sehemu CUF na CHADEMA walirudisha wote fomu tulikosa majimbo kama Ukonga,Segerea.Kwahiyo kama kulikua na mchango wa UKAWA kwanini CHADEMA hawakukaa na wenzao kushauriana tupeleke kina nani ama wakati wa kushirikiana umeisha tunasubiri 2019 tuanze muungano wa kinafki tena.
Ndugu zangu wapinzani siasa ni hesabu,uongo kwenye hesabu huangukia pua haraka sana,tunahitaji umoja kwenye Upinzani.Ifahamike lengo letu sio vyeo lengo letu ni kuleta Elimu bure,Afya ya tija,Maendeleo,Ajira hili ndio lengo na Act,Chadema,Cuf hawawezi fanikiwa wao kama wao bila ushirikiano kuunda upinzani wenye nguvu.
Daima tuamini upinzani ukiwa mmoja wenye nguvu tutawashinda wapinzani wetu,karaha ya Wabunge wa Africa Mashiriki kwa kweli ina kera inafahamika Cuf ina matatizo yake hayo tuache lakini Chadema kufanya mchakato bila kuwashirikisha washiriki wenzake kwenye Ukawa ni ukakasi mkubwa.Bila kuwasahau Act wanahitajika kujenga upinzani imara rejea matokeo ya Uchaguzi mkuu Kigoma,Rejea matokeo ya Udiwani mwaka jana.
Mtafanya sisi vijana tuanze uliza maswali mnataka badilisha hii nchi kweli ama mnataka madaraka,umoja wa upinzani kwa maendeleo ya kweli.Tuanze na Ubunge wa East Africa