Upinzani Tanzania Ujivue Magamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upinzani Tanzania Ujivue Magamba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Prophet, May 27, 2011.

 1. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema ni chama kikuu cha upinzani Tanzania. Anayekerwa na hilo asage sumu anywe au ajitie kitanzi. Sisi tutakula ubwabwa.

  Kutokana na mamlaka waliyonayo CHADEMA kisheria ya kuwa chama kikuu cha upinzani, inabidi, sambamba na suala muhimu la kuwaamsha watanzania na mapambano dhidi ya uozo wa rushwa, ufisadi na mauwaji kama yaliyotokea juzi-kati.

  CHADEMA sasa kijipange kuangalia ni nani kenge katika katika kundi la vyama vya upinzani. Kenge hawa lazima wadhibitiwe ikiwa ni pamoja na kuwaeleza ukweli wananchi juu ya kenge hawa ambao wao wako kimaslahi binafsi zaidi kuliko kuwatetea watanzania.

  John cheyo ni gamba.
  Gamba hili linazidi kuota kipara tu, na hakuna jambo lolote la tija amewahi kuwafanyia watanzania zaidi ya kujiita bwana mapesa. Gamba hili pamoja na chama chake lazima kuwawekea vikwazo ili ama waamue wabaki wapinzani waadilifu ama warudi CCM wakaendeleze ufisadi.

  Lyatonga ni gamba
  Gamba hili ni gumu kweli, aliingia upinzani akiwa mweusi tii, lakini sasa ameanza kujipodoa kutokana na ulaji anaoupata kutoka kwa waliomtuma, ccm. huyu hastahili vikwazo. Ni wa kufukuza kabisa kutoka upinzania.

  Dovutwa
  Huyu naye sijui alitoka wapi, aliingia kama mjusi, sasa anautaka ukenge kwa udi na uvumba. CHADEMA hakikisheni watanzania wanapata habari za mtu huyu.

  Lipumba
  Huyu anathiriwa na hulka ya wanyamwezi ya kuabudu wenye pesa, anawaogopa CCM. Hutoa matamko mengi yasiyotekelezwa na yeye mwenyewe na hao anaowatolea matamko (CCM).

  Chadema lazima kufahamu kuwa watanzania kwa mamilioni wana imani na wanawaunga mkono, kejeli, kuvunjwa moyo na mambo mengine ya namna hiyo yasiwape wasiwasi. Pambaneni na aina yoyote ya watu wanaotaka kuvunja harakati zenu za kuwakomboa wananchi wa Tanzania kutoka kwa koloni la CCM.

  Nimemaliza
   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hasa huyu mtu anayejiita Dovutwa naona anatumika kwa kasi sana.
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Kabla ujaleta thread yako jipange kwanza, nifunze matumizi ya herufi kubwa na ndogo, ebu angalia ulinyo andika kama mtoto wa darasa la tatu
   
 4. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hasa yule Dr anae kifisadi Chama chake kwa kulipwa Milioni 7.5 ajivue gamba kabisaaa ilijifanya akiwa bungeni analalamika kumbe unafiki!
   
Loading...