Upinzani sio uadui....

Upinzani sio uadui....

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2013
Posts
2,602
Reaction score
409
Katika maana kueleza maana ya upinzani lazima niweke tofauti iliyopo kati ya uadui na upinzani
Upinzani ni kuwa na kundi la watu/taasisi fulani iliyoundwa na watu wenye kusudi moja,fikra,maono,falsafa na mitazamo inayofanana.Na uadui ni kuwa na uhasama na mtu/kundi fulani la watu baada ya kukufanyia kitu kibaya,ndiyo maana unaweza kukosana na rafiki yako na kuwa adui yako baada ya kukufanyia jambo baya.
Lakini,upinzani nikiutazama katika mazingira ya kisiasa naona ni uadui, kitu ambacho sio kweli! Bali ni mitizamo tofuti ya kiitikadi na kisera. Nasema sio uadui kwa kuwa upinzani hauna kulipiza kisasi.
Yanayoendelea ndani ya chama cha mapinduzi kwa chama cha demokrasia na maendeleo na vyama vingine vilivyowahi kuwa na nguvu(NCCR-mwaka 1995 na CuF mwaka 2000) ni dhahiri kuwa CCM inachukulia upinzani ni Uadui,kitu ambacho sio kweli.
Hapa tumeshuhudia mengi,zikiwemo tuhuma mbalimbali zenye lengo za kuharibu vyama vya upinzani,hii ni dhahiri pale inapotokea chama kuwa na nguvu zaidi ya chama tawala cha CCM.
Tumeshuhudia matamko mengi ya ajabu majukwani ya chama tawala,mara chama hiki ni cha wapi,mara cha watu hawa.Athari za kauli hizi zi bayana,na hakuna haja ya kuzitaja
CCM,kauli zao ndizo zinaharibu utulivu,amani na umoja wa taifa letu. Kifupi ccm uwezo wao wa kutawala umeshafika mwisho.Watakuja na kauli za ajabu ajabu juu ya upinzani,lakini kauli hizo wananchi wanazichukulia kuwa n uzushi,uongo na hujuma dhidi ya upinzani.
Wananchi wanajua lipi jema mlilofanya,mabaya mnayoyafanya,na wanajua kasoro,udhaifu wenu.Lakini kwa kuwa hamkotayari kupingwa,kukosolewa,matokeo yake ndio kung'oa watu kucha na meno.
Wananchi kuunga mkono vyama vya upinzani,sio kwamba ni wajinga bali wako rational katika kufanya maamuzi.Sasa nyie kazi yenu ni kulaumu vyama vya upinzani. Itafikia wakati hata geti likigoma kufungua mtaulumu upinzani.
Ccm nchi imewashinda,na dalili ya kushindwa ni kulalamika kila linapotokea tatizo na kuwa na kauli zinazokinzana.Katika management principles,ukikuta kiongozi analalamika juu ya tatizo fulani na wananchi wanalalamika tatizo hilo hilo ujue huyo ni kiongozi kipofu.
Na matokeo yake kiongozi kuwa na yake kiongozi kuwa na majibu ya mkato,yanayolenga kuonesha kuwa chanzo cha tatizo limetokana na upande wa pili.Kitu ambacho sio kweli.Dalili zingine kwa kiongozi kuwa kipofu ni pale anaposhughulikia matokeo ya tatizo na siyo chanzo cha tatizo.
Upinzani,sio kulipizana visasi,sio kuoneana bali ni kukosoana na kupingana kwa hoja. Na kazi ya mpinzani wako sio kukusifia,na kusifiwa wakati ni wajibu wako na serikali yako hii ni wazi kuwa hakuna uwajibikaji.
Kazi ya chama tawala ni kutekeleza ilani yake,kama unatekeleza ilani yako nani atyasimama na kukukosoa?
CCM mbadilike wananchi hawawataki!!
 
Wanaelewa na katika kuongezea ni kwamba mmoja ana dola na mwingine anataka kushika dola,sasa mziki unaujua kwamba kuachia dola inamaana kuachia chakula,sasa obviously anayetaka kunyang'anywa hawezi kubali kirahis,so is the survial of the fittest,ni kanuni tu kuzielewa na kuzi apply
 
Back
Top Bottom