Upinzani: Serikali inatarajia kukusanya Tril 23.9 ila itatumia Tril 26.9 utasikia Ndiooooooooooooooo

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,883
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeeleza kuwa takwimu za vitabu vya bajeti iliyowasilishwa Bungeni zinatofautiana sana na pia sura ya bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Phili Mpango inatofautiana pia na vitabu hivyo.

Naibu Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango David Silinde (Mb) ameeleza Bungeni kuwa;

“Wakati kitabu cha Mapato ya Serikali kinaonyesha kuwa Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 itakusanya jumla ya shilingi trilioni 23.9; kitabu cha Matumizi ya Serikali kinaonyesha kuwa Serikali inakusudia kutumia jumla ya shilingi trilioni 26.9 ikiwa ni ongezeko la matumizi ya shilingi trilioni 3 ambayo vyanzo vyake havijaonyeshwa kwenye kitabu cha mapato. Wakati huo huo, sura ya bajeti iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango inaonyesha kuwa bajeti ya Serikali kwa maana ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/18 ni kiasi cha shilingi trilioni 31.7”.
 
Wazee wa Kupika Data., Uzuri wa Number Ni kwamba HAZIONGOPI.. zinawaumbua hadharani.
 
CCM ni janga la taifa. Mungu naomba hawa watu ufanye mpango wowote ili waondoke mara moja!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom