Upinzani mmepata mikutano ya hadhara msituangushe

Upinzani mmepata mikutano ya hadhara msituangushe

AFRIKAMOJA

Member
Joined
Aug 11, 2022
Posts
30
Reaction score
37
Hivi karibuni Rais wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa juu wa vyama 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu nchini alitangaza rasmi kuliondoa zuio la mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa.

Ukweli ni kwamba kufanikisha au kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa ni gharama kubwa sana. Ufanisi wake unategemea upatikanaji wa rasilimali fedha, nguvu kazi, magari/vyombo vya usafiri, vyombo vya muziki/matangazo, waandishi wa habari nk

Sasa nimejaribu kutazama kwa kina vyama vyote vya upinzani kiujumla na kiuweli vyote vina hali mbaya kiuchumi. Havina uwezo wa kufanya mikutano ya hadhara kwa ufanisi lazima vitasuasua sana.

Naona dhihiri kabisa kwa awali watawekeza sana kwenye siasa za mtandaoni ili kuendelea kuonesha uwepo wao lakini kwenye ground watapotea.

Hivyo naona wazi wataanza kampeni za kuhamasisha wanachama wao, wafuasi wao, wapenzi wao na wapenda demokrasia au siasa za mabadiliko/mageuzi kutakiwa kuwaunga mkono kupitia wanayoiita michango ya hiyari kwa kuwachangia chochote kitu kupitia laini za simu, akaunti za benki au mauzo ya kadi na ada za uanachama.

CCM wao naona wako tayari wakiviacha mbali sana na vyama vingine kwenye maeneo yote ya msingi na muhimu kwa mikutano ya hadhara yenye ufanisi.

Nashauri tena, michango sasa basi jipangeni wenyewe!

#MwelekeoMpya #WananchiKwanza
 
Hivi karibuni Rais wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa juu wa vyama 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu nchini alitangaza rasmi kuliondoa zuio la mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa...
Akuchangishe nani wewe njaa kali unayeishi kwa dadako hata kupanga chumba kimoja umeshindwa? Lini mbu akamchangia binadamu damu? Dhiki hadi kwenye kope za macho.
 
We umezoea mikutano ya kupakia watu kwenye maroli na kuwabwaga kwenye eneo la mkutano ili wamsikilize Zuchu.

Kuna vyama ambavyo vinahitaji eneo na jukwaa Tu. Wafuasi wao watakuja na kujaa kwa usafiri wao. Sasa chama kama hiki kinahitaji fedha ya kazi gani?
 
Back
Top Bottom