Upinzani kupewa Wizara (?)

Upinzani kupewa Wizara (?)

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,866
Reaction score
4,252
Ndio maono yangu. Kuna dalili kadha wa kadha zinazoashiria upinzani kupewa wizara moja ambayo ni ya Fedha. Wanasema mchawi mpe mwanao amlee. Katika kuutazama upinzani nikaona hakuna dalili ya UKAWA kwenye safu ya uwaziri. Ndipo nikamuona kiongozi mkuu wa ACT akipewa jukumu hilo. ACT waliandaa maandamano ya kumpongeza Rais Magufuli katika utendaji wake. Cheki hapa Kwa upande wa UKAWA wao wanadai kuwa Magufuli anatekeleza ilani ya UKAWA ila haitekelezi ipasavyo.

Baadhi ya viashiria.
1. Zitto kupongezwa na Rais kubaki Bungeni wakati wa hotuba yake.
2. Zitto kukutanishwa na Magufuli kupitia Kikwete.
3. Zitto kuwa mtaalam wa uchumi na mambo ya fedha
4. Zitto kuwa karibu zaidi na chama tawala kuliko wapinzani wengine. Rejea hata kubadilishana majimbo na Serukamba
5. Zitto kuongoza kamati ya POAC/PAC kwa ufanisi na muda mrefu.
6. Rais kutotenda haki kwa wabunge wa majimbo kwa kutowateua kuwa mawaziri
7. Rais kupenda kushitukiza kwa matukio ya uteuzi. Mfano kwa Waziri mkuu Majaliwa.
8. Rais kutimiza kauli yake kuwa yeye ni Rais wa wote bila kujali itikadi, vyama, dini, n.k.
9. Rais kutaka kuzima 'kelele' za upinzani bungeni na serikalini
10. Na mengine mengi

Hivyo yawezekana tukashuhudia hiki ninachokifikiria. Tatizo CCM watamwelewa Rais? Ni jambo la kukaa na kusubiria.
 
Habari kama hii ilitolewa na Kaka Kiiza akiiita ni breaking news kutoka ITV kuwa ProPesa Ibrahim Lipumba ameteuliwa kuwa msahauri wa .......
 
prof. lipumba waziri wa fedha na mipango. naibu zitto kabwe ......
 
Awaweke tu!watakua tayr wanajua mashart,ila naona muda si mrefu watz tutabaini yaliyo nyuma ya pazia
 
Kwa Lipumba kuwa Waziri na ZZK kuwa naibu wake is very possible. Binafsi nitaipenda japo hao jamaa wote kwa pamoja waliusaliti upinzani dakika za mwisho, lakini JPM ataweka historia mpya katika!!
 
Back
Top Bottom