Upinzani kufa Tanzania?

Tukumbuke kwenye hivi vyama vya upinzani kuna vipandikizi vingi vya CCM ili vyama vife. Migogoro inayoonekana kwenye vyama vya upinzani ni kule kugundua njama za CCM na sasa wanaamua kusafishana (japo njia wanayoitumia inaweza isiwe muafaka sana)
Ila naamini ndo vinakomaa sasa. CDM naiaminia zaidi
Kwa upande wa pili CCM ndo wana hali mbaya zaidi. badala ya kiutekeleza ilani yao wenyewe, wanagombania kijiti cha 2015 wakati bado kuna miaka 3. Hofu imeshawingia kuipoteza ikulu na hawajajua watajinasuaje kwenye hasira za Watanzania. Mkuu MKUNGA, jarinbu kuwapelekea tiba wenzio japo nina wasiwasi na tiba yako maana hata ugonjwa wao huuoni mpaka sasa. Usije ukawapa sumu tu maana ndo style waliyoanzisha ili wapunguzane.
 
wakati mwingine upuuzi kama huu ndio unaidhalilisha jamii forum.Ukiwa mtumwa wa Nepi unaweza hata kutembea uchi bila kujijua[/QUOTE

Kwenye red,... inaweza kuonekana upuuzi lakini ukweli ni kwamba migogoro inayoendelea ktk vyama vikubwa vya upinzani haihitaji darubini kupima afya ya upinzani nchini. Hii fukuzaa fukuza uanachama inaua vyama. Angalia mf. CCM unadhani wanashindwa kuwakuza watu? Wanaogopa kuleta instability kwani unapomfukuza mmoja anaondoka na kundi lake. Nasisitiza viongozi wa upinzani kubadilika na kuelekeza nguvu zao ktk kukuza na kusaka wanachama na viti zaidi na sio kuvipunguza kwa kufukuzana

Mkuu umesema kweli. Huyu bundi wa migogoro kwenye vyama vya upinzani si mzuri. Nakumbuka kwamba mwaka 1995 NCCR Mageuzi kilikuwa chama chenye nguvu. Mrema alikuwa na mvuto wa kisiasa kuzidi alivyo Dr. Slaa sasa. NCCR Mageuzi ilikuwa na ma Dr. wa kumwaga (Limbu), ilikuwa na maprofessor (Baregu), ilikuwa na wanasheria lukuki (Marando), ilipata wabunge wengi (Chiku Abwao). Chama kilikuwa kinatishia CCM kuelekea uchaguzi wa 1995 na punde baada ya uchaguzi. Lakini bundi wa migogoro akaingialia NCCR Mageuzi wakatimuana na mwisho wake sote tunaujua.

Kinachoendelea kwenye vyama vya upinzani sasa siyo kitu kizuri sana kwa mustakabali wa upinzani hapa nchi. Ni kweli na CCM haiko shwari lakini ni vizuri upinzani ukawa uko shwari na kuchekelea CCM ikilumbana. Sasa malumbano kila mahali. Mustakabali wa siasa za Tanzania uko shakani!

Naona CDM kama imetulia ila sijui kama imetulia kweli au ni cosmetics.

Ni vema upinzani ukaachana na migogoro ili kuimarisha medani ya siasa.
 
Back
Top Bottom