Queen V
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 776
- 1,330
Vyama 10 vya Upinzani leo vimefanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa.
Vyama hivyo vimefanya hivyo leo Januari 27 ikiwa ni miaka 18 tangu machafuko yaliyotokea Zanzibar mwaka 2001 kufuatia madai ya udhalimu wa kisiasa yaliyopelekea mauaji ya watu 46 na majeruhi zaidi ya 600 huku Tanzania kwa mara ya kwanza ikizalisha wakimbizi ambapo watu takribani 2000 walikimbilia Mombasa.
Katika taarifa yao, wameipongeza Kamati ya Bunge kwa kuweza kubadili baadhi ya vifungu ambavyo walivizungumzia hapo awali katika Muswada.
Moja ya mambo waliyopongeza ni kuondolewa kwa hati yenye mashaka kama kigezo cha chama kusitishiwa ruzuku.
Licha ya mabadiliko hayo, wamesema kuwa bado muswada huo unahitaji marekebisho zaidi ikiwemo kupunguzwa kwa Ujinai wa Vyama vya Siasa. Wanaelezea kuwa karibu kila kifungu kina adhabu na ingawa kamati imejitahidi kupunguza lakini bado mkazo unahitajika.
"Haya Mambo kama ugaidi yana Sheria zake, tuyaache yashughulikiwe na sheria zake ili kufanya siasa nchini Tanzania isigeuke kuwa jinai" amesema Salum Mwalim(CHADEMA).
Jambo lingine walilozungumzia ni suala la kukataza vijana kufanya siasa vyuoni. Wamesema hakuna chuo cha siasa hivyo vijana waachwe wajijenge tangu vyuoni na kama kuna haja ya kudhibiti uwekwe utaratibu watakaolazimika kuufuata.
Pia wamemshutumu Katibu Mkuu wa CCM kuwa yuko Dodoma kuwashawishi Wabunge wa chama chake kuyakataa mabadiliko yaliyofanywa na Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ili kusimamia ahadi/dhamira aliyoweka ya muswada kupita kama ulivyo.
Salum Mwalimu amehoji kuwa, kama CCM hawakutaka mabadiliko katika muswada, kwanini Katibu Mkuu na Katibu Mwenezi walienda kutoa maoni mbele ya Kamati.
Amewaasa Wabunge wa CCM kufuata nyayo za wenzao walio kwenye Kamati ya Katiba na Sheria katika kuweka maslahi ya nchi mbele pindi Muswada utakaposomwa mara ya pili na kujadiliwa.