Upinzani historia inawahukumu

Upinzani historia inawahukumu

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
339
Reaction score
677
Leo asubuhi nilipoamka nilikutana na Tweet moja ya Mh. Jakaya Kikwete Rais Mstaafu wa Tanzania. Twitter iliandikwa hivi, ‘’ What a wonderful bird's eye view of our beautiful Mount Kilimanjaro, I was able to capture today February 12th, 2020. I was on a TGFA flight from Nairobi to Dar es Salaam. I have never been this lucky before and I have seen this much snow’’. Chini aliweka over view ya Mlima Kilimanjaro.

Kwenye twitter hii ilichangiwa na watu wengi, lakini Mh Godbless Lema yeye alichangia kwa kuandika maneno haya “That was nice!! I think you also need to take a picture of the real situation of the country at the moment.The political situation of this country need your camera too.We need your voice Sir to work like your iPhone’’. Baada ya kusoma mchango wa Mh Lema pamoja na kuwa nimejibu comment yake, lakini nikapata kichwa cha kuandaa makala fupi ya ‘’UPINZANI TANZANIA HISTORIA INAWAHUKUMU’’.

Ndugu zangu inawezekana wazo la Mh Lema ni jema. Lakini historia inaonyesha upinzani wa Tanzania hauujawahi kumkubari Rais aliyemadarakani. Niwakumbushe tu, Mzee Mwinyi alitukanwa sana na NCCR- Mageuzi ikiongozwa na Mzee MREMA. Mnaokumbuka swala la CHAVUDA mtakubaliana na mimi juu ya Mrema alivyolisaliti Baraza la mawaziri. Lakini leo sizungumzii doctrine of ministerial responsibility.

Baada ya uchaguzi Mrema na wenzake walianza kumtukana mzee Mkapa. Walisema ameficha pesa, ameuza viwanda na mambo kedekede. Enzi hizo kulikuwa na CUF ya Ngangari na NCCR-Mageuzi kabla haijafanyiwa substation na CHADEMA. CUF walijaribu kwenda nje baada yam zee Mwinyi kuwagomea juu ya hoja yao ya yeye kuwakutanisha na Mh Mkapa. Wakati CUF wakizunguka nje ya nchi, mwaka 2001 Mzee Mkapa alitoa kauli nzito, alisema ‘’WABWEKE NJE AU WABWEKE NDANI, SERIKALI ILIYO MADARAKANI NI ILEILE’’. Alitoa kauli hiyo baada ya baadhi ya nchi kutaka kuingilia mambo ya ndani ya nchi.

Wapinzani hawa hawa baada ya JK kuwa Rais walimtukana JK matusi yote. JK hakuwajibu bali aliendelea na kazi. Walimpa majina yote, mara dhaifu, Vascow Da Gama nk lakini Kikwete aliendelea kuchapa kazi na wakati mwingine aliwaita kunywa nao chai Ikulu. Wakati JK kiongozi walisema Mh. Mkapa ndiye bora.

Leo JPM anafanya kazi usiku na Mchana, hao hao waliomtukana JK wanasema JK was excellent. Wanataka JK aongee naJPM. Yaani aliyeitwa Dhaifu aongee na JPM. Historia inawafunga. Inaezekana hoja zao ni nzuri, ila kwa kuwa imejengeka Tabia kuwa kila kiongozi anatukanwa awapo madarakani basi wanajikuta wanakosa msaada.

USHAURI: Upinzani uwe na tabia ya kukukubali baadhi ya mambo, lakini yale wanayokosa ufafanuzi wawe wanaomba kibari cha kuonana na PM au Rais. Rais hawezi kukataa kuzungumza na Mh Mbowe akitumia channel nzuri. Waziri mkuu hawezi kataa kumsikiliza Mbowe. Tukiwa na utamaduni huo nchi itaenda na hatutatunishiana misuli.

Na; Elius Ndabila
0768239284
 
Katiba yetu ndio tatizo. Tanzania inaonekana ni mali ya chama kitakachokuwa madarakani,hata Chadema au CUF ikiwa madarakani itafanya haya haya ya CCM. CCM inaona upinzani ni adui na Chadema au CUF itaona hivyo hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usema kweli serikali ya awamu ya tano ni mbaya mbaya sana ukilinganisha na serikali ya awamu ya nne maana haizingati haki za binadamu, sheria na kanuni za nchi hazifuwatwi bali nchi inaendesha kwa matakwa ya mtu mmoja pia serikali hii iliopo madarakani haina demokrasia kwa ustawi wa nchi yetu bali inaendeshwa kwa maslahi ya chama mbele na kudharau vyama vingine. Serikali hii ya awamu ya tano inahusudu maendeleo ya vitu kuliko maendeleo ya watu tofauti na serikali ya awamu ya nne ambayo maendeleo ya watu yalikwenda sambamba na maendeleo ya vitu chakushangaza serikali ya awam ya nne kulikuwa na mafisadi ila mzunguko wa fedha ulikuwa mkubwa kushinda hii serikali ya awam ya tano
 
The Coolest Jw Coolest Jw Serilaki ya awamu ya nne ilihusika na mauaji ya Daudi Mwangosi tena ushahidi ulikuwepo mchana kweupe na wakina Mbowe walizunguka ughaibu na picha za marehem wakionyesha jesho la police lilivyohusika na mauaji yale.
Pia usije kusahau Dkt Ulimboka pia usimsahau yule mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba aliekakutana na yule gavana wetu kule umaghairibi akataka kutoa siri wakamfyeka. Ndiyo hyo leo mnasema aliheshim haki za binadamu.
 
Leo asubuhi nilipoamka nilikutana na Tweet moja ya Mh. Jakaya Kikwete Rais Mstaafu wa Tanzania. Twitter iliandikwa hivi, ‘’ What a wonderful bird's eye view of our beautiful Mount Kilimanjaro, I was able to capture today February 12th, 2020. I was on a TGFA flight from Nairobi to Dar es Salaam. I have never been this lucky before and I have seen this much snow’’. Chini aliweka over view ya Mlima Kilimanjaro.

Kwenye twitter hii ilichangiwa na watu wengi, lakini Mh Godbless Lema yeye alichangia kwa kuandika maneno haya “That was nice!! I think you also need to take a picture of the real situation of the country at the moment.The political situation of this country need your camera too.We need your voice Sir to work like your iPhone’’. Baada ya kusoma mchango wa Mh Lema pamoja na kuwa nimejibu comment yake, lakini nikapata kichwa cha kuandaa makala fupi ya ‘’UPINZANI TANZANIA HISTORIA INAWAHUKUMU’’.

Ndugu zangu inawezekana wazo la Mh Lema ni jema. Lakini historia inaonyesha upinzani wa Tanzania hauujawahi kumkubari Rais aliyemadarakani. Niwakumbushe tu, Mzee Mwinyi alitukanwa sana na NCCR- Mageuzi ikiongozwa na Mzee MREMA. Mnaokumbuka swala la CHAVUDA mtakubaliana na mimi juu ya Mrema alivyolisaliti Baraza la mawaziri. Lakini leo sizungumzii doctrine of ministerial responsibility.

Baada ya uchaguzi Mrema na wenzake walianza kumtukana mzee Mkapa. Walisema ameficha pesa, ameuza viwanda na mambo kedekede. Enzi hizo kulikuwa na CUF ya Ngangari na NCCR-Mageuzi kabla haijafanyiwa substation na CHADEMA. CUF walijaribu kwenda nje baada yam zee Mwinyi kuwagomea juu ya hoja yao ya yeye kuwakutanisha na Mh Mkapa. Wakati CUF wakizunguka nje ya nchi, mwaka 2001 Mzee Mkapa alitoa kauli nzito, alisema ‘’WABWEKE NJE AU WABWEKE NDANI, SERIKALI ILIYO MADARAKANI NI ILEILE’’. Alitoa kauli hiyo baada ya baadhi ya nchi kutaka kuingilia mambo ya ndani ya nchi.

Wapinzani hawa hawa baada ya JK kuwa Rais walimtukana JK matusi yote. JK hakuwajibu bali aliendelea na kazi. Walimpa majina yote, mara dhaifu, Vascow Da Gama nk lakini Kikwete aliendelea kuchapa kazi na wakati mwingine aliwaita kunywa nao chai Ikulu. Wakati JK kiongozi walisema Mh. Mkapa ndiye bora.

Leo JPM anafanya kazi usiku na Mchana, hao hao waliomtukana JK wanasema JK was excellent. Wanataka JK aongee naJPM. Yaani aliyeitwa Dhaifu aongee na JPM. Historia inawafunga. Inaezekana hoja zao ni nzuri, ila kwa kuwa imejengeka Tabia kuwa kila kiongozi anatukanwa awapo madarakani basi wanajikuta wanakosa msaada.

USHAURI: Upinzani uwe na tabia ya kukukubali baadhi ya mambo, lakini yale wanayokosa ufafanuzi wawe wanaomba kibari cha kuonana na PM au Rais. Rais hawezi kukataa kuzungumza na Mh Mbowe akitumia channel nzuri. Waziri mkuu hawezi kataa kumsikiliza Mbowe. Tukiwa na utamaduni huo nchi itaenda na hatutatunishiana misuli.

Na; Elius Ndabila
0768239284
Umeandika upumbavu, ccm wamechelewesha maendeleo ya Tanganyika kwa miaka 59 sasa,

kama una akili utaelewa
 
Mstari wa mwisho kwenye hoja yako una uzito kuliko maneno mengi ya yasiyo na mantiki. Ilitosha tu kuweka namba yako ya simu na juu yake ukaweka maneno matatu manne ya kusifu, halafu ukakaa pembeni kusubiria uteuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elius W Ndabila ,

..kukosolewa siyo kutukanwa.

..ccm mkiondokana na dhana au imani kwamba kukosolewa ni kutukanwa mtaendesha nchi vizuri sana.

..mnapaswa kutathmini nafasi ya ccm na nafasi ya vyama mbadala ktk mfumo wa demokrasia ya vyama vingi na ushindani wa kisiasa.

..kwenye demokrasia zilizokomaa Raisi na chama chake huwa hawasifiwi na kupongezwa wakati wakiwa madarakani bali wanapokuwa wametoka madarakani.

..lakini wakati ccm mkilalamika kwamba wapinzani hawawasifii hebu jiulizeni ni lini ccm mmepata kusema jambo jema kuhusu wapinzani.
 
Back
Top Bottom