Upinzani DRC kumteua mgombea mmoja Uswisi

Upinzani DRC kumteua mgombea mmoja Uswisi

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,201
Reaction score
64,679
000_1918l3_0_2_0.jpg

Kutoka kushoto kwenda kulia, , viongozi wa upinzani wa DRC Vital Kamerhe, Felix Tshisekedi, Adolphe Muzito, Moise Katumbi na Jean-Pierre Bemba, katika mkutano wa Brussels mnamo 4 Septemba 2018.© AFP/John Thys

Vigogo saba wa upinzani nchini DRC wanatarajia kuteua mgombea mmoja kuelekea uchaguzi wa urais wa Desemba 23 katika mkutano utakaofanyika siku ya Alhamisi huko Geneva, nchini Uswisi, licha ya ya mvutano unaoendelea katika kambi hiyo.

"Hadi tarehe itakayotangazwa, viongozi wote wa upinzani watakutana nchini Uswisi kushiriki katika mkutano wa kuteua mgombea mmoja wa upinzani atakayepeperusha bendera ya upinzani katika ucaguzi wa urais " wa Desemba 23, Freddy Matungulu, mmoja wa wagombea wanne wa upinzani ameliambia shirika la Habari la AFP.

Mnamo Oktoba 26 huko Afrika Kusini, vigogo saba wa upinzani waliahidi kuteua mgombea mmoja kabla ya Novemba 15 kwa ajili ya uchaguzi utakaopelekea kupatikana kwa mrithi wa Rais Joseph Kabila ambaye amekuwa madarakani kwa miaka miaka 18.

"Matarajio ni makubwa kutoka kwa raia, na kama kundi tunategemea ushindi katika uchaguzi wa urais tukiwa pamoja," amesema Matungulu.

"Mkutano wa Uswisi unaweza kuchukua siku tatu," Wakili Peter AFP Kazadi, Naibu mkurugenzi wa wagombea wa upinzani katika uchaguzi wa urais Felix Tshisekedi, kiongozi wa chama cha upinzani cha kihistoria (UDPS ). "Rais Tshisekedi atakuwepo," Kazadi alisema.

Mkutano huu umepangwa kwa tofauti za msingi juu ya matumizi ya mashine za kupiga kura ambazo zinapaswa kuruhusu wapigakura kuchagua mgombea wao na magazeti kura katika vituo vya kupigia kura.
 
Stashangaa kambi hii ikishindwa, ambalo ni jambo la wazi, kuona wanaanzisha vurugu kwa msaada wa walowezi wa mali za DRC.
Ni ukweli usiopingika hawa hawana msingi wa kupata kura huko DRC ndiyo maana shughuli zao wanazifanya chini ya 'uangalizi wa walowezi'.
Hata hivyo nina imani waDRC watakuwa wamepata uwelewa na watawashughulikia kwenye sanduku la kura na ikibidi hata mitaani. Kibaya zaidi kuna chama fulani hapo Tanzania hakijifunzi kutokana na makosa yanayofanywa na kambi hii ya akina Moise Katumbi.
 
Viongozi wengi wa kiafrica wana attitude ya kuamini bila wazungu nchi zao haziwezi kuendelea, ndyo maana kila leo safari za huko haziishi kwenda kuomba msaada....sasa ona hya majinga ya drc yameenda uswiss kwa suala ambalo hta wangekuwa kigoma wangeweza kulifanikisha!
 
Stashangaa kambi hii ikishindwa, ambalo ni jambo la wazi, kuona wanaanzisha vurugu kwa msaada wa walowezi wa mali za DRC.
Ni ukweli usiopingika hawa hawana msingi wa kupata kura huko DRC ndiyo maana shughuli zao wanazifanya chini ya 'uangalizi wa walowezi'.
Hata hivyo nina imani waDRC watakuwa wamepata uwelewa na watawashughulikia kwenye sanduku la kura na ikibidi hata mitaani. Kibaya zaidi kuna chama fulani hapo Tanzania hakijifunzi kutokana na makosa yanayofanywa na kambi hii ya akina Moise Katumbi.
Kwahiyo hao wapinzani ndio vibaraka zaidi kuliko huyo kabila?? Hivi kabila ndani ya miaka 18 amefanya nini la maana la kukumbukwa?? Hao wapinzani wakiungana wanashinda sana tu kama issue ni ukibaraka ni the same case kwa kabila na huyo pandikizi wake aliemuweka kumrithi. Muhimu demokrasia ichukue nafasi yake!!

Alafu pia unaposema Tanzania wajifunze una maana gani?? Ina maana hao wapinzani wa Tz ndio wanatumika na wazungu ila chama tawala ndio hakitumiki?? Kama wapinzani ndio vibaraka unaweza nieleza ni mikataba gani mibovu ya rasilimali iliingiwa na wapinzani?? Unaweza nisaidia kuna ufisadi gani umefanywa na serikali inayoongozwa na upinzani Tanzania??

Kama unachukia vibaraka anza kwanza kupinga hizi serikali uchwara kabla hujaingia upinzani.
 
Alafu pia unaposema Tanzania wajifunze una maana gani?? Ina maana hao wapinzani wa Tz ndio wanatumika na wazungu ila chama tawala ndio hakitumiki?? Kama wapinzani ndio vibaraka unaweza nieleza ni mikataba gani mibovu ya rasilimali iliingiwa na wapinzani?? Unaweza nisaidia kuna ufisadi gani umefanywa na serikali inayoongozwa na upinzani Tanzania??
Ngoja tusubiri maoni ya wengine...ili tuboreshe mjadala.
 
Nguvu ya akina Kabila na huyo kibaraka chake ni kutegemea wizi wa kura kwani hiyo miaka 18 aliyokaa madarakani imeenda bure, hakuna lolote la maana alilofanya na ndio sababu alitaka kung'ang'ania madaraka.

Hao hao mnaowaita walowezi ndio wale wanaowatupia mfupa mgumu uliyowashinda. Africa No Good.
 
Wapinzani nchini DRC bado wanatapata tatizo sio wamoja kivile ,baadhi ni wanafiki hapo

Pamoja na madudu ya JKK lkn bado upande wa upinzani hkn MTU wa kumshinda Shadary ,Congo pia ukabila unaitafuna ,acha mswahili Shadary na JKK wake wachukue nchi kwa Mara nyingine
 
Mmmh usichanganye na kule Congo ya mashariki ,goma ,Kivu,bukavu huko ndiko kuna mapigano

Kinshasa na huko mashariki ni mbali sana
Nilikutana na M-Kasai mmoja. Ana mbwembwe anaonyesha kana kwamba Wakasai ni class ya juu kuliko Wakongo wengine
 
Hahahaha, wa-kasai ndivyo walivyo lkn ndio maskini balaa ,hao wanakula hadi wadudu ,Kasai ndio masikini mno, ingawa wapambanaji sana

Ukiona MTU ana zururazura hovyo huyo Kasai ktk miji kikubwa ,kwa Congo Kasai anadharaulika mno

Congo ukabila upo sana,hasa mluba na mkasai [ wapinzani Hawa]

Jb Mpiana ni Mkasai?
 
Back
Top Bottom