Upimaji wa viwanja 20*20 ni uharibifu wa mazingira

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,595
Upimaji wa viwanja 20*20 unaonekana kuchochea sana uharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa joto sehemu za mijini.

Katika ujenzi kwenye viwanja vya 20*20 ni vigumu kuacha sehemu ya kupanda miti ya kivuli kwa ajili ya utunzaji wa mazingira.

Napendekeza upimaji uanzie 40*40 ili kuwezesha upandaji wa mti ya kivuli na kwa ajili ya utunzaji wa mazingira: Kwa kuwa Tanzania hatuna uhaba wa Ardhi ila kuna msongamano wa watu maeneo ya mijini tuu.

Tatizo sio bei maana bei hizi hupangwa na serekali hivyo huweza kupunguzwa ili vupatikane kwa bei rahisi.
 
Upimaji wa viwanja 20*20 unaonekana kuchochea sana uharibifu wa nazingira na kuongezeka kwa joto sehemu za mijini. Katika ujenzi kwenye viwanja vya 20*20 ni vigumu kuacha sehemu ya kupanda miti ya kivuli kwa ajili ya utunzaji wa mazingira.

Napendekeza upimaji uanzie 40*40 ili kuwezesha upandaji wa mti ya kivuli na kwa ajili ya utunzaji wa mazingira: Kwa kuwa Tanzania hatuna uhaba wa Ardhi ila kuna msongamani wa watu maeneo ya mijini tuu.

Si wote wenye uwezo wa kununua 40*40, 20*20 au 15*15 vikipangiliwa vizuri, miti inaoteshwa bila shida yoyote hasa pembezoni mwa barabara. Kosa lililofanyika ni kugeuza 20*20 kwa kujenga magorofa.
 
Huwa nashangazwa sana na wataalamu wetu wa mipango miji, sijui huwa wanafikiria nn ktk vichwa vyao. 20*20 kwa mpango upi? Ni mambo ya ajabu sana haya! Wataalamu wa mazingira mje mtusaidie kwenye hii mipango miji yetu!
 
Hili huwa nalisema sana. Tatizo la wataalam wetu kukariri mambo ya wakoloni bila kujali uhalisia na mazingira yetu. Kakiwanja mtu anajenga nyumba panakosekana hata nafasi ya watoto kucheza! Ovyo kabisa,
 
hivi hii bei ya kuanzia 7M kwa wastan inapangwa na nani na je kwa mazingira ya kawaida mtanzania wa hali ya chini atapata ardhi kweli?
Mkuu nimenunua kiwanja Mafinga Iringa sq mita 1 tsh 1200 ila ukiulizia kibaha au bagamoyo utaambiwa tsh 4000 au zaidi kwa sq mita 1!!! Ina maana bei inaweza kupungua!
 
Sawa... si unajua mwenye shibe atamjuaje mwenye njaa....
Sio hivyo mkuu nimeenda kisarawe ndani ndani kabisa tena pori ila unakuta viwanja vinauzwa 20*20 baada ya miaka hutakuta mtu kwa maana ni vigum mtu kujenga na kuacha sehem ya kuapanda mtu/miti
 
Hili huwa nalisema sana. Tatizo la wataalam wetu kukariri mambo ya wakoloni bila kujali uhalisia na mazingira yetu. Kakiwanja mtu anajenga nyumba panakosekana hata nafasi ya watoto kucheza! Ovyo kabisa,
Ndo hivyo mkuu hizi scale zipo toka enzi za mkoloni lakini ni kweli tumeshindwa kuadjust na kuweka scale zetu let's high density ikawa sq mita 800?
 
Upimaji wa viwanja 20*20 unaonekana kuchochea sana uharibifu wa nazingira na kuongezeka kwa joto sehemu za mijini. Katika ujenzi kwenye viwanja vya 20*20 ni vigumu kuacha sehemu ya kupanda miti ya kivuli kwa ajili ya utunzaji wa mazingira.

Napendekeza upimaji uanzie 40*40 ili kuwezesha upandaji wa mti ya kivuli na kwa ajili ya utunzaji wa mazingira: Kwa kuwa Tanzania hatuna uhaba wa Ardhi ila kuna msongamani wa watu maeneo ya mijini tuu.
Unalalamika 20 by 20!! ..nenda kwa malkia ujionee15*15 from tegeta to mbagala nyumba nyomi.
 
Bado tuna mapori mengi sana, lakini kupata kiwanja kilicho pimwa ni mtihani, bei per sq meter 1 haina uwiano na vipato vya watanzania wengi, bei ingepunguzwa ili vipimwe viwanja vyenye kuruhu hata kupanda vijimiti vichache vya kimvuli
 
Back
Top Bottom