Upimaji wa mafuta, Flow Meters v/s Deeps Sticks

Shakir

JF-Expert Member
Jul 31, 2012
1,621
1,906
Wadau,

Hapo jana uliibuka mjadala ni kwanini Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vipimo (Weight & Measures Agency) aliamua kusitisha matumizi ya Flow Meter na kuamua kuendelea kutumia mfumo wa Vijiti (Deep Sticks). Hapa ningeomba nifafanue vijiti vinatumikaje na meters zinatumikaje pia ili tujadili kwenye uzi ule wa jana tukijua hivi vitu ni vitu gani.

1. FLOW METERS
Hizi zinakua ni mita tuseme ufanyaji wake wa kazi ni kama zile za Petrol Stations.

1.1 Faida
Faida ya hizi meters ni kua ni rahisi tu kujua kiasi kilichopita kwenye mita maana ndicho kinachosomwa. Haihitaji kujua kabla ya kupitisha mafuta kulikua na balance ya kiasi gani. Kilichopita kwenye mita ndicho kinachosomwa na mita. Tuseme kama kama Mteja alikua na salio la lita 10,000 na mita hii ikapitisha mafuta lita 20,000 basi ukiona zimefikia hizo 20,000 zilizopita ndio hizo hizo zitakazoonyeshwa.

1.2 Hasara
Hasara ya hizi mita ni rahisi kuzichezea. Hata wengi wetu hupenda kulalamika kua tunapunjwa na wenye vituo vya mafuta sababu tu tunadhani wamezichezea. Petrol Stations nyingi hua wanakataa wateja kwenda na vidumu. Sisi wateja hudhani kua sababu ya wao kukataa ni kua kwenye mita zao zinaweza kusoma zimepita lita 5 wakati ukweli kwenye dumu ziko labda lita 3 au 4 tu. Vivyo hivyo pale bandarini huu mchezo una uwezekano wa kutendeka. Kwamba wanaweza kuonyesha umepokea lita 20,000, nawe ukalipia lita hizo 20,000 kumbe ki ukweli zilizoingia ni lita labda 17,000 tu, kisha hizo 3,000 zikawa faida yao.

Iliwahi kusikika huko nyuma kua kuna lorry lilikamatwa bandarini likiwa na mafuta ya wizi, ni lorry lililokua likihusika na kufanya usafi pamoja na kukusanya au kunyonya maji yaliyotuama, lakini siku hiyo likanswa na mafuta. Kwa mfano huu ni hayo 3,000 yanakwenda kuuzwa hapo.

2. DEEP STICK/KIJITI
2.1 Inavyotengenezwa

Hizi hufanya kazi kwa ushirikiano wa Calibration Papers. Ni Kua kila Tank linalotumika kwenye uhifadhi wa Mafuta hupelekwa kwa WMA kulifanyia Calibrations. Kazi hii ya kulifanyia Calibration hufanyika kwa Kutumia Stick Ndefu iliyokaa kama Ruler. Stick huingizwa kwenye Tank kisha mafuta au Maji hujazwa kwenye Tank kwa Vipimo mbalimbali kuanzia kidogo hadi ujazo wa juu wa Tank. Tuseme labda wataanza kujaza lita 1,000 kwenye Tank kisha wataingiza stick na kupima hizo lita 1,000 zimefikiwa wapi kwenye Ruler/Stick. Kisha wataandika kwenye karatasi. Wataongeza zingine 1,000 na kua lita 2,000 na kusoma kwenye stick zimefikia wapi na kuandika kwenye karatsi pembeni. Hivyohivyo mpaka Tank litakapojaa kisha watatengeneza Calibration paper ambayo itaenda sambamba na hiyo Stick/Ruler/Kijiti kwa Tank hilo TU.

2.2 Inavyofanya Kazi
Tank hupimwa kwanza kiasi cha mafuta yaliyopo kwa kutumia hiyo Stick/Kijiti. Kisha baada ya Mafuta mapya kuingia kwenye Tank, hupimwa tena kuangalia mafuta yaliyopo. Tofauti hutafutwa kwa kuchukua vipimo vya mafuta yaliyopo kabla ya kuingia uvitoe kwenye mafuta yaliyopo baada ya mafuta kuingia, na hii yote hufanyika kwa kutumia Kijiti/Deep stick. Tuseme Tank linaweza kua lina mafuta lita 10,000 kabla halijapokea masuta mapya. Kisha baada ya Kupokea mafuta tuseme vipimo vinasoma lita 30,000. Kwa hiyo yaliyoingia ni lita 20,000

2.3 Faida
Faida ya Deeps Stick ni kua kama vipimo hivi vitatu (Stick, paper & Tank) vinakua "Calibrated" ipasavyo na watu wa WMA, basi uwezekano wa kutokoea kuzidisha au kupunjwa ni mdogo.

2.4 Hasara
Hasara zinaweza kua nyingi zaidi kuliko faida.
2.4.1 Too much Manual Works. Hii inahusisha upimaji wa tank kabla ya ku[pokea mafuta na baada ya kupokea ili kutafuta tofauti (yaliyoingia).

2.4.2 Deteriorating of Measures. Tank likititia/didimia kidogo au kupinda basi vipimo hupotea. Karatasi inaweza kufutika na hata hiyo Deep Stick inaweza kupinda au kufutika.

2.4.3 Unexpected Mismatching. Deeps Stick (kijiti) kinatakiwa iendane na Calibration Paper ileile na kwa Tank Lile lile, inaweza kutokea bahati mbaya kuchanganya kimoja katika hivi ikawa shida. Yaani kila Tank lina Stick yake na paper yake ambayo haitakiwi kuchanganyika au kubadilishwa na ingine.

2.4.4 Deliberately (Fraudulent) Mismatching. Uko uwezekano wa mtu kuiba mafuta kwa kufoji either Stick au ile paper

Na-declare interest kua nimewahi kufanya kwenye makampuni ya mafuta kwa zaidi ya Miaka Mitano hivyo nitakachoeleza hapa ni kwa kadri ya uzoefu wangu huo.
 
Ni kwanini "zichezewe"? Si kuna watu wameajiriwa kuhakikisha zinafanya kazi inavyotakiwa? Au ndio hao hao wanaozichezea? Kama ndivyo, basi muhimu wachezewe wao ili taifa lisonge mbele. Kiukweli inatakiwa ifike mahali watu wale vitanzi bila mizaha. Hii ndio dawa pekee ya kumaliza huu upuuzi.
 
Yote ni sawa, tatizo sisi binadamu ujanja ujanja mwingi ndio maana hatuamini hata kimoja, watachezea mashine watahonga watu wafanyao calibration watoe vipimo vya uongo, hivi kwali la jana bandarini EWURA hawahusiki?
 
Mkuu, unachanganya kati ,Dip stick' za kupimia tenki za malori ya mafuta na ( lory tanks) na matenki makubwa ya kuhifadhia mafuta ( Bulk storage Tanks) ambapo tenki hizi hazitumii Dip stick kama unavyodai.
 
Mkuu,
Tanks Kubwa zinatumia kamba, iko kamba futi kamba hizi wanazotumia washona nguo lakini ufanyaji wake wa kazi ni kama tu deep sticks
 
Nilidhani wewe ni guru kwenye mambo ya upimaji, kumbe ulikuwa mfanyakazi tu kwenye kampuni za mafuta. Kwa huo uzoefu wako ungeongeza taarifa kwa kusoma literature nyingine ndipo uandike kitu cha uhakika, maana kufanya kazi kwenye makampuni ya mafuta hakukufanyi uwe mtaalamu wa kujua kipimo kipi kizuri, zaidi unakuwa biased. Sasa kwa haya uliyoandika utatudanganya wengi.
 
Sisi tunataka vitumike vipimo vya kisasa, siyo hizo fimbo, nani atachezea na kwa faida ya nani? hebu wafunge hizo metres afu tuone nani wa kuzichezea...
 
BIASHARA YA MAFUTA NI ........TOTALLY CONFUSING DEPARTMENT......
MSAFIRISHAJI ANAKWIBA...MTEREMSHAJI ANAKWIBA...MUUZAJI ANAKWIBA...MTUMIAJI (DEREFA) NAYE ANAKWIBA...SASAAAA....DAAAAH......
 
Fanya utafiti wa miongozo mbalimbali ya upimaji wa mafuta mengi yaliyotuwama ( static measurements) duniani mfano MPMS
 
Fanya utafiti wa miongozo mbalimbali ya upimaji wa mafuta mengi yaliyotuwama ( static measurements) duniani mfano MPMS

MPMS ( Manual of Petroleum Measurements Standard)
 
Nilidhani wewe ni guru kwenye mambo ya upimaji, kumbe ulikuwa mfanyakazi tu kwenye kampuni za mafuta. Kwa huo uzoefu wako ungeongeza taarifa kwa kusoma literature nyingine ndipo uandike kitu cha uhakika, maana kufanya kazi kwenye makampuni ya mafuta hakukufanyi uwe mtaalamu wa kujua kipimo kipi kizuri, zaidi unakuwa biased. Sasa kwa haya uliyoandika utatudanganya wengi.

Mkuu usibeze presentation yake

The man is good, maelezo yake almost yote nisahihi isipokuwa hiyo stick ndipo kajichanganya.......Hata hivyo nimemkubali.
 
Nilidhani wewe ni guru kwenye mambo ya upimaji, kumbe ulikuwa mfanyakazi tu kwenye kampuni za mafuta. Kwa huo uzoefu wako ungeongeza taarifa kwa kusoma literature nyingine ndipo uandike kitu cha uhakika, maana kufanya kazi kwenye makampuni ya mafuta hakukufanyi uwe mtaalamu wa kujua kipimo kipi kizuri, zaidi unakuwa biased. Sasa kwa haya uliyoandika utatudanganya wengi.
Ha ha ha,
Onyesha basi hata nlipodanganya Mkuu?
Au wapi nimekua biased?
Sijataka taarifa za ku-google kisha niwaletee hapa, nimeeeleza nachokifahamu maana watu wengi hudhani hivi vijiti labda ni primitive au local ways za kupima mafuta.

Kwa taarifa tu ni kua hata gari zikienda kujaza kwenye Depots za makampuni zilizoko kurasini huhakikisha mafuta yao kwa hizi deep sticks. na vilevile wenye Petrol Stations wakiwa wanashusha mafuta kutoka kwenye magari nao hutumia hizi sticks
 
Nilidhani wewe ni guru kwenye mambo ya upimaji, kumbe ulikuwa mfanyakazi tu kwenye kampuni za mafuta. Kwa huo uzoefu wako ungeongeza taarifa kwa kusoma literature nyingine ndipo uandike kitu cha uhakika, maana kufanya kazi kwenye makampuni ya mafuta hakukufanyi uwe mtaalamu wa kujua kipimo kipi kizuri, zaidi unakuwa biased. Sasa kwa haya uliyoandika utatudanganya wengi.
At least hata ujaribu kushukuru kile alichokieleza. Unaongea lugha kama vile ya kum - discourage, lengo lake ni kukuza uelewa wa walio wengi, japo katika uhalisia kuna wanaomzidi katika maarifa ya kile alichokieleza kwa urefu.
 
Hapa wafanyabishara wanafanya mhezo tu kulazimisha serikali iendelee kutumia stik,huu ni wizi tu hakuna kingine,teknolojia hiyo ilikuwa inatumika karne ya 19 zamani sana,
hakuna nchi inayotumia style hiyo katika wakati huu tulionao,
kuna meter ambazo hufungwa na nchi nyingi wanatumia kama hizo wanazodai zinawapunja ndio sahihi kabisa,
ukitaka kujua kama kulikuwa na mchezo mchafu pale kwanini wameanza kuzirekebisha baada ya kujua waziri mkuu anakwenda pale?
wanarekebisha na kuanza kuzifanyia kazii za nini wakati wateja wao wanadai walishazikataaa?
hapa ukitazama mchezo unachezwa na wote kuanzia watumishi wa serikali na wafanyabiashara
 
Nilidhani wewe ni guru kwenye mambo ya upimaji, kumbe ulikuwa mfanyakazi tu kwenye kampuni za mafuta. Kwa huo uzoefu wako ungeongeza taarifa kwa kusoma literature nyingine ndipo uandike kitu cha uhakika, maana kufanya kazi kwenye makampuni ya mafuta hakukufanyi uwe mtaalamu wa kujua kipimo kipi kizuri, zaidi unakuwa biased. Sasa kwa haya uliyoandika utatudanganya wengi.
Guru wa kuponda tu...........andika unachokijua tuone
 
Nilidhani wewe ni guru kwenye mambo ya upimaji, kumbe ulikuwa mfanyakazi tu kwenye kampuni za mafuta. Kwa huo uzoefu wako ungeongeza taarifa kwa kusoma literature nyingine ndipo uandike kitu cha uhakika, maana kufanya kazi kwenye makampuni ya mafuta hakukufanyi uwe mtaalamu wa kujua kipimo kipi kizuri, zaidi unakuwa biased. Sasa kwa haya uliyoandika utatudanganya wengi.

Mbona ni rahisi sana kuelewa? kupima kwa mtambo kuna uhakika zaidi ya uwezo wa kibinadamu. Hakuhitaji kukwambia kama aauzoefu wa kazi hiyo ndo uamini, hii iko wazi kabisa....

Suluhisho ni kuweka automated meters ambazo zinatunza kubukumbu zenyewe, na pia zina peleka kubukumbu kwenye kompyuta maalum, na siku hizi komputa hiyo uyaweza hata kuwa mbali kabisa; Ikulu au ofisi ingine yoyote kwa jinsi technoligia ilivyosonga mbele.

Matukio yote yaweza kurekodiwa; ujazo, tofauti ya msukumo(pressure) na kama kuna tukio lolote lisilo la kawaida. Na hizi zaweza kufanyuiwa calibration na kutompunja au kumwongezea yeyote.

Kuna makusudi yalikuwa yanafanyika na kutajirisha watu kwa kafara, imagine zaidi ya miaka mitano watu wanapata mnafuta kupitia mabomba ya pembeni, hizo si pesa za kusimamia uchaguzi zatosha!!!!
 
Ni kwanini "zichezewe"? Si kuna watu wameajiriwa kuhakikisha zinafanya kazi inavyotakiwa? Au ndio hao hao wanaozichezea? Kama ndivyo, basi muhimu wachezewe wao ili taifa lisonge mbele. Kiukweli inatakiwa ifike mahali watu wale vitanzi bila mizaha. Hii ndio dawa pekee ya kumaliza huu upuuzi.
Kabisa mkuu
Hapo umenena
 
Back
Top Bottom