Upigaji kura wa Rais, wabunge na madiwani 2020

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Hamjambo wanajamvi. Ni matumaini yangu kuwa hamjambo mkiendelea vema kabisa na majukumu ya hapa na pale.

Leo 27-1-2017 wazo limenijia juu ya vitambulisho vya kupigia kura ktk uchaguzi mkuu wa 2020 wa rais,wabunge na madiwani.

2015 zilijitokeza changamoto za hapa na pale ktk upigaji wa kura ikiwemo na watu kulazimika kurudi sehemu waliyojiandikisha ili kupiga kura.

Hali hii iliwawaia vigumu wanafunzi wa vyuo vikuu kupiga kura kutokana na kutokuwepo kwenye maeneo yao waliyojiandikisha.

Twende sawa na title ili kukidhi upigaji kura 2020.
Tume ya uchaguzi ya Taifa(NEC) imejipangaje juu ya namna wananchi watakavyopiga kura ukizingatia kuwa wananchi hawapo tena kwenye maeneo(baadhi) waliyojiandikisha. Serikali isisubiri mpaka muda wa uchaguzi ufike ndiyo ianze kutapaTapa kutafuta namna ya kuwawezesha wananchi wote waliojiandikisha kupiga kura.

Wewe mwanajamii forum yapi mapendekezo yako kwa tume ya taifa ya uchaguzi juu ya upigaji kura kwa wananchi wote waliojiandikisha?

Maoni yako ni ya msingi sana katika kuhakikisha kuwa Tume ya uchaguzi ya Taifa inawapa fursa wananchi wote kupiga kura.
Karibuni tujadili pamoja.
Nawasilisha.
Rais2020
Rais wa mioyo ya watu.
 
UANDIKISHAJI AU UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA-1

Baada ya kujifunza baadhi ya mambo kuhusu uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani uliofanyika Januari 22 mwaka huu katika jimbo la Dimani na kata 20 za Tanzania Bara, hebu tuanze kuangalia kwa undani dondoo za msingi zinazoijenga elimu ya mpiga kura kwa ujumla.

Tunapozungumzia elimu ya mpiga kura tunalenga kumuwezesha mpiga kura kutekeleza kwa usahihi na kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu jukumu la msingi la kupiga kura ambalo linapatikana katika mchakato mzima wa Uchaguzi.

Uandikishaji wa wapiga kura au Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura, ni katika hatua za awali za mchakato wa Uchaguzi.Uandikishaji uhusisha kuingiza majina na taarifa za watu waliotimiza sifa za kuwa wapiga kura kwenye orodha maalumu (daftari).

Uboreshaji ni mchakato wa kuingiza majina mapya ya watu waliotimiza sifa za kuwa wapiga kura, kuondoa majina ya watu waliopoteza sifa za kuwa wapiga kura kutoka kwenye orodha ya awali na kurekebisha taarifa za wapiga kura ili waweze kupiga kura kwa mujibu wa Sheria na Kanuni.

Wanaohusika katika uboreshaji ni wananchi wote waliotimiza umri wa miaka 18 na kuendelea ambao hawakuwahi kuandikishwa na wote waliojiandikisha awali ambao wamehama kata au jimbo moja kwenda lingine.

Uboreshaji pia unajumuisha kuondoa majina ya watu wote waliofariki; kufanya marekebisho ya majina yaliokosewa wakati wa uandikishaji na kutoa kadi mpya kwa wale waliopoteza au kuharibu kadi za kupigia kura.

Katika kutekeleza jukumu la uboreshaji wa daftari Tume hushirikiana na watendaji ambao huteuliwa kwa kuzingatia Kifungu cha 7A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura namba 343 na Kifungu cha 10 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura Namba 292.

Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lilianzishwa chini ya Ibara ya 5 (3) (a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, iliyolipa Bunge mamlaka ya kutunga Sheria ya kuanzisha Daftari hilo na kuweka utaratibu wa kurekebisha yaliyomo katika daftari hilo.

Vifungu vya 11, 12 na 15 (5) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na kifungu cha 15 B cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 pia vinaeleza kuhusu Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hutekeleza jukumu la uboreshaji au uandikishaji wa Wapiga Kura chini ya Ibara ya 74 (6) (a) na (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kupitia Ibara hiyo Tume inawajibika kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura wapya waliotimiza umri wa kuandikishwa kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na Kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

Kwa kuzingatia kifungu cha 15 (5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume inatakiwa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili kati ya Uchaguzi Mkuu mmoja na uchaguzi unaofuata.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilianzisha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kwa mara ya kwanza mwaka 2004 kwa lengo la kuandikisha kila raia mwenye sifa za kupiga kura na kutunza taarifa zake kwenye daftari hilo.

Uanzishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulienda sanjari na matumizi ya teknolojia ya ukusanyaji wa taarifa za Wapiga Kura pamoja na uhifadhi wa taarifa hizo kielektroniki.

Teknolojia iliyotumika wakati wa uanzishaji wa daftari hilo kwa wakati huo ilikuwa ni ya kutumia Fomu maalumu za “Optical Mark Recognition” (OMR) ambayo ilihusisha matumizi ya Kamera za “Polaroid” zilizokuwa zinatoa picha za papo kwa hapo kituoni.

Taarifa za kibaiolojia za Wapiga Kura zilizochukuliwa wakati huo zilikuwa ni picha, saini na alama ya dole gumba ya mpiga kura ambazo ziliwekwa katika Fomu hizo na kusomwa na “scanner”.

Awamu ya pili ya Uboreshaji ilifanyika mwaka 2009 ambapo Tume ya Taifa ya Uchgauzi ilitumia “Digital Registration Kits” kutokana na matumizi ya Kamera za “Polaroid” kusimamishwa kote duniani.

Hata hivyo, kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa matumizi ya teknolojia hizo pamoja na zile za kimfumo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ililazimika kutumia teknolojia nyingine.

Teknolojia hiyo ilitumika ili kusaidia kuondoa na kukabiliana na changamoto za kiteknolojia na kuwezesha kuwepo kwa daftari sahihi na linaloaminika zaidi na wadau.

Kuwepo kwa Daftari sahihi la Wapiga Kura linaloaminiwa na wadau ni kigezo muhimu cha kufanikisha chaguzi huru, wa wazi na wenye kukubalika na wa haki zaidi.

SOURCE: Gazeti la Mwananchi la tarehe 25/1/2017.
 
kiukweli mimi Binafsi hata sioni umuhimu wa kupiga kula maana tume inafahamika iko upande gani sasa naona kama wanapoteza pesa tu. juzi juzi mkubwa kateua viongozi wapya kwenye tume, hivi hata wewe ukiulizwa nani atashinda 2020 utakosa? mimi kupiga kura yangu tena mpaka miaka tume itakapokuwa huru
 
kiukweli mimi Binafsi hata sioni umuhimu wa kupiga kula maana tume inafahamika iko upande gani sasa naona kama wanapoteza pesa tu. juzi juzi mkubwa kateua viongozi wapya kwenye tume, hivi hata wewe ukiulizwa nani atashinda 2020 utakosa? mimi kupiga kura yangu tena mpaka miaka tume itakapokuwa huru

Usiache kupiga kura yako aiseee utampunguzia ushindi mgombea wako! Tume ya Kenya ni Tume Huru lakini ona wananchi wanavyopiga kelele hawaiamini tena sijui hapo vipi
 
Nami natabiri kupungua kwa idadi ya wapiga kura 2020 jambo siombei itokee hivyo.shida ya wananchi wengi ni uhalali wa refa anaechezesha mechi ya simba na yangu huku akiwa ni mwanachama damu damu wa yanga unategemea matokeo gani hapo?
 
Usiache kupiga kura yako aiseee utampunguzia ushindi mgombea wako! Tume ya Kenya ni Tume Huru lakini ona wananchi wanavyopiga kelele hawaiamini tena sijui hapo vipi
Me huwa nashangaa sana viongozi wa Afrika ujue kiongozi ukichaguliwa na idadi kubwa ya wananchi na wote wakaridhia ushindi wako hata kuwatawala utawatawala vizuri kwani nao watakuonyesha ushirikiano. lakini ukipita kwa mazingaombwe utaongoza ndio lakini utapambana na changamoto nyingi sana kila utalofanya hawawezi acha kukukosoa na kweli litakuwa na dosali pia ogopa mawazo ya watu wengi huwa wanaibua mambo ya kushangaza. sasa nashangaa hata yule raisi wa Gambia watu waliowengi hawakutaki ila wewe unataka tumia mabavu duuuhhhh
 
unachoona kama zilikuwa changamoto ktk uchaguzi uliopita, kwa wengine zilikuwa ni fursa kupata ushindi. kuna hisia kuwa fursa hizo ni mtokeo ya mikakati iliopangwa vizuri kufanikisha malengo. kwa 2020 usiharakishe, u cross the bridge when u reach it.
 
Kuwepo kwa Daftari sahihi la Wapiga Kura linaloaminiwa na wadau ni kigezo muhimu cha kufanikisha chaguzi huru, wa wazi na wenye kukubalika na wa haki zaidi.

Issue ni process nzima na msimamizi wa process hiyo na wala si vinginevyo wala kuangalia vipande vya process nzima.
 
muda ukifika watarekebisha tuu, sasahivi wanashughulikia kero za watanzania kwanza hayo mambo ya daftar la wapiga kura ni mapema sana kulilalamikia, si ndiyo kwanza tu juzi kati tumetoka kwenye uchaguzi.
 
Issue ni process nzima na msimamizi wa process hiyo na wala si vinginevyo wala kuangalia vipande vya process nzima.

Nini maoni yako sasa! Unataka Tume huru kama ya Kenya siku ukiipata unaanza kulalamika na kuandamana kudai sio huru tena? Wanadamu chenga sana nikiangalia mapichapicha ya Walibya sina hamu bora Tume iendelee hii hii mi naona inafaa sana Uhuru wa Binadamu ukizidi sana anakua kichaaa.
 
Hamjambo wanajamvi. Ni matumaini yangu kuwa hamjambo mkiendelea vema kabisa na majukumu ya hapa na pale.

Wewe mwanajamii forum yapi mapendekezo yako kwa tume ya taifa ya uchaguzi juu ya upigaji kura kwa wananchi wote waliojiandikisha?

Maoni yako ni ya msingi sana katika kuhakikisha kuwa Tume ya uchaguzi ya Taifa inawapa fursa wananchi wote kupiga kura.
Karibuni tujadili pamoja.
Nawasilisha.
Rais2020
Rais wa mioyo ya watu.
Maoni yangu
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...
 
Back
Top Bottom