Upi ukweli kuhusu hizi fununu?

Upi ukweli kuhusu hizi fununu?

Kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia kuwa wanawake ni wengi kuliko wanaume hapa duniani, kln sijawai ona wala sikia ni lini na wapi iliwai fanyika Sensa ya utambuzi huu, aidha sijabahatika kuiona na kuisoma takwimu yoyote inayothibitisha jambo hili.

Nimalizie tu kwa kukubali usemi usemao: kutotambua kwako uwepo wa jambo fulani haina maana kuwa jambo hilo usilolitambua wewe ni kwamba halipo, kwa heshima na tahadhima napenda kujuzwa juu fununu hizi kama zinaukweli wowote kwa fact zilizoshiba na sio blabla tu vijiweni.
Karibu.
Mfano ni nchi yako ya Tanzania, sensa ya mwaka 2012 mikoa miwili tu wanaume ndiyo wengi kuliko wanawake. Nayo ni Manyara na Njombe. Mikoa mingine yote wanawake ni wengi kuliko wanaume. Tafuta kitabu cha sensa au ingia mtandaoni utaona hili nalosema.
 
Back
Top Bottom