Upi hasa ufisadi wa Lowassa?

Upi hasa ufisadi wa Lowassa?

Mimi naamini kwamba tuliimbishwa kweli na vyombo vya habari wimbo unaosema "EL ni fisadi" na sisi tukauimba bila kujua maana yake.Sio siri kwamba unachokiamini ni matokeo ya unachokisikia hasa kama kitu hicho unakisikia mara kwa mara.Sasa naamini kwamba Lowasa sio fisadi kama tulivyoaminishwa.Nadiriki kusema kwamba hata kama Lowasa ni fisadi,ufisadi wake ni bora kuliko wa wengi walioko CCM.

Kuna nyimbo nyiingi mkuu tulikuwa tukiimbishwa enzi zile...Banda wa malawi ni jitu baya sana...jomo kenyatta ni linyan'gau...idd amin dada ni joka kuu jitu katili sana..but.was it true...nenda nchi hizo mkuu ufanye research kidogo tu utaona hao marais ndo waliokuwa wanapendwa sana na wananchi wao wakati ule...kinachotokea ni media feed toka kwa viongozi wetu hasa kutokana na kuhitilafiana na pia chuki za kimaendeleo...ili kujisafisha ni lzm kuwepo na watu watakaosanua ukweli..now we know EL sio fisadi bali ni feeds tulizolishwa na wabaya wake..hasa wa kisiasa kwa manufaa yao binafsi!
 
Siasa ni game inayohitaji akili, ccm km mazuzu wamebadilishana dhahabu na vipande vya chupa...
 
Kwa nini mmeshindwa kumtetea kwa ID zenu zilizozoeleka badala yake mnatumia zile za akiba?

Acheni unafiki, mbona hamkumhoji Slaa alipoitaja ile orodha maanake alisema ushahidi anao?

Mbona Mbowe aliposema anashangaa fisadi Lowassa yupo mtaani ilhali vibaka wanachomwa moto mlikuwa mnakenua tu?.

Nyie jamaa hata hamueleweki mnachokisimamia ni kipi hasa?

Msitufanye wote wajinga humu mazee.

Lazima mlipe gharama za uropokaji wenu.

Sasa ndo ueleze huo ufisadi wake , acha blah blah
 
Awe fisadi asiwe fisadi maadamu anashiriki kuiondoa serikali ya magamba nampa kura yangu asubuhi na mapema kama ni fisadi anapiga lifisadi jingine shida ni nini. Mimi hata kama ni mbwa inaongoza mapambano ya kuiondoa CCM madarakani nitampigia mbwa kura siyo CCM. Kwangu mimi kuiondoa CCM ni jambo la kipaumbele kuliko lolote maadam si kwa VITA hata haje mfungwa wa kesi ya ugaidi maadamu ana ajenda ya kuiondoa CCM nitampa kura yangu
 
Kama huo wa kutaka madaraka kwa njia yoyote ata kwa kukana chama chako!,kujiwekea wanamikakati na kuuhakikishia umma kwamba yeye ndio alistahili kwenye kura ya maoni...hakika amekuwa agaist na desturi na malezi ya CCM aliyokuzwa nayo,ila katabia kakazidi kuwa balaa kama hayati alivyotaadharisha!..all in all CCM mbele kwa mbele!
 
Back
Top Bottom