Nimekuwa nikijiuliza na kuuliza raia wenzangu wengine bila kupata majibu yaliyonyooka.
Ufisadi wa Lowassa ni upi hasa? Wengine ukiwauliza wanajibu we hujui kila mtu anajua, wengine wanasema hujui Richmond? Wengine wanasema ni tajiri sana yule kaupataje utajiri?
Binafsi naona raia mwenzetu hatendewi haki, ndiyo maana mwenyewe kashasema mwenye ushahidi aende mahakamani vinginevyo nyamaza.
Nami naendelea kujiuliza mtu ambaye ameshadidiwa ufisadi na pande zote chama tawala na upinzani kwa nyakati tofautitofauti kiasi ya kwamba hata mtoto aliyezaliwa miaka 8 imepita sasa labla yupo darasa la pili naye anaaminishwa kuwa Lowassa ni fisadi lakini yupo huru hatuoni hapo kuna tatizo. Mtu ambaye hadi bungeni amekuwa na cheo nyeti tu, hivi nchi hii wenye sifa mbaya ndiyo tunawapa vyeo au kinyume chake.
Naelekea kuamini Lowassa anaonewa kwasababu maalum. Na kwakuwa sasa ni mgombea kupitia upinzani basi ndiyo itakuwa shida kubwa. Wanaomnanga wajitokeze kutuelekeza nini hasa ufisadi wake?
Watu wengi wameimbishwa wimbo na kukubali kuuimba bila kujua maana ya maneno ya wimbo. Sasa tutafakari vizuri siasa za namna hii.