Upepo Wa Tanganyika Kung'oa Wabunge Wengi CCM 2015

Upepo Wa Tanganyika Kung'oa Wabunge Wengi CCM 2015

Wa Mjengoni

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2010
Posts
480
Reaction score
128
Awali ya yote nampongeza Mh.Mbunge Lembeli kwa kujitambua na kuona mbali kuna upepo wa serikali tatu ili izaliwe Tanganyika unaoelekea kuwang'oa Wabunge wengi wa Chama Tawala 2015.

Kangi Lugora, Lembeli na wengineo wachache wamesoma upepo unakoelekea huku uraiani kwa jinsi Wananchi wanavyoingoja kwa hamu Tanganyika yao na wameamua kuwa upande wa waajiri wao yaani wananchi. Kwa hili ni wazi kwamba kwa Wabunge wa aina hii watapita kwa kishindo bila kujali watakuwa CCM, upinzani au wagombea binafsi, watasaidiwa na kitu TANGANYIKA KWANZA vyama baadae.

Kwa kura ya wazi watakwenda kinyume na wananchi na wataonekana wazi. Watawafurahisha viongozi wao wa chama lakini wakati huohuo wakisahau kuna upepo halisi uliopo unaosababishwa na kukosa hoja zenye mashiko kwa nini tuendelee na muundo uleule ulioshindwa kutatua kero kwa miaka kadhaa.

Ni bora wangekubali kura ya siri imani ya wananchi kwao ingebaki vilevile bila risk ya kupotea.Kilichofanyika sasa ni kama Jenifa Mgendi, msanii nyimbo za injili alivyoimba - ​ Shimo umelichimba mwenyewe (kura ya wazi) na utatumbukia mwenyewe.... Let us see!
 
Back
Top Bottom