Upepo na hewa ni kitu kimoja au vitu tofauti?

Upepo na hewa ni kitu kimoja au vitu tofauti?

Cascos

New Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
0
Reaction score
198
Fid Q aliwahi kusema maneno haya kwenye mojawapo ya nyimbo zake, "Ni vema kujifunza mengi sio kujua kila kitu" na mie kwa kulitambua hilo ningependa kujuzwa kuhusu upepo na hewa.

Je, ni kitu kimoja au vitu tofauti? Nini chanzo cha upepo na hewa?
 
Mi nadhani ni hicho hicho ila maelezo ni tofauti kwa sababu hiyo hewa bila huo upepo huwezi ipata
 
Upepo ni hewa isiyotulia na huenda kwa kasi.

Hewa ni upepo mwororo inayozunguka na kutulia na huvutwa na viumbe hai.

Chanzo: kamusi sanifu ya kiswahili 2016.
 
Hewa ni oxygen,nitrogen,carbondioxide e.t.c lakini upepo ni hewa iliyo katika mwendo!
 
Lakini tukiangalia binadamu huwa anavuta hewa sio upepo, iweje upepo na hewa iwe ni kitu kimoja mkuu?
Upepo ni hewa inayotembea kwa kasi kutoka sehemu kuliko na mgandamizo mkubwa kuelekea sehemu kuliko na mkandamizo mdogo.
Hewa ni pale inapokuwa haitembei
 
Upepo hupimwa kwa kutumia vifaa kama anemometer na wind vane kuangalia mwendo na uelekeo.
Hewa ni mchanganyiko wa gesi kama oksijeni, naitrojeni na nyinginezo, kwa hiyo ukitaka kupima hewa itabidi upime gesi moja kama gesi, mfano kipimo cha gesi ya oksijeni ni kuamsha moto, kipimo cha gesi ya haidrojeni ni sauti ya muziki pop
 
Hewa ni mchanganyiko Wa gesi mbalimbali katika tabaka la anga (Atmosphere), Mara zote hewa ni mchanganyiko Wa gesi sifuatazo; 78% nitrogen, 21% oxygen, 0.9% argon, 0.04% carbon dioxide, na kiasi kidogo kabisa cha gesi mbalimbali.Pia kuna asilimia 1% ya mvuke (vapour)
kwa maana hiyo, Hewa inapotembea (flow) Hutembea kutoka ukinzani mkubwa kwenda ukinzani mdogo, lile tendo la Hewa kutembea huitwa UPEPO, Kwa lugha rahisi naweza kusema, Upepo si lolote si chochote Bali ni Hewa iliyo kwenye Mwendo;
na Upepo unapotokea umechanganyikana na maji huzalisha Mvua.
ndiyo maana Ogopa sana mtu kukufananisha na UPEPO,
NOTE;Upepo ukiwa Mkubwa zaidi kiasi vumbi huitwa kimbunga, pia kimbunga kinapokuwa kikubwa kiasi cha kusukuma mrundikano Mkubwa Wa Maji kama baharini n.k huitwa TUFANI.
=====================
Kipindi cha Leo naomba, niishie hapa
 
Upeopo ni hewa inayofukuzwa na kimbunga, ni kama baba Jesca, yeye ndo Rais lakini dada mrembo wa US anamfanya apaone Ikulu pa moto.
 
Back
Top Bottom