Upepo Mpya Uvumao Kiaina: CCM Mpoooo!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upepo Mpya Uvumao Kiaina: CCM Mpoooo!!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SHIEKA, Apr 13, 2012.

 1. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,135
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Baada ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki niliuona huu upepo. Ukizingatia jinsi ccm walivyojiweka sawa kwa nguvu nyingi za kisiasa kwa kutumia ushawishi wa wanasiasa wakongwe wa nchi hii, halafu wakafunikwa chini kwenye matokeo mtu mwenye akili unaogopa na kushangaa hiyo nguvu ya kuiangusha ccm imetoka wapi. Lakini huo ndo upepo mpya ulioanza kuvuma kanda ya kaskazini (Kilimanjaro, Arusha). Upepo huu ni ujumbe ulioandikwa kwa herufi kubwa kuiambia ccm kwamba:

  1.Watu wengi wameshaanza kuzichoka sera za ccm.
  2.ccm imekuwa chura wa kisimani anayepiga kelele lakini maji yanaendelea kuchotwa ovyo(Tazama ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya serikali)
  3. ccm inahubiri kunywa maji ilhali wao wanakunywa mvinyo na wananchi wengi wanaliona hili
  4.Wimbi la kuwaondoa wabunge wa Chadema waliochaguliwa 2010 kwa visingizio mbalimbali linaongozwa na ccm.

  Kwa hiyo:

  1.iwapo ccm itafanikiwa kuwaondoa wabunge wa chadema, wasijiingize kwenye uchaguzi mdogo, wataaibika sana sana: watakaab uchi (kwa kiswahili cha mtaani).Ubunge wa Arushs mjini kwa mfano, hata ccm ikapata mgombea toka mbinguni, atapigwa chini tu kwa kadri upepo ulivyo.
  2.ccm ikae chini ipime upepo ulivyo na nguvu kisha wajirekebishe haraka angalau kabla ya 2015. Waanze seriously na ripoti ya CAG.Hii ripoti ina madudu ya ajabu ya kumpa mtu kifafa
  3. ccm iache kubeza na kudharau wapinzani. It's a force to reckon with!
  4.Mkiendelea kupuuzia na kudharau kama ilivyo kawaida yenu, ITAKULA KWENU VIBAYA SANA

  MUNGU BARIKI TANZANIA!
   
 2. s

  slufay JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,372
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Itakula kwako sisiem ina wapiga mpaka porini nyie mtaambulia mjini tu tena kura twagawana
   
 3. d

  dada jane JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jipe moyo ndugu. Hata Keneth Kaunda alijipaga sana matumaini. Matokeo yalimkuta yupo kucheza gofu.
   
 4. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,982
  Likes Received: 1,880
  Trophy Points: 280
  time will tell. hata mbuyu ulianza kama mchicha
   
 5. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,771
  Likes Received: 6,104
  Trophy Points: 280
  Ukiona kiongozi wa kawaida wa chama cha upinzani anaweza kusimama hadi vijijini akakusanya maelfu ya wananchi akamwaga sera na akakubalika basi tambua hizi ni ENZI MPYA.

  Juzi Wenye alikuwa Bunda akinadi sera za chama chake kwa maelfu ya wanavijiji waliohudhuria. Huko Njombe yanafanyika hayo hayo na maeneo mengi nchini.
   
 6. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kwa karne hii kama unaipenda ccm utakuwa taahira
   
 7. M

  MgungaMiba JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2012
  Joined: Aug 28, 2011
  Messages: 890
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 80
  Arumeru wapiga kura wake wengi wako porini, lakini mbona sisiem yako imelia Mzinga?
   
 8. P

  Praff Senior Member

  #8
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ccm has no longer life.
   
 9. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Magambaz wamekufa na ukiipenda magambaz inabidi ukapimwe akili.
   
 10. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  Very soon ccm will become an opposition party, wamekuwa wakisurvive through ballot rigging, ni wataalam sana wa kuiba kura, na hatari waliyonayo ni kuwa watanzania wameamka kama arumeru kijijini wamelinda kura zao wa mijini hatutakubali tena kuibiwa kura zetu na apo kiamahence kifo cha ccm kitakuwa bayana
   
 11. m

  mwanakidagu JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 208
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapo porini wapiga kura hao ni jamii ya wasira wanaoishi porini au)?
   
 12. m

  mwanakidagu JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 208
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mbona mleta hoja ana onekana ni gamba lililolainishwa kwa mafuta.ati unaonesha huruma kwa ccm.kwamba wasipojipanga imekula kwao.inanikumbusha kuhusu vita ww2.pale pearharbour?.wanajesh wa kimarekani siku hyo jumapili walikuwa wakitanua na vimwana na wiskey na nyama na nk.taarifa ikaja toka radar comand sector ya kuwa kuna ndge inakuja.tena si chata yetu.walivyolewa.na utamu wa maraha,walipuuza onyo.mara muda mfupi tu japani ilitupa makombora mazito yaliyo kiangamiza kikosi kizima na kuzamisha manoari zao.nahoji upo wapi ule mtaji wa kura 5milion wa ccm?.wa mzee makamba.uko wapi ule msemo wa hv ni vyama vya msimu iliyotoka magogoni huku moshi wa hasira ukitoka mapuani mwa mtoa kauli.kama japan pale pearhabour,ccm hamna chenu.
   
 13. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 650
  Trophy Points: 280
  hakuna kitu kinanichefua kama wabunge wa chama tawala kupiga kelele za ndiyooo hata kwenye marekebisho ya maana. Wanaonyesha ni kiasi gani chama ni cha wezi au mambumbumbu. Inaudhi sana na nadhani 2015 itawapunguza wengi wa kutosha.
   
 14. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 650
  Trophy Points: 280
  zalikuwa zamani ndugu yangu. Not now days
   
Loading...