Upendo wa watanzania kwa JPM kulingana na ushabiki wa vyama vya siasa.

Halord

JF-Expert Member
May 1, 2016
213
105
Kwa kufuatilia katika mitandao ya kijamii na na katika makundi ya watanzania baada ya uchaguzi wote wamevutiwa na utendaji wa raisi Magufuli.
Upendo huu umegawanjika katika makundi mawili na unaonekana pale raisi anapofany kitu ambacho kinakua na utata kisheria kama ifuatavyo.
1. Kundi la kwanza ni wanachama.na mashabiki wa CCM ambao hawa wanamsifia tu hata hata kama anachofanya nikinyume na katiba ya nchi.
2. Kundi la pili ni la washabiki wa vyama vingine ambao hawa humsifia pale tu anapofanya kitu kizuri na kumkosoa pale anapofanya kitu wanacho ona sio sahihi.
Makundi haya mawili kwa sasa yanatengeneza mipaka kiasi kwamba kuchukiana na kutukanana kama tunavyo ona kwenye miatandao ila tatizo kubwa wote hakuna kundi lenye ushawishi kwa raisi JPM kitu kinacho fanya makundi haya yaendelee kuhasimiana. Kwa ushauri wangu nadhani sisi tuliopo humu JF kwakuanzia tutoe haya mahaba ya vyama vyetu vya siaasa ili tuelimishanae ukweli na uhalisia juu ya mustakabali wa nchi yetu. Nasisitiza hili tulione kwakua vyama na uongozi vinabadilika huku nchi na wana nchi tukibaki palepale.
Pia haya maneno mawili ya kisiasa ya TAWALA na UPINZANI yasitutenganishe kiasi hiki. Katiba yetu inaruhusu chama chochote kushinda na kuwa chama tawala au kikishindwa kuwa chama cha upinzani. Pia tusisahau kushabikia vyama vyama vya siasa ni sawa na kushabikia timu za mpira tusijenge uelewa mbaya maana washabiki wa vyama vya upinzani ndi ndugu zetu na kiuhalisia wote tunatetea nchi yetu moja Jamhuri ya Muungano wa Tanzani. Nihayo tu kwa leo.
 
  • Thanks
Reactions: J C
Umenena mkuu . kama hatutochukua ushauri huu hakika hatutoboi.
 
Kuna kundi humu pia HALINA CHAMA.Halijawahi wala halifikirii kuwa na unazi wa vyama.Wao na vyama vya siasa ni kama Mashariki na Magharibi.
 
Back
Top Bottom