Pagan Amum
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 1,932
- 4,400
Mbunge Upendo Peneza wa viti maalum kupitia mkoa wa Geita (CHADEMA) ameitaka serikali kupitia upya mikataba yote ya tozo za kodi katika migodi yote iliyopo nchini..
Mbunge huyo kasema hayo alipokuwa akichangia hoja katika bajeti ya Nishati ya Madini. Ambapo kaonyesha kusikitishwa kwake kwa jinsi serikali inavyopoteza fedha nyingi kwa kuruhusu mianya ya kodi katika maeneo ya migodini. mfano katoa mgodi wa Blayahungu ambapo serikali imetoa "Fuel Leavy" hivyo kupelekea kupoteza mapato mengi sana... Pamoja na hilo kalitaka serikali kuliangalia na kufanyia marekebisho service levy kwa makampuni ya migodi nchini..
Mh. Peneza katika mchango wake kaonyesha ni jinsi gani serikali inaweza kufaidika na mapato mbalimbali katika sekta ya madini tofauti na sasa ambapo mapato mengi upotea mikononi mwa wawekezaji...
Katika mchango wake bungeni, Mbunge wa Viti Maalum kupitia mkoa wa Geita, Upendo Peneza kasikitishwa na jinsi kampuni ya GGM inavyodharau na kuonyesha kiburi cha hali ya juu kwa serikali...
Mbunge huyo katoa malalamiko hayo baada ya kampuni ya GGM kukaidi kutekeleza agizo la serikali lililotolewa na Naibu waziri wa Nishati na Madini Dr. Kalemani. Katika agizo hilo, Waziri aliitaka uongozi wa kampuni hiyo kushughulikia athari zinazokabili wananchi zitokanazo na vumbi, tetemeko na maji machafu yatokanayo na mgodi huo...
Hivyo, Mbunge kaitaka serikali kuwachukulia hatua kali, ili iwe fundisho kwa wawekezaji wengine,ikiwa ni pamoja na kulinda afya za wananchi...