African Believer
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 436
- 428
Habari ndugu wana JF!
Na baada ya salamu.
Karibuni katika mjadala kuhusu upendo.
Katika miaka ya karibuni dunia imeshuhudia kuchanua kwa ndoa ya mke mmoja (monogamy) na kudumaa kwa ile ya wake wengi (polygamy). Kukua huko kumeambatana na hoja dhaifu inayoenezwa na wale wanaopinga ndoa ya mke zaidi ya mmoja (polygamy) inayodai kuwa upendo/mapenzi hayagawanyiki jambo ambalo si kweli.
Kwa nini nasema ni hoja dhaifu? Twaweza kupata majibu sahihi kwa kuangazia kwanza maana ya neno Upendo.
Upendo (love) ni neno linalotumiwa sana na wanadamu katika kuelezea hisia za ndani kabisa katika nafsi ya mtu/mnyama kuelekea kitu, mtu au jambo fulani.
Neno upendo linatokana na kitenzi "kupenda" na hufanana pia na neno pendo, mapendo pamoja na mapenzi.
Hivyo, mapenzi/upendo ni haja ya msingi kabisa ya binadamu au mnyama pale anapovutiwa na jambo fulani likifuatiwa na hamu iambatanayo na furaha hasa pale lengo linapofanikiwa. Kwa sababu hiyo upendo/mapenzi ni mojawapo ya haja za msingi kabisa za mwanadamu.
Kama tulivyokwisha kuona hapo awali kuwa mapenzi (both sexually & non sexually) yanahitajika sana hasa kwa mwanadamu. Lakini ni lazima pia tujue kuwa akili ya mwanadamu haikuumbwa kupenda kitu kimoja yaani sio prewired na mtu atapenda tu kile alichokitamani kwa ajili ya furaha yake na pasipo na ukomo.
Watafiti wa mambo ya sayansi ya ubongo wa mwanadamu wameweka wazi kuwa kuna sehemu maalumu katika ubongo wa binadamu huratibu na kupangilia upendo/mapenzi katika mfumo wa Limbic ambapo kupitia kituo chake cha amygdala hisia zote za mwanadamu ikiwa ni pamoja na zile zihusianazo na mapenzi hupangiliwa. Hivyo twaweza kusema upendo wote huratibiwa sehemu moja.
Pia ukisoma uchambuzi wa mwanasaikolojia maarufu wa Marekani Abraham Maslow kwenye nadharia yake "Hierarchy of Needs" utaweza kuona namna alivyotenganisha mapenzi (sexual desires) kutoka mapenzi (love) ambapo alielezea mapenzi(sex) kuwa kwenye mahitaji ya kisaikolojia (psychological needs) na mapenzi (love) kwenye kundi la kupendwa (being loved/belonging) kwa maana hiyo mtu huhitaji kufanya mapenzi na pia atahitaji kupenda au kupendwa.
Kutokana na maelezo ya Maslow suala la kuhitaji mtu wa kufanya nae mapenzi(sex desire) halina uhusiano wa moja kwa moja na upendo kwani wafanyaji/mfanyaji anatimiza tu takwa la kimaumbile. Na ndiyo maana mtu aweza kwenda kutafuta mtu wa kulala nae usiku mmoja na akaridhika kabisa japo hakumpenda na wala hatomkumbuka ijapokua haja yake imetimizwa.
Kwa maana hiyo ya mapenzi mtu aweza kupenda mtu mke wa kwanza kwa mapendo ya dhati kwa kuwa moyo wake umevutika nae hivyo ili furaha yake itimie akaamua kufunga nae ndoa si kwa lengo la kufanya nae mapenzi tu bali kwa kuwa moyo/roho/akili yake imependezwa nae. Na baada ya muda akampenda tena mwingine na mwingine kwa namna ileile. Kwa kuwa amewapenda wote aweza kuwaoa wote.
Kumbuka wivu sio kipimo cha mapenzi bali ni ishara ya ubinafsi uliokithiri. Na yeyote mwenye wivu huwa na chuki kwani hapendi kumwona mwenzake anafaidi na siku zote hutamani kila kitu kiwe chake. Hivyo ni upotoshaji kwa mtu kutumia wivu kihalali, wivu ni mbaya kiasili na hauna zuri hata moja isipokua kwa umiliki peke.
Mwanadamu mmoja aweza kupenda bila kikomo, hebu angalia mifano ifuatayo;
Ndugu wana jamvi tukate minyororo na kupenda bila kikomo.
Karibuni tujadili.
Rejea: Maslow, A. H (1943) "A Theory of Human Motivation" in Psychological Review.

- Aweza wapenda wenzi wake (waume zake au wakeze)
- Aweza kuwapenda wazazi wake (baba &mama)
- Aweza kuwapenda ndugu zake (kaka & dada zake)
- Aweza kuwapenda watoto zake (binti zake & vijana wake)
- Aweza kuwapenda rafiki zake wake kwa waume.
- Aweza kuwapenda wanyama wake wakufugwa; Farasi, paka, mbwa nk.
- Pia aweza penda timu ya mpira wa miguu ya mtaani kwake pamoja na klabu moja maarufu duniani.