Upelelezi kesi ya Lema wakamilika

Upelelezi kesi ya Lema wakamilika

KIBE

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2010
Posts
943
Reaction score
186
[h=2]Upelelezi kesi ya Lema wakamilika[/h]



Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema


Upelelezi wa kesi ya kuchochea kutenda kosa na kusababisha uvunjifu wa amani katika Chuo cha Uhasibu Njiro inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema umekamilika.

Wakili wa Serikali, Eliainenyi Njiro, alieleza hayo jana wakati akiomba tarehe nyingine ya kusikilizwa shauri hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Devotha Msofe.

Aliomba kesi hiyo itajwe tena mahakamani hapo Julai 2 kwa ajili ya kumsomea Lema maelezo ya awali.

Njiro alieleza kuwa, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Kwa upande wake, Hakimu, Msofe alikubaliana na upande wa Jamhuri pamoja na Wakili wa Lema ambaye ni Humphrey Mtui kuwa kesi hiyo ipelekwe tena mahakamani hapo Julai 2 mwaka huu, kwa ajili ya mshtakiwa Lema kusomewa maelezo yake ya awali yanayomkabili katika kesi hiyo.



CHANZO: NIPASHE
 
Wasisahau na video iliyoko jf na u-tube wakati lema anaongea na wanachuo.
 
wakati wa kujua pumba na mchele huo, lakini washazoea kuaibika hawa watu
 
Mzizi ulikuwa ni usalama wa wanachuo, Vipi muuwaji alishapatikana! au nguvu zote ni kumwandama lema?. Au ndio ashageuzwa mhusika?
 
hii migamba inatumia nguvu nyingi kupambana na lema wakati mpaka leo polisi hawaja twambia wana chuo wana fanyiwa vitendo vya kikatili na kinananii hilo ndilo swala kuu kwasababu mtu aliyeleta uchochezi ni mkuu wa mkoa na si mh lema hiloliko wazi
 
Back
Top Bottom