UPDP yabadili uongozi wake

Lilombe

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
242
39
CHAMA cha UPDP kimefanya mabadiliko ya uongozi kwa kumwondoa aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Abdallah Ally.
Mwenyekiti wa chama hicho, Fahmi Dovutwa, alisema mabadiliko hayo yalifanyika katika kikao cha halmashauri kuu ya chama kilichofanyika mwishoni mwa wiki.
Kwa mujibu wa Dovutwa, kutokana na hali hiyo, Hamad Ibrahimu, ameteuliwa kushika nafasi ya katibu aliyepita na kwamba Ally atapangiwa shughuli nyingine.
“Kikatiba halmashauri kuu ndiyo inapitisha na kuchagua katibu mkuu, hivyo tumefanya mabadiliko hayo na Ally tumempangia majukumu mengine ya kujenga chama pia,” alisema Dovutwa.
Dovutwa alisema kwa sasa chama chake kimejipanga kuhakikisha kinafanya kazi na kuvutia wanachama wengi zaidi na kujipanga na na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.


Source: Tanzania Daima
 
FAHMI DOVUTWA ni mmoja wa watanzania waliojitokeza kugombea Urais mwaka jana na kura hazikutosha kuwa Mkazi wa Jengo la Magogoni
 
Utitiri wa Tu vyama hutu ndio unaoua upinzani. Jiungeni na vyama kama CDM muongeze nguvu kuikomboa nchi.
 
Correction ndogo: kabla ya uchaguzi wenyewe huyu jamaa,na wenzake wawili akina nani sjui nimeshawasahau wakatangaza kumuunga mkono JK.na kuwasihi "wafuasi wao" kumpigia kura kwa "wingi" teh teh...siasa bana,kama bangi vile ah!
FAHMI DOVUTWA ni mmoja wa watanzania waliojitokeza kugombea Urais mwaka jana na kura hazikutosha kuwa Mkazi wa Jengo la Magogoni
 
Ni vizuri ukajua vyama hivyo ili uweze kupanga mikakati ya kuungana nao nguvu, kwani vyote vipo katika daftari la Tendwa, tena majuzi walipewa mwaliko wa sherehe za Muungano, wakapanda pipa hadi Unguja
 
mhhh vyama hivi bana ....sasa huyu DOVUTWA ndo nani?


ha ha ha haaaaaaa muulize mzee Kiravu na mwenzie L Makame watakueleza vizuri

kwangu huyu jamaa ni bonge la kibaraka cha waliovua magamba
 
Fahmi Dovutwa alijitoa kwenye uchaguzi na kusema kura zake apewe JK baada ya kudai kuwa NEC ilikosea jina lake kwenye karatasi za kupigia kura kwa kuandika Yahmi badala ya Fahmi. Hata hivyo aliata kura kadhaa kuliko hata NCCR kwenye baadhi ya maeneo!
 
Dovutwa ni mzaramo wa Maneromango, katika kuzindua kampeni za kugombea urais katika ukumbi wa Maelezo, alisema kama akiingia Ikulu, serikali yake itajenga viwanda vingi vya silaha kwa vile kuna soko la kutosha nchi zilizo jirani na TZ. Hata hivyo kabla ya siku ya uchaguzi alitangaza rasmi kujitoa kwa kile alichodai "NEC wamefanya makusudi kupotosha jina lake katika karatasi za kupigia kura kwa kuchapisha jina la Dovutwa Yahmi Nassoro Dovutwa badala ya Dovutwa Fahmi Nassoro Dovutwa" na akatangaza kumuunga mkono JK. NEC hawakutambua kujitoa kwake hivyo jina lake lilipigiwa kura, hatimaye kati ya wagombea 7 akawa wa mwishio kwa kupata kura 13,123 sawa na 0.15% ya kura zote za urais.
 
Back
Top Bottom