Tumezoea utani na kila kitu kumuachia “Mungu” hatakama ni jukumu letu kutatua jambo utasikia ‘Mungu atuepushe’
Ukiona BBC wanavoonyesha hatua za hizo nchi zingine zinavuchukua unaweza kusema pengine sisi tuko sayari nyingine ndio maana tume relax.
Washington juzi kuna mtu alikua Diagnose na hiyo kitu walifunga Metro, Shule zilizokua Karibu na barabara ya yeye alipopita pamoja na kufanya Fumigation ya mahali pote alipokanyaga.
Kwetu sisi ni maigizo kwenye Daladala kugusana lazima bado pantoni, Kariakoo misongamano daily. Kingine ni mtu akiwa na dalili au akiwa ametoka kwenye hizi nchi zenye haya milipuko inapaswa akae Quarantines kwa siku 21 kujua kama anao au la, pale JNIA wanapima temperature tu ikiwa normal unasepa kama unao dalili utaenda kuzipata nyumbani kwako.