Updates: Hukumu kesi ya EPA leo

Hawa sio Dagaa ila walitumia njia mbaya, wangetumia kama ya ile ya KAGODA mambo yangekuwa shwari
 
Ni lazima usafishe mtandao kwa kuanza na dagaa. Hata sinema huwa tunaona kwanza wanamalizwa maadui halafu ndio anasakwa kubwa la maadui. Uliona sinema ipi "gang leader" akamalizwa mwanzo, si sinema itakwisha kabla haijaanza.
Mambo ya sinema hayapo hapa, angalia wenzako wameanza na Mubarak then wasaidizi wake ndio wamefuata, mwendo ndio huo.
 
Pesa iliyoibwa EPA ni zaidi bil 40 tunahangaika na 2bil. wako wapi walioiba bil 20?
Asalamaleku walah

Mkubwa naomba nikusahihishe;pesa iliyoibwa EPA ni zaidi ya billion 133 siyo billion 40 tu.Mimi naona wote washughukikwe kikamilifu bila kujali nani kaiba nyingi au chache.Wizi wa mali ya umma haukubaliki hata kama ni elfu 10 kwa nini uibe wakati unalipwa mshahara na mafao mengine?
 
Aliyekulamba billion mbili unamwita kidagaa? kwi kwi kwi teh teh teh!


Kuna kubwa la maadui kalamba 13Bil kupitia Kagoda kwenye uchaguzi flani ulioagiza gari special za Kijani Wilaya zote ukiacha pikipiki na baiskeli, hivyo wanaziba kibomba wanatanua mtaro wa kuzibeba zaidi........
 
Update is still loading the page!! Please wait!
 
Alichomaanisha Hosea Jana ni kuwa ukiwa umepiga hela nyingi ni safi kwao kwani hata ukienda kumchunguza mtu anaweza akakutoa hela kidogo ukapotezea siku ila kama unaiba vijisent then utagawana kiasi gani na wao Takukuru? Hivyo kwa kuondoa usumbufu ndio maana kesi za mwizi wa kawaida huwa hazichukui miaka. Kuna tofauti kubwa sana kati ya mwizi wa 1ml na mwizi wa 1bl. Hujakosea Hosea. Only in TZ.
 

EPA ilikuwa na wezi wa aina mbili yaani mwizi msafi na mwizi mchafu,msafi u huru kwa usafi wake ila mchafu jela.Eh nyinyiemu na hukumu zenu za macho.
 
EPA ilikuwa na wezi wa aina mbili yaani mwizi msafi na mwizi mchafu,msafi u huru kwa usafi wake ila mchafu jela.Eh nyinyiemu na hukumu zenu za macho.

EPA yenyewe yote ni halali isipokuwa wako waliofanya haramu katika kipindi cha Mkapa kutumia mwanya uliokuwepo na hao ndio wako jela. Wale waliofanya kihalali wameambiwa haya rudisheni hizo fedha biashara imekwisha.

Wizi wa mali ya umma ni wengi sana, walianzia siku nyingi sana toka enzi za Nyerere, wakauwa viwanda karibu vyote, vilivyojengwa na walivyodhulumiwa matajiri wa siku hizo, Jee Nyerere aliwafanya nini? Mwinyi? Mkapa? at least sasa tunaona Kikwete akiwafanyizia.
 
Kweli nyie wachangiaji watu wa hajabu. jambo kidogo tu limewajaza upepo na kuwatoa relini na tayari mmepotelea porini na hakuna anayebani kuwa ndo mnazidi kupotezana maana mmekuwa vipofu. Ebu rejea kwenye mstari tusonge mbele sio kuzunguruka tu! Mada inasema "Updates: Hukumu kesi ya EPA leo". Ni busara tu, kama kuna mwenye updates atujuze kama mweupe kubali wapishe wenye hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…