ALEX PETER
Senior Member
- Jan 17, 2012
- 117
- 23
Mgomo wa madaktari jijini Dar es Salaam umeanza kushika kasi ambapo katika baadhi ya hospitali ikiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wagonjwa walikosa huduma na kuishia kutangaziwa warejee nyumbani hadi watakapopata taarifa kuwa mgomo huo umeisha.
Katika uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika hospitali za jijini hilo, umebaini kuwa mgomo huo umeshika kasi zaidi Muhimbili na Hospitali ya Amana ambako baadhi ya vitengo vya huduma za afya vilifungwa ili kuongeza nguvu ya madaktari katika vitengo vya dharura.
Katika Hospitali ya Muhimbili, gazeti hili lilishuhudia wagonjwa wakiwa wamezagaa na kujazana hasa katika Kitengo cha Mifupa (MOI) huku wengine wakiwa wamekata tamaa ya kupatiwa huduma.
Gazeti hili lilishuhudia mmoja wa watoa huduma za kupokea wagonjwa akiwatangazia wagonjwa waliojazana katika eneo la mapokezi hospitalini hapo kuwa waondoke hadi watakaposikia mgomo umeisha kwa kuwa sasa hakuna huduma yoyote.
Mimi mtoto wangu ana matatizo ya kichwa kuwa kikubwa leo tulitakiwa kuja kuonana na daktari, lakini tangu asubuhi nimefika hapa nimekuta umati mkubwa wa watu wakilalamika kukosa huduma, hadi tulipotangaziwa kuwa tuondoke hakuna huduma, alisema mkazi wa Morogoro, Martha Said.
Naye Khalfan Juma mkazi wa Kigogo alisema anasumbuliwa na miguu na amefika hospitalini hapo tangu asubuhi lakini hakupatiwa huduma yoyote kwani daktari aliyekuwapo ni mmoja wa watoto na hadi kufikia saa tano mchana alisitisha naye huduma.
Katika maeneo ya wodi za hospitali hiyo, hali ilikuwa mbaya kwa kuwa wagonjwa walilalamika kutopata huduma yoyote ya matibabu zaidi ya madaktari na wauguzi kuwapitia na kuwaulizia hali tu huku wauguzi wengine wakitoa lugha za kashfa.
HabariLeo ilijaribu kuwatafuta wasemaji wa hospitali hiyo ambao ni Jezza Waziri na Almas Juma bila mafanikio kwa kuwa ofisi zao zilikuwa zimefungwa huku kukiwa na ulinzi mkali wa askari ambao waliishia kugombana na waandishi wa habari.
Kwa upande wa Hospitali ya Amana hali haikuwa nzuri kwa kuwa kulikuwa na msongamano mkubwa wa wagonjwa huku madaktari wakiwa wachache hali iliyosababisha huduma kudorora kwa wagonjwa wa nje na ndani.
Mmoja wa maofisa wakuu hospitalini hapo aliyekataa jina lake kutajwa gazetini kwa kuwa si msemaji, alilihakikishia gazeti hili kuwa mgomo wa madaktari upo kwa kuwa madaktari wengi wa hospitali hiyo jana hawakufika kazini na kusababisha baadhi ya vitengo kufungwa.
Tumeamua kufunga vitengo vya kliniki kwa akinamama kutokana na upungufu wa madaktari waliofika kazini leo ili kufidia maeneo mengine ya dharura na huduma zinaendelea ingawa ni kwa kusuasua, alisema Ofisa huyo.
Hata hivyo, hali ilikuwa tofauti katika hospitali za Mwananyamala na Temeke ambako gazeti hili lilishuhudia madaktari wake wakiendelea na kazi bila dalili yoyote ya mgomo.
Easther Sufian, mkazi wa Tandika alithibitisha ndugu yake kupatiwa huduma katika Hospitali ya Temeke huku akikiri kuwa na hofu wakati wakienda hospitalini hapo ya kukosa huduma.
Lakini pia gazeti hili katika Hospitali ya Mwananyamala lilishuhudia wagonjwa wakitibiwa. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dk Amaan Malima, alisema hali ya hospitalini hapo ni shwari na hakuna mgomo kwa kuwa madaktari wote wameripoti kazini na amewashuhudia wakiendelea na kazi.
Kwa upande wake Katibu wa Hospitali ya Mwananyamala Edwin Bisakala, alisema kazi zinaendelea kama kawaida hospitalini hapo hakuna daktari wala muuguzi ambaye hayuko kazini kwa sababu ya mgomo