Update:kuvuja kwa mitihani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Update:kuvuja kwa mitihani

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mzee wa Gumzo, Oct 9, 2008.

 1. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #1
  Oct 9, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati taarifa za awali hapo asubuhi zilitanabaisha kuwa mtihani wa geography uliokuwa ufanyike leo asubuhi ulitangazwa kufutwa baada ya kuvujishwa kwa makusudi, taarifa za uhakika zimejulisha kuwa mtihani wa geography ulifanyika kama ilivyopangwa isipokuwa ulisambazwa mtihani mwingine hivyo kuwaduwaza wanafunzi ambao walikuwa na uhakika wa kuvuna wasichokipanda(A).

  Taarifa zinadhibitisha kuwa kwasasa mitihani inasambazwa usiku usiku kuanzia saa tisa na kwa kuwa mitihani yote imevujishwa, mitihani mingine imesambazwa kusudi ratiba iendelee kama kawaida.Hata hivyo wizara bado inakataa kuwa mitihani mingine imevujishwa.Mtihani wa history,physics,chemisty imesambaa kila kona za miji na vitongoji.

  Taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa kuvuja huku kwa mitihani kulisukwa na wahusika ambao walitaka kuiaibisha serikali kutokana na kukataa au kushindwa kutatua malalamiko ya waalimu.Wakati tunajiuliza kwanini mitihani ivuje kwa kiwango hiki,tarifa ni kwamba huu ni mpango maalumu na ulikuwa na kamati ya kuhakikisha kila mtihani unavujishwa na kusambazwa.

  Kilichopo sasa ni kujaribu kupambana na wanafunzi wenye mitihani hiyo mitaani na kusambaza mitihani mipya usiku usiku kwenye vituo na shule lakini ukweli ni kuwa wahusika wakubwa wa hujuma hii wapo kwenye ofisi hizohizo za mabosi wa WIZARA NA NECTA
   
 2. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Wizara ya Elimu na NECTA wanapaswa kuchukua hatua mathubuti moja wapo ni kuanzisha kitengo cha upelelezi kwa ajili ya mitihani. Bila hivyo itabaki kupiga kelele kila mwaka na mambo yale yale yakiendelea. Ni mbaya sana kwa wanafunzi wanaofanya mitihani kwa jitihada na uwezo wao kutochaguliwa kwenda form six kwa kuzidiwa alama (marks) na walioiba mitihani. Wito wangu ni kuanzisha kitengo cha intelligence kwa ajili ya mitihani.
   
Loading...