Upanuzi wa miji unaua Kilimo chetu

Upanuzi wa miji unaua Kilimo chetu

Kifaurongo

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2010
Posts
4,287
Reaction score
2,437
Katika kutembea miji mbali mbali nchini nimeshuhudia kupanuka kwa kwa kasi kwa miji yetu.

Halmashauri zetu zimekuwa zikiwanyang'anya wakulima maeneo yaliyokuwa mashamba, kuyapima na kuyageza kuwa makazi. Kwa kigezo cha kila mkilima mwenye shamba, kugaiwa kiwanja.

Sera na sheria hii ya kugeuza mashamba ya wakulima kuwa makazi kwa mkulima kupewa kiwanja ktk eneo husika nimegundua inamakosa makubwa sana, sababu inaua kilimo na inasababisha kubsdilisha mfumo wa maisha ya waliokuwa wakitegemewa kilimo kama kazi ktk maisha yao kushindwa kujua cha kufanya.

Mawazo yangu ninadhani serikali inapoamuwa kupanua miji kwa kupima viwanja maeneo ya wakulima, ingekuwa vema wafidiwe maeneo mengine kwa ajili ya kuendeleza kilimo chao kuliko kuwaacha wakihangaika na jinsi ya kumudu maisha yao bila kilimo. Kuliko shida wanayopata ya jinsi ya kupata pesa za kununua chakula.
 
Ni kweli upanuzi wa miji hapa kwetu Tz haizingatii hifadhi ya ardhi yenye rutuba ya kilimo. Matokeo yake maeneo ya kilimo yamegeizwa makazi badala ya kuzalisha mazao huku maeneo yasiyofaa kwa kilimo yakibali.
 
Sasa unataka kama kuna aridhi ya rutuba mijini tuache watu walime na kufuga ?? Ebu fikiri ingekuwa vipi kama tukitafuta tiba ya aridhi zisizo na rutuba . Kwa mawazo yangu me nasupport kwa asilimia 1000 ugawaji wa viwanja hvylakini wakulima wetu sasa wasibweteke inatakiwa wafanye tafiti zaidi kukabilia na aridhi zozote watakazo kumbana nazo
 
sasa hivi baada ya halmashauri kugundua kuwa wakiuza viwanja wamekimbilia kwa kasi kubwa sana kugeuza mashamba kuwa viwanja hali hii ikiachiwa baada ya muda mfupi tutakuwa ombaomba wa chakula na pia hizi wilaya mpya na mikoa mipya nayo inapunguza ardhi ya kilimo
 
Katika nchi yetu ardhi haijawa tatizo, kwani hata halmashauri zikiamua kupima hazimalizi ardhi yote, tatizo ni kutokuwa kuwa na mipango ya kuwafanya waliokuwa wakilima maeneo yanayopimwa wanaendelezwa na shughuli yao kwa kugaiwa maeneo mengine badala ya kubadilishiwa mfumo wa maisha kwa kupewa kiwanja bila kujua watajikimu vipi!

Wakulima wengi walionyang'anywa maeneo yao sasa wanstegemea chakula cha kununua hali kuwa hawana kazi.
 
Katika kutembea miji mbali mbali nchini nimeshuhudia kupanuka kwa kwa kasi kwa miji yetu.

Halmashauri zetu zimekuwa zikiwanyang'anya wakulima maeneo yaliyokuwa mashamba, kuyapima na kuyageza kuwa makazi. Kwa kigezo cha kila mkilima mwenye shamba, kugaiwa kiwanja.

Sera na sheria hii ya kugeuza mashamba ya wakulima kuwa makazi kwa mkulima kupewa kiwanja ktk eneo husika nimegundua inamakosa makubwa sana, sababu inaua kilimo na inasababisha kubsdilisha mfumo wa maisha ya waliokuwa wakitegemewa kilimo kama kazi ktk maisha yao kushindwa kujua cha kufanya.

Mawazo yangu ninadhani serikali inapoamuwa kupanua miji kwa kupima viwanja maeneo ya wakulima, ingekuwa vema wafidiwe maeneo mengine kwa ajili ya kuendeleza kilimo chao kuliko kuwaacha wakihangaika na jinsi ya kumudu maisha yao bila kilimo. Kuliko shida wanayopata ya jinsi ya kupata pesa za kununua chakula.
Mkuu hili hata mimi limekuwa likinisumbua sana kila nianvyoona ardhi yenye rutuba iliyokuwa inatumikwa kwa kilimo inageuzwa kuwa makazi ya watu au viwanda, nimeshangaa kuona kumbe tuko wengi wenye mawazo kama yako!! Huwa nasononeka sana ninapoangalia ardhi nzuri iliyokuwa inatumika kwa kilimo cha mpunga pale Mwanza maeneo ya Igoma na huku njia ya kwenda Shinyanga maeneo ya mpakani na wilaya ya Misungwi ukitoka Buhongwa sasa hivi ni makazi ya watu na viwanda. Hivi haiwezekani kuacha japo kilomita kadhaa kwa ajili ya kilimo? Kwa mfano hayo maeneo yaliyokuwa yanatoa mpunga kwa wingi isingewezekana kuachwa yakaendelea kutoa mpunga na hayo makazi yakatafutiwa sehemu ambazo hazina rutuba? Hebu serikali yetu ibadili mtazamo jamani.

Sasa hivi na hapa kwetu Shinyanga kuna eneo zuri sana la kilimo cha mpunga pale daraja la Mhumbu lakini si ajabu ndani ya miaka miwili ijayo litageuzwa kuwa makazi au viwanda???!!!
 
Kifaurongo, umeleta mada nzuri sana. Mfano mzuri wa hayo unayosema ni yanayoendelea kutokea sasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru. Wanavamia mashamba kama wamechanganyikiwa!!! Kuna mashamba yalikuwa/yana miundombinu mizuri ya kilimo ikiwemo umwagiliaji lakini wanavamia hayo maeneo na kugeuza viwanja. Tatizo ni kwamba hatuna sheria zinazolinda ardhi ya kilimo. Ardhi ya misitu, wildlife, etc. inalindwa, ila ardhi ya kilimo ndo inaonewa. Huu ni upumbavu ambao hatuna budi kuupiga vita. Kuna mengi tunaweza ku-share ili tuushauri umma, ebu nitumie private text tuwasiliane then turudi kwa wadau tukiwa na facts zilizokamilika tujadili hii ishu kwa kina. Kilimo kitaangamia kwa sababu ya tamaa za Serikali za Mitaa.
 
Sasa unataka kama kuna aridhi ya rutuba mijini tuache watu walime na kufuga ?? Ebu fikiri ingekuwa vipi kama tukitafuta tiba ya aridhi zisizo na rutuba . Kwa mawazo yangu me nasupport kwa asilimia 1000 ugawaji wa viwanja hvylakini wakulima wetu sasa wasibweteke inatakiwa wafanye tafiti zaidi kukabilia na aridhi zozote watakazo kumbana nazo

Kijana umewahi kuishi kijijini kweli? Nchi hii kazi ya kilimo tumewaachia wazee vijana wenye nguvu na elimu tumekimbilia mijini, Huyo mkulima wa kijijini anauwezo gani wa kufanya utafiti wa ''soil treatment''

Ardhi 'Kikatiba' ni mali ya serikali, umemnyang'anya mkulima ardhi yake, atapataje ardhi nyingine pasipo kusimamiwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi unaosimamiwa na serikali za vijiji au Halmashauri za miji?
 
Mleta mada hili swala ni nyeti umelileta linahitaji kujadiliwa kwa kina.
 
Mleta mada hili swala ni nyeti umelileta linahitaji kujadiliwa kwa kina.

Ni kweli hili ni moja ya mambo ya msingi yakujadiliwa tubaili tabia hii iliyozoeleka nataraji tukichangia kwa makini tutaawasaidia viongozi wetu kuona kasoro hizi.
 
Back
Top Bottom