Ule mradi wa Terminal 3 ulikuwa ufanyike kwa utaratibu wa PPP na wajenzi wangeuendesha kwa muda lurejesha gharama zao. Lakini hapa katikati ilionekana mkandarasi alichaguliwa bila kufuata utaratibu kama sheria ya public procurement inavyotaka na tatizo kubwa lilihusu namna ambavyo financing ya mradi ilikuwa ifanyike.
Kama ulipita hivi karibuni utaona yale mabango ya Contractor yameondolewa na hii ilikuwa wakati wa kilele cha debate ya Bunge la April na wahusika walikuwa wanajaribu kufuta madudu yao.
Machakato umeanza upya wizarani na huenda kampuni ile ile wakapewa hiyo kazi baada ya kuhalalisha kupewa kwao hiyo kandarasi.
Mwakyembe FUFUA Air Tanzania(tena ikiwezekana) waalike Wawekezaji wa CHINA/KOREA then ndo tujenge uwanja!
Hii inchi tunapenda ufahari ivi wangeenda watu wachache huo uwanja usingejngwa.Huwezi amini ndgu yangu serikali ya Kikwete ilivyo na vioja vya ajabu,kusaini mkataba wa ujenzi wa uwanja wizara nzima imeamia Uhollanzi akiwepo Kikwete, WAZIRI MWAKYEMBE,Naibu Dr.Tizeba, Katibu Mkuu, Chambo na wakurugenzi wengine.Ni aibu kwa utawala wa Kikwete, Kwani Katibu au ceo wa TAA au mmoja wa mawairi hao hawezi kuwakilsha mpaka ofisi ya umma kufungwa kwa kukosa viongozi wenye maamuzi?.