Upande wa pili wa hotuba ya JK Bungeni

Upande wa pili wa hotuba ya JK Bungeni

Vujole

Member
Joined
Apr 3, 2013
Posts
33
Reaction score
22
Hivi JK angeunga mkono kwa uzito uleule alioutumia kuikosoa, ungekuwa na maoni gani?
 
Haikuwa kazi ya JK kuunga mkono au kupinga Rasimu ya Katiba Mpya. Hiyo ni kazi ya wajumbe wa Bunge la Katiba. Kazi yake ilikuwa KUZINDUA BUNGE MAALUMU AFU ACHAPE MWENDO, PERIOD!
 
Ndiyo maana nimetaka kujua maoni yako, Ni kweli hakufanya lililokuwa jukumu la "mgeni rasmi". asingewazodoa tume, akawapongeza je?
 
Kama kuna hotuba mbaya nilizowahi kuzisikiliza hii ilivunja rekodi. Hakuwa na sababu ya kuichambua rasimu wala kutoa maoni. La kwake lilikuwa ufunguzi na mengine awaachie aliowateua kwa kazi hiyo. Kutoa angalizo ni kuwalead wajumbe kufanya maamuzi anayoyataka yeye. Bunge hilo lingekuwa na busara lingejiuzulu na kumwachia rasimu na katiba yake kwani kitendo cha kuendelea na kazi ni usaliti kwa umma uliotoa maoni.
 
Kwa mtazamo wangu mdogo, JK alitakiwa kuzungumza mambo mkuu matatu. Moja kuonesha mapungufu yaliyokuwepo kwenye katiba ya sasa na kuwaasa wajumbe wasirudie makosa na ndio maana ya mchakato huo mzima wa katiba mpya. pili alipaswa na kuwatia moyo wajumbe watambue kazi waliyopewa sio ndogo na jinsi gani serikali inaingia gharama kubwa hivyo wasiende kulala bungeni. Tatu serikali yake iko makini kuhakikisha uwepo wao Dodoma hakukwamishwi hasa kuhusu maslahi yao, serikali itafanya kila linalowezekana kuhaikikisha wajumbe wanapata stahiki zao ili waweze kutekeleza jukumu hilo baada ya hapo ATANGAZA BUNGU MAALUMU KUZINDULIWA.
 
Angefungua bunge maalumu, na angetumia muda mwingi kuwasihi wajumbe wawe wazalendo zaidi, wawe wamoja bila kujali itikadi za kivyama.
Ila yeye kapeleka mipasho pale, kavurugua maoni ya tume waliokusanya kutoka kwa wananchi, aayotaka yeye na chama chake ndio wajumbe wafuate.

Angekubaliana na maoni ya tume na ndio alitakiwa afanye, kama si hivyo kungekuwa hakuna faida ya tume kwenda kuwahoji wananchi. Hizo hela bora zingeelekezwa kwenye huduma za kijamii hasa vijiji huko.
 
Kama kuna hotuba mbaya nilizowahi kuzisikiliza hii ilivunja rekodi. Hakuwa na sababu ya kuichambua rasimu wala kutoa maoni. La kwake lilikuwa ufunguzi na mengine awaachie aliowateua kwa kazi hiyo. Kutoa angalizo ni kuwalead wajumbe kufanya maamuzi anayoyataka yeye. Bunge hilo lingekuwa na busara lingejiuzulu na kumwachia rasimu na katiba yake kwani kitendo cha kuendelea na kazi ni usaliti kwa umma uliotoa maoni.
Kama watanzania wangekuwa na elimu ya kuwawezesha kujitambua walitakiwa waondoke warudi kwao kwani inaonekana dhahiri kwamba kikwete hana political will ya kuiletea NCHI hii katiba waitakAyo.
 
Kwa mtazamo wangu mdogo, JK alitakiwa kuzungumza mambo mkuu matatu. Moja kuonesha mapungufu yaliyokuwepo kwenye katiba ya sasa na kuwaasa wajumbe wasirudie makosa na ndio maana ya mchakato huo mzima wa katiba mpya. pili alipaswa na kuwatia moyo wajumbe watambue kazi waliyopewa sio ndogo na jinsi gani serikali inaingia gharama kubwa hivyo wasiende kulala bungeni. Tatu serikali yake iko makini kuhakikisha uwepo wao Dodoma hakukwamishwi hasa kuhusu maslahi yao, serikali itafanya kila linalowezekana kuhaikikisha wajumbe wanapata stahiki zao ili waweze kutekeleza jukumu hilo baada ya hapo ATANGAZA BUNGU MAALUMU KUZINDULIWA.

TRULY, YOU ARE A GREAT THINKER!! Hivyo ulivyo sema nivyo Nyerere angelisema,au Winston charchil angesema au George Washington angeselisema.
 
Back
Top Bottom