Upande wa pili kuhusu serikali ya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upande wa pili kuhusu serikali ya Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nakei, Jun 25, 2011.

 1. N

  Nakei Member

  #1
  Jun 25, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Katika serikali ya kikwete ni rahisi sana kupata haki yako pindi unapodhulumiwa au kunyanyaswa, mimi binafsi nilishawahi kutwangwa barua ya kulipa sh milioni mbili na TANESCO, kisa jamaa wamenisingizia nimeiba umeme, hiyo barua ilikuwa na vitisho sana. Kila mtu niliyemuomba ushauri aliniambia nitoe hongo ili mambo yaishe. Niliingia kwenye website ya TANESCO nika download mkataba kati ya tanesco na mteja, kuna kipengele killisema kama KAMA MTEJA HUJARIDHIKA NA MAAMUZI YA TANESCO APELEKE MALALAMIKO EWURA. Nikatuma email kwa EWURA. EWURA walifuatilia hii issue hadi mwisho na nikarudhishiwa umeme. Sijasafiri kwenda Dar nilikuwa nawasiliana na EWURA pamoja na TANESCO kwa njia ya email wakati nipo ofisini kwangu. Jioni narudi nyumbani nakuta umeme umerudishwa. Hata TANESCO wanakitengo cha kushughulikia matatizo ya mteja.

  Kuhusu polisi, siku hizi ni rahisi sana kumuona mkubwa yeyote wa polisi awe OCD, OCS hata IGP, nilishapata matatizo fulani fulani ikabidi niende kituo kikubwa cha polisi, nikaomba kuonana na OCS, sikupata kikwazo chochote niliweza kumuona na kumuelezea shida yangu, alinisikiliza na kunipa ushauri ambao ulinisaidia sana, pia kuwasiliana na IGP ni rahisi siku hizi, namba yake ipo wazi na ni rahisi kumuona.

  TATIZO LETU:
  Watanzania wengi hawajui kutafuta haki, mara nyingi tunakimbilia kwenye kutoa rushwa badala ya kutafuta haki. Na tunapenda sana short cut kwenye kila kitu.


  UZURI WA TANZANIA
  Kwa sisi watu wa hali ya chini ni rahisi sana kupata maisha mazuri kama utafanya bidii, ndio maana wakenya na waganda wanakimbilia TZ. Hata wachina wameanzisha biashara maeneo ya kariakoo, biashara wanazofanya nizakawaida kabisa lakini wanavuna hela. Hata ukifanya utafiti utagundua matajiri wengi hapa kwetu ni watu wa kawaida tu. Tuondokane na TRADITIONAL WAY OF EARNING MONEY(kuajiriwa), hata kama ukiwa msomi tumia elimu yako kuingia kwenye ujasiria mali achana na kutafuta kazi za kuajiriwa, sisi hatuna viwanda. Mazingira ya kunyanyuka kimaisha TZ ni mazuri sana kwa sasa.
   
 2. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Ushauri mzuri sana,binafsi nitaufanyia kazi
   
 3. Researcher

  Researcher Senior Member

  #3
  Jun 25, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Very positive..
   
 4. k

  kajembe JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  umeniongoa aisee hasa kwenye kipengele cha kujiajili!
   
 5. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  thx ndugu..umechochea sumu kali zaidi ya niliykuwa moyoni mwangu!..kwa kweli tz ni sehemu nzuri ya kufanya biashara,kuna maeneo mengi sana hasa huku mikoani hayajakuwa exploite kibiashara. lazima tuchukue fursa hizi na kuacha kulalamika lalamika!
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nakei unayoyaseman ni kweli lakini tatizo ni kuwa hayo hotokea katika sehemu ndogo sana ya maisha ya kawaida ya mtanzania... wengi hawana 'bahati' kama yako ya kufanikiwa kumaliza mambo kwa kutumia email
   
 7. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  You deserve to be a great thinker ila tatizo heading yako haijakaa vizuri lakn content ya message yako iko poa.
   
 8. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Thanks kaka,mimi nimemaliza advanced dipl6a ya computer mpaka sasa sijapata kazi ya maana kwa miaka2.naungaunga tu kazi so nimefarijika na mchango wako ila tatizo la tanzania ni mtaji.
   
Loading...