Upandacho utavuna......

mnyandzombe

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2015
Posts
245
Reaction score
194
Habari wanaMMU.

Bila hata kuchoshana naenda kwenye mada tajwa.

Kutokana na hali ya mfumo wa maisha kutazamwa na watu wenye akili tofauti nakuona kila kitu wanaweza kufanya, kuna mambo ambayo kamwe ukifanya kwa wengine hakika utavuna kwa wakati wake usipozimia roho.

Wewe ni mwanaume rijali una nguvu lakini unaishi kivivu kama hakuna kesho tegemea kutofanikiwa kimaisha. Utaishia kusikia mafanikio ya wenzio wanaofanikiwa lakini kumbe wanajituma .Wewe ni kuhudhuria vikao vya wanywa kahawa tena asubuhi na kupitia kwa wauza magazeti kujua nini kimejiri

Umeoa kama mimi na una watoto wa kike japo wadogo lakini Ukware haujakuishia kila siku unapepesa macho kuhangaika na vibinti vya wenzio ambao ndo wanakua subiri na wako wakue kidogo wapapupiliwe sawasawa.

Unahangaika na kufunua tupu za wake za watu tena kwa kuvizia waume zao wakiwa kazini Subiri wako afumuliwa hadi linda na watakuletea hadi mlangoni.

Mwanaume mzima unashindia majungu na umbea kama mwimbaji wa taarabu wakati wanaume wenzako wanapiga kazi wewe jioni ikifika unapiga mizinga ya dinner bila hata aibu. Utakufa na njaa siku moja kisa majungu na ukizubaa utafumuliwa tuuuu na wenye njaa kali.

Jioni njema na Mungu abariki kazi za mikono yetu na afya njema
 
Najua unamsema mtu kakufika shingoni..
Wanaume hatusutani wanaume ni kazi tu hata kifunua sketi ni moja wapo ya kazi..
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…