Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Chungu kibovu kimekuwa magae! Naam, kila matokeo ni nakisi ya mipango. Wanasema ukipanda mahindi ndiyo utakayoyavuna! Maji ya nazi, yataka uvungulio, kwamba umakini unahitajika kila hatua katika kupanga na kutekeleza, kosa moja litakuhamishia kilioni.
Mbona kelele nyingi? Ooh Edward Lowassa anaweza kufa kwa presha kwa sababu ya pigo la Dodoma. Wewe unayemuwazia hivyo na kupaza sauti kijiweni, umeshakutana naye akakwambia maumivu yake? Utasikia namuonea huruma Bernard Membe! Maskini January Makamba? Sijui anajiwazia nini Jaji Augustine Ramadhan? Je, Mwigulu Nchemba na safari yake iliyotakaswa na TB Joshua?
Wanatazama ya juujuu tu, nyuma ya pazia hawajaangalia. Hivi, kuna mwenye maumivu ya matokeo ya Dodoma kuliko Jumbura? Humjui Jumbura! Kwenye mtaa wao ndani ya Jiji la Dar es Salaam, yeye ndiye kama JK, neno lake sheria, mambo yote makubwa anaulizwa yeye. Si msanii wala mwana michezo, siyo mwanasiasa wala mwana taaluma yoyote, ila ni mjuvi wa mengi!
Jumbura ndiye aliyeumizwa hasa na matokeo ya Dodoma. Akikusikia unasema sijui Lowassa au Membe ndiyo walioathirika, anaweza kulibondabonda tofali na kuligeuza mchanga kichwani kwako. Jumbura ana hasira sana, kila dakika anangata meno. Anatembea na kisu, usipite karibu yake!
Hakuwa mwenye kuwania tiketi ya uteuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ila alikuwa na mbwembwe kuliko mgombea yeyote. Alipewa ahadi kubwa na mgombea wake, naye akaamini. Alipewa tenda ya kukusanya vijana wapiga kelele watakaomshangilia mgombea mara atakapotangazwa kuwa mgombea Urais wa CCM katika Uchaguzi Mkuu 2015. Alitekeleza kikamilifu!
Aliambiwa vijana wanatakiwa wawe wa kutosha ili shamrashamra ziwe za kufuru ndani ya Dodoma, kusudi ionekane kweli uteuzi umekwenda vizuri na kwamba mteule anakubalika sana! Jumbura kwa uaminifu na matumaini ya hali ya juu, alikusanya vijana wa kutosha. Aliingia Dodoma na washangiliaji 200. Palepale Dodoma akakusanya wengine 100, jumla 300.
Ila Jumbura alidanganya, kwa bosi wake aliripoti vijana 350 aliwasafirisha kutoka mikoa mbalimbali na 150 ndiyo aliwakusanya Dodoma, ina maana alipiga panga vichwa 200. Na aliamini maisha yatakuwa murua kwa sababu baada ya kushinda aliahidiwa angezunguka na vijana wake nchi nzima, wakimshangilia mteule wao, wakati wa ziara ya chama kumtambulisha mgombea Urais.
Alipiga hesabu ya jumla na kujihakikishia kujenga nyumba, kuwa na gari la kutembelea pamoja na kufungua duka la vifaa vya ujenzi Mbweni, Dar, baada ya ziara ya nchi nzima ya mteule wa chama kutambulishwa kwenye mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar. Aliona nyota ya jaha imemtembela.
Alipofikiria na kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015, aliona fungu lingine litakuwepo, alichokifanya ikawa ni kuhakikisha anajionesha sana kwa mgombea ili amuone anavyofanya kazi. Alijitahidi kuwa mbunifu wa maneno ya upambe, kila wanapokutana anakuwa na matamshi mapya ya mapambio ili kumteka zaidi.
Jumbura ndani ya Dodoma, alikwenda na mke wake, Mama Kaundime! Wakawa wanakula matunda ya upambe kwa mgombea Urais. Yeye na mkewe walifikia kwenye ile hoteli babkubwa iliyopo Area D, wale washangiliaji waliowakusanya, waliwatawanya kwenye hoteli tofautitofauti za uswahilini, zenye bei nafuu.
Mke wangu, mwaka huu nitakufanyia mambo makubwa, nataka nikununulie na wewe gari ndogo la kutembelea, Jumbura alimwahidi mkewe, wakiwa wamebarizi nje ya hoteli, wakisubiri orodha ya majina matano ipitishwe na Kamati Kuu (CC) ya CCM kisha waende Halmashauri Kuu (Nec) na baadaye Mkutano Mkuu. Kote, Jumbura alikuwa na uhakika wa mgombea wake kupita.
Kila majina yalipotabiriwa, mgombea wa Jumbura alikuwemo. Upepo ulibadilika usiku wa manane, Julai 11, mwaka huu, pale ilipovuja orodha ya Kamati Kuu kwamba Dk. John Magufuli, Dk. Asha Rose Migiro, Balozi Amina Salum Ali, January na Membe ndiyo walisogezwa Nec kwa ajili ya kuchuja kwa kura, kupata majina matatu ya kupelekwa Mkutano Mkuu.
Toba! Mgombea wa Jumbura hakuwemo. Taarifa hiyo hakukubaliana nayo kabisa, akazoza na mkewe: Hawa wasambaza uzushi mitandaoni siwapendi, wanatoa majina na Rais wetu hayumo, waongo sana. Ila kwa mbali kiroho kilidunda, hofu ilimjaa kwa mbali. Hakutaka kabisa kusikia minongono ya mgombea wake kukatwa.
Kuna kipindi mkewe nusura achezee mkongoto, alipomwambia: Inawezekana ni kweli, si Kamati Kuu ndiyo imemamiliza kikao chake usiku huu? Jumbura aliwaka: Wewe mwanamke umetumwa nini? Au na wewe ni kambi ya mabarabara? Inawezekana vipi huyu Balozi Amina aingie, Rais wetu akatwe, inaingiaje akilini? Kelele wewe mwanamke.
Mama Kaundime hakuongeza neno, aligeuka, akavuta shuka mpaka utosini, gubigubi, na baridi la Dodoma linavyopuliza, huyo akapotelea njozini. Jumbura usingizi haukuwa rafiki kwake tena. Alipitia mitandao, kila alipozunguka majibu yalikua yaleyale. Hata kambi zilizoshindwa, ziliripoti matokeo hayohayo.
Saa 11 juu ya alama, Jumbura aliwasili Makao Makuu ya CCM, White House, wengine wanaita Jumba la Hukumu. Alishangaa watu wamejazana kama mchana, kumbe ni yeye na mkewe ndiyo walikuwa na tabia ya kulala usiku, wapambe wote walikesha kusubiri matokeo. Alikuta makundimakundi, kila alipouliza, jibu alilopewa ni moja.
Yaani amekatwa, Mungu wangu, nimekwisha, sijui nitalipaje madeni! Jumbura alipayuka. Watu wote waligeuka kumtazama yeye, kila mmoja alitaka kujua kinachomliza. Yale maneno yaani amekatwa, yaliyofuatiwa na kilio cha sauti na kwikwi, yalivutia wengi kutaka kujua anayemlilia. Jumbura alikusanya umati wa watu kwenye viunga vya White House.
Alipoona maswali yamekuwa mengi, akajishtukia, akagundua ameshaharibu. Akawa mpole, huyooo, akatoweka taratibu. Alipojiona yupo peke yake, akapiga namba ya mgombea Urais wake, majibu yakawa: Namba unayoipigia haipatikani kwa sasa, tafadhali jaribu tena baadaye. Akaona labda bado amelala, akavuta subira.
Saa mbili ikafika, ikaja tatu, mara nne, kutahamaki tano, namba ya mgombea wake ikawa bado haipatikani. Macho yalimtoka utafikiri mlevi mwoga amekutana na jini. Alikaa ikashindikana, alisimama lakini hakumudu, kutembea haikuwezekana pia. Alifuatilia hotelini alipofikia, akaambiwa mgombea Urais alisaini auti tangu alfajiri.
Taarifa za mgombea Urais kutoroka zilisambaa, wale vijana waliokodiwa kwa ajili ya kushangilia walipopata habari, walimtafuta Jumbura na kumuweka kati, tulipe chetu, wakamzidishia mateso ya moyo, pale alipo mbuni mfukoni hana, halafu wanamwambia awalipe. Ukizingatia yeye ndiye mwathirika mkuu wa kukimbiwa.
Jamani hata mimi nimekimbiwa, Jumbura aliwajibu wale washangiliaji kwa sauti iliyozidiwa na kilio. Nao wakamjibu: Sisi tunakujua wewe uliyetukusanya na kutuleta hapa Dodoma. Zogo lilipamba moto, ndipo Mama Kaundime alipotokea, akamkuta mume wake amezungukwa na hapewi nafasi.
Si unajua mwanamke akiamua huwa hashindwi? Basi akawatuliza wale washangiliaji kisha akamchukua mumewe na kukaa naye pembeni.
Akamsomesha: Hapa sisi tumekimbiwa na hawa lazima tuwakimbie, hakuna jinsi mume wangu. Jumbura akamjibu: Tutakimbiaje wakati hata shilingi mia hatuna?
Hilo niachie mimi, Mama Kaundime alisema akimshika mkono mumewe mpaka kwa wale washangiliaji, akawaambia: Ndugu zangu mnakuwa na presha ya bure, mheshimiwa Rais ametuma ujumbe anakuja. Alikwenda Morogoro mara moja, anarudi kwa ajili ya kushiriki Nec na Mkutano Mkuu, kesho atafanya mkutano na timu nzima. Nafasi ya jina lake kurudishwa ipo na ndiye Rais wetu, kwa hiyo kila mmoja arejee hotelini kwake, tumieni mwandike bili, zitalipwa zote na malipo yenu mtapewa.
Walipotawanyika tu, Mama Kaundime alimshika mkono mumewe mpaka chumbani, akamwambia wewe tulia hapa ndani usitoke, nakuja, Jumbura kwa kiwewe hata hakumuuliza mkewe alikuwa anakwenda wapi, aliitikia tu! Mama akapotea kwa muda wa saa tano, aliporejea, alikuwa na kitita cha shilingi 150,000. Mume akataka kuuliza zimetoka wapi, akaambiwa: Utajua tu, ngoja tulipe bili za hii hoteli halafu tuhame, wale watu hawatakiwi kutukuta hapa.
Jumbura na mkewe walifanikiwa kuhamia kwenye lodge moja nyuma ya ofisi za TRA. Walipopata chumba na kuweka mizigo yao, kwa mara nyingine Mama Kaundime alitoka, alirejea usiku wa manane akiwa amelewa, akafika anabwaga mezani fedha ambazo Jumbura alipozihesabu alikuta ni shilingi 300,000.
Jumbura alipotaka kumuuliza mkewe alipokuwa usiku wote huo na alipopata fedha, alikuta tayari anakoromea usingizini. Hata hivyo, hakujali sana, aliamini fedha zinapatikana kwa njia halali, maana mke wake ana ndugu Dodoma. Alfajiri Jumbura alimwamsha Mama Kaundime waanze safari, maana fedha walizonazo zinawatosha kufika Dar. Mkewe akamjibu: Tutakwenda kesho, leo nina appointment na watu, nataka tufanye na shopping ya chakula njiani.
Palipokucha Mama Kaundime aliondoka hotelini, usiku alirejea na kitita cha shilingi 700,000. Alikuwa amelewa bwiii binti chakaliii. Alfajiri walianza safari ya kurudi Dar. Kwa kuhofia kukutana na wale washangiliaji, walitafuta gari ndogo inayokwenda Dar, wakalipa nauli. Njiani ilikuwa manunuzi tu! Jumbura alifurahia kushika fedha!
Siku mbili baada ya kufika Dar, Jumbura alisahau ya Dodoma akataka kujifanya mbabe kwa mkewe. Akarudi usiku amelewa, tena kwa fedha zilezile ambazo alibaki nazo bada ya safari na matumizi ya njiani.
Mama Kaundime: Umeanza kuvimba kichwa eeh, badala ya utulize kichwa kujua unajipanga vipi na haya maisha, unaamua kulewa pesa nilizopewa na wanaume wenzako.
Maneno hayo, yalimwingia barabara Jumbura, akauliza: Wanaume wenzangu akina nani, wewe mwanamke. Alimfuata mkewe ambaye alikuwa imara, alimpisha na kumsuka, akadondokea kwenye kiti. Mama Kaundime akafunguka: Ina maana hukujua wala kuhisi kwamba nilikuwa nakwenda kujiuza kwa wanaume ndiyo tukapata fedha za kutuondoa na aibu ya kuadhirika Dodoma? Kama hukulijua hilo utakuwa mtu wa ajabu sana. Mkeo anatoka, hujui anakwenda wapi, anarudi amelewa na pesa, hujiulizi amezipataje.
Yalikuwa ni maneno mazito sana kwa Jumbura kuyamudu, presha ilishuka ghafla, akazimia. Alipata huduma, asubuhi alipokuwa sawa na kukumbuka maneno ya mkewe, akaamua kumfukuza nyumbani, mke akagoma kuondoka kwa sababu alitafuta pesa ziwasaidie wote na kweli ziliwasaidia. Mpaka leo, Jumbura anangangania mkewe aondoke, mke hataki. Kila siku vilio, presha inapanda na kushuka.
Hapa ndipo unaweza kuelewa kuwa kuna wapambe wa wagombea Urais, waliathirika na matokeo ya Dodoma kuliko hata wagombea wenyewe. Hivyo basi, usirudie kuwataja akina Lowassa, Membe na wengineo kwamba ndiyo wanaotia huruma sana, tambua wapo wanaoendelea kuteswa na panga la Kamati Kuu Dodoma kuliko hata wale waliokuwa wanashabikiwa.
By Luqman Maloto