Uongozi wa Rais Magufuli utapunguza sana misuguano ya kidini nchini

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
Wadau, amani iwe kwenu.

Ni dhahiri kwamba Rais Magufuli ni chaguo la Mungu. Ni Baraka na Neema ambayo Watanzania tumepewa ili nguvu ya Mungu idhihiri.

Nimekuwa nikifuatilia jinsi viongozi wa serikali wanavyoshiriki matukio ya kidini kwa usawa hakika kuna kitu cha kujifunza. Mathalan, kwenye swala ya Eid iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa alishiriki ibada hiyo ijapokuwa si Mwislam. Baada ya swala, Waziri Mkuu alitoa neno ambapo aliwaasa waislam na wasio waislam kudumisha amani nchini.

Kwenye Baraza la Eid, Rais Magufuli alikuwa Mgeni Rasmi. Katika baraza hilo, Rais alitoa fedha taslimu shilingi milioni mbili kwa kijana aliyesoma vizuri Qur'an ili zimsaidie wakati wa maandalizi ya safari yake ya kidini nchini Uturuki. Pia alitoa fedha kiasi kama hicho kwa kundi la Qaswida la Amani ambalo liliimba kwenye Baraza hilo. Vile vile Rais ametoa kiasi cha fedha ambacho hakikubainishwa kwa ajili ya kuchangia mahujaji watakaoteuliwa na Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA). Pia Rais aliwaomba waislam na wasio waislam kudumisha amani ya nchi na kuwaombea viongozi wa serikali ili waongoze kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Kikubwa zaidi ni pale alipoahidi ushirikiano kwa BAKWATA katika kurejesha mali za baraza hilo ambazo ziliporwa kiujanja na baadhi ya wafanyabiashara ambao waliwarubuni viongozi wa BAKWATA waliotangulia.

Nimetafakari sana hii movie ya viongozi wangu hakika nimefikia kwenye point ya kuamini kuwa utawala huu utapunguza sana misuguano ya kidini. Itakuwa ni vigumu kuibuka kwa mijadala kama ile ya haki ya kuchinja. Ijapokuwa Rais na Waziri Mkuu si Waislam, ila wanaonesha kujali sana imani za dini zote. Huu ni mwanzo mzuri na kila mmoja wetu anapaswa kuwaunga mkono viongozi wetu hawa.

========

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ali kwa juhudi zake za kuwaunganisha waislamu wote na kupanua uwigo wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kutoa huduma za kijamii na ameahidi kuwa serikali ya awamu ya tano itaunga mkono juhudi hizo.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo tarehe 06 Julai, 2016 wakati akihutubia Baraza la Eid el-Fitr kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lililofanyika kitaifa katika viwanja vya Karimejee Jijini Dar es salaam.

Dkt. Magufuli amesema kitendo cha kuwaunganisha waislamu wote katika Baraza la Eid el-Fitr kinafungua ukurasa mpya na ni moja ya hatua muhimu za kuimarisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa waislamu wa makundi mbalimbali pamoja na watanzania wengine waisio waislamu.

Aidha Rais Magufuli amezungumzia juhudi zinazofanywa na BAKWATA katika kuimarisha taasisi zake zinazotoa huduma za kijamii na kulinda mali zake akisema serikali itahakikisha mali zote za waislamu zinakuwa salama na kwamba wote waliodhulumu mali za waislamu watazirejesha.

Awali akisoma taarifa, Katibu Mkuu wa BAKWATA Alhaji Suleiman Said Lolila amesema BAKWATA inakusudia kupanua huduma za kijamii kwa lengo la kuwahudumia wananchi ikiwemo kujenga chuo kikuu Mkoani Dodoma na pia amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake za kuondoa umasikini huku akimtaka asikatishwe tamaa na wachache watakaoudhika kwa kuguswa na hatua zinazochukuliwa.

Nae Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali pamoja na kumshukuru Rais Magufuli kwa kuongoza bila ubaguzi amewataka watanzania kuungana na juhudi za serikali kupinga matendo maovu ikiwemo rushwa na ufisadi na pia amelaani ndoa za jinsia moja akisema ni kinyume na maadili ya dini.

Baraza la Eid el-Fitr pia limehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, mabalozi na wabunge.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

06 Julai, 2016

1.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo July 06 2016 amehutubia Baraza la Eid el-Fitr kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lililofanyika kitaifa katika viwanja vya Karimejee Jijini Dar es salaam.
1.jpg

Katika hotuba yake amemupongeza Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ali kwa juhudi zake za kuwaunganisha waislamu wote na kupanua uwigo wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kutoa huduma za kijamii na ameahidi kuwa serikali ya awamu ya tano itaunga mkono juhudi hizo.
2.jpg

Rais Magufuli na Sheikhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum mara baada ya kuwasili.
3-1.jpg

Rais Magufuli na Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya Baraza la Eid Elfitri.

4.jpg

President Magufuli amesema kitendo cha kuwaunganisha waislamu wote katika Baraza la Eid el-Fitr kinafungua ukurasa mpya na ni moja ya hatua muhimu za kuimarisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa waislamu wa makundi mbalimbali pamoja na watanzania wengine waisio waislamu.

Aidha Rais Magufuli amezungumzia juhudi zinazofanywa na BAKWATA katika kuimarisha taasisi zake zinazotoa huduma za kijamii na kulinda mali zake akisema serikali itahakikisha mali zote za waislamu zinakuwa salama na kwamba wote waliodhulumu mali za waislamu watazirejesha.
5.jpg

6.jpg

9.jpg

Rais Magufuli na Mufti Mkuu Sheikh Aboubakar Zubeir.
10.jpg
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Ni dhahiri kwamba Rais Magufuli ni chaguo la Mungu. Ni Baraka na Neema ambayo Watanzania tumepewa ili nguvu ya Mungu idhihiri.

Nimekuwa nikifuatilia jinsi viongozi wa serikali wanavyoshiriki matukio ya kidini kwa usawa hakika kuna kitu cha kujifunza. Mathalan, kwenye swala ya Eid iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa alishiriki ibada hiyo ijapokuwa si Mwislam. Baada ya swala, Waziri Mkuu alitoa neno ambapo aliwaasa waislam na wasio waislam kudumisha amani nchini.

Kwenye Baraza la Eid, Rais Magufuli alikuwa Mgeni Rasmi. Katika baraza hilo, Rais alitoa fedha taslimu shilingi milioni mbili kwa kijana aliyesoma vizuri Qur'an ili zimsaidie wakati wa maandalizi ya safari yake ya kidini nchini Uturuki. Pia alitoa fedha kiasi kama hicho kwa kundi la Qaswida la Amani ambalo liliimba kwenye Baraza hilo. Vile vile Rais ametoa kiasi cha fedha ambacho hakikubainishwa kwa ajili ya kuchangia mahujaji watakaoteuliwa na Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA). Pia Rais aliwaomba waislam na wasio waislam kudumisha amani ya nchi na kuwaombea viongozi wa serikali ili waongoze kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Kikubwa zaidi ni pale alipoahidi ushirikiano kwa BAKWATA katika kurejesha mali za baraza hilo ambazo ziliporwa kiujanja na baadhi ya wafanyabiashara ambao waliwarubuni viongozi wa BAKWATA waliotangulia.

Nimetafakari sana hii movie ya viongozi wangu hakika nimefikia kwenye point ya kuamini kuwa utawala huu utapunguza sana misuguano ya kidini. Itakuwa ni vigumu kuibuka kwa mijadala kama ile ya haki ya kuchinja. Ijapokuwa Rais na Waziri Mkuu si Waislam, ila wanaonesha kujali sana imani za dini zote. Huu ni mwanzo mzuri na kila mmoja wetu anapaswa kuwaunga mkono viongozi wetu hawa.
hahahaha naona siku hizi unashinda mitandaoni ili na wewe uchaguliwe kama wenzako lakini wewe elimu yako ni form 4 pale mazengo lakini unaweza pata bahati maana magu uchagua watu wasio na vision kama wewe jitahidi

swissme
 
Sina shida ya kuchaguliwa ama kuteuliwa. JF ndio mahala pangu
 
Unajitahidi kijana ila huna bahati hata u DAS wamekunyima.
Kuwa mvumilivu bado kuna nafasi za maafisa tarafa,watendaji wa kata na watendaji wa vijiji.
Unaweza ukabahatika wakakupa utendaji wa kijiji cha ndelenyuma.
 
Mkuu, nafahamu akina Kassim wengi ni Waislam ila Kassim Majaliwa ni Mkristo. Hilo nina hakika nalo kabisa
Lizaboni kuna wakati anapoteza, hivi unawezaje kutoka Lumumba alafu usijue kwa Kassimu ni mwislamu? Hao ndo vijana wa bk 7
 
Unajitahidi kijana ila huna bahati hata u DAS wamekunyima.
Kuwa mvumilivu bado kuna nafasi za maafisa tarafa,watendaji wa kata na watendaji wa vijiji.
Unaweza ukabahatika wakakupa utendaji wa kijiji cha ndelenyuma.
Mkuu, hata kushinda JF ni bonge na kazi. Labda huko kwenu ufipa mnakolipana buku mbili. Lazima njaa iwashike
 
Kassim Majaliwa ni Muislam,katika utaratibu wa swala za Kiislam ni vigumu kwa asie muislam kushiriki,kwani zina masharti mengi ikiwe kanuni za usafi....
 
Kikubwa zaidi ni pale alipoahidi ushirikiano kwa BAKWATA katika kurejesha mali za baraza hilo ambazo ziliporwa kiujanja na baadhi ya wafanyabiashara ambao waliwarubuni viongozi wa BAKWATA waliotangulia.
Sawa, Lakini Kazi ya Mahakama ni nini?
 
Back
Top Bottom