Uongozi wa kiMUNGU, unavyotuokoa

Uongozi wa kiMUNGU, unavyotuokoa

Mwezeshaji1

Senior Member
Joined
Sep 26, 2023
Posts
140
Reaction score
307
Aisee! Leo nakumbuka wakati nina umri wa wastani wa miaka 11, hapa tulikuwa na utaratibu wa kupanga siku ya kugombana (ndondi) na utoto ulikuwa unachangia uwe na utayari usiopingika kwa kutetea HESHIMA mtaani.

Siku moja ikatokea ugomvi ambao haukuisha, tukaweka siku ya kuziweka mezani na ikawa inasubiriwa.

Haikufika siku ile, roho yangu ikagoma (sikuelewa kwa ajili gani, hata hivyo ile sauti haikuacha kusema "acha, usiende kupigana", hata kama nilitaka kutoonekana mnyonge, ikabidi mwisho wa siku NISIENDE)

Hili tukio likafuatiwa na makatazo mbalimbali (je NAWE hukutokea?)

1. Huyu si rafiki wa kuweka karibu, acha (nikitii napata amani, nikijidai najua - nitarejea na TUKIO)
2. Huu mchongo sio (ukijitia huelewi, hela inaenda au madhira mengine usiyotarajia hutokea)
Au Acha huu uhusiano (nikijidai "ooh lakini anafaa" - ati naona zaidi ya Mwenyezi Mungu, aaah nitarudi naweweseka tu, haina kupindisha)
 
Back
Top Bottom