Elections 2010 Uongozi wa Chadema waanzishe Electronic Database ya Wanachama

George Maige Nhigula Jr.

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
470
149
Ndugu Wana JF,

Napenda kutoa pendekezo kwa uongozi wa Chadema kuanzisha Database ya computer itayotunza kumbukumbu muhimu za wanachama wake kama vile Majina kamili, Anwani za mwanachama, Number ya Simu,Email, Number ya Kadi ya kujiandikisha kupiga kura, sehemu aliyojiandikisha kupiga kura, Elimu ya mwanachama, Shughuri za uzalishaji za mwanachama, na data zingine muhimu.

Chadema wakiweza kuwa na database yenye information muhimu ya wanachama wake, itaweza kufaidika sana na mambo yafuatayo:

1.Itarahisisha mawasiliano na wanachama wake on regural basis through email,sms, barua au leaflets, hata pale wanapohitaji kupata maoni ya wanachama moja kwa moja kuhusu sera au mabadiliko flani, itarahisisha mawasiliano

2.Chadema itaweza kujua mtaji wao wa kisiasa ni kiasi gani na unaongezeka kwa kasi gani na itaweza kujiwekea malengo ambayo kutakuwa na chombo cha kupima kama wanachama wanaongezeka au la, kwa mfano: Sidhani kama chadema wana data za uhakika kujua operation sangara ilifanikiwa ku sajili wanachama wangapi

3. Kwa kuwa na database ya wanachama itarahisisha kuwa rank wanachama ili baadhi ya wanachama waweze kupewa majukumu ya kuwaleea kisiasa baadhi ya wanachama wachanga walio maeneeo yao

4.Database ya wanachama itasaidia kuweza kupata na ku recruit potential Leaders ndani ya chama na wagombea wa nafasi mbali mbali wa uongozi pindi inapotokea fursa hiyo, itasaidia chama kujua wanachama wake wenye potentials na vigezo vya kukubalika na kuwaandaa kugombea nafasi za uongozi.

5.Database hii itaweza kutumiwa na kitengo cha mawasiliano ya chama kuwahamasisha wanachama kujitokeza kwa wingi wakati wa kupiga kura,

6. Database hii ya wanachama inaweza kutumika kama nyenzo ya kupata taarifa muhimu za hujuma kwa chama au scandals mbali mbali na kero za wananchi

7.Database ya wanachama itaweza kutambua ni wanachama wapi ni hai na wanalipia kadi na michango yao kwa chama, na kuweza kuwakumbusha wajibu wao kwa chama.

8.Database hii itaweza kuwaweka wanachama karibu zaidi na kuwapasha taarifa mara kwa mara kupitia personalized email zaoo za chama, kwa mfano kila mwanachama wa chadema anaweza pewa email adress yake ya chama example: vnyerere@chadema.com

9.Kuwa na Database ya chama itaifanya chadema ifanye research zake kwa urahisi zaidi na kwa uhalisia, kwa mfano kama chama kinataka kusimamisha mgombea flani katika jimbo flani itaweza kufanya study zake kwa kuwasiliana na wanachama wa jimbo hilo bila kutumia gharama kubwa ya kuwa ajili REDET au Synovate

10. Chadema ni chama cha kisasa hivyo kinatakiwa kurahisisha utendaji ya kazi zake kwa kuikumbatia technologia ya computer na kuwa na database ya wanachama.

Ndugu wana JF, Chadema ina vijana wengi wasomi na wanavipaji na ubunifu wa ku design software imara itakayoweza kutumiwa na chama hivyo viongozi wetu watoe Tangazo hapa JF kuna wazalendo wanaweza kujitolea ku design sofware na hiyo database kwa manufaa ya chama kwa kujitolea au kwa ujira mdogo sana, kwani hii leo tukiwauliza uongozi wa chadema wanajua idadi halisi ya wanachama wake ambao ndio mtaji wa kisiasa, Nadhani kuna utata mkubwa, tena inawezekana Chadema wakawa na wanachama wengi kuliko ccm lakini bado uongozi haujajua jinsi ya kuwaweka wanachama karibu na chama na wakawa involved on the process.

Napenda kuwakilisha wazo langu wazalendo.
 
I definitely agree with you. Wenye vipaji jitoleeni na sisi wengine tuko tayari ku support kwa njia yeyote ile. Umoja ndio nguvu yetu. But I need to apply for Chadema membership as soon as possible; mimi na nyumba yangu we pledge our allegiance to Chadema and to change for all Tanzanians!!!!
 
Dah,mkuu una mawazo yanayo reflect jina lako!
Binafsi nakubaliana na mawazo yako kwa 100% na kama watakua tayari kuchukua idea hii mimi ni nasoma B.sc in comp. science UDSM niko tayari kufanya kazi (kama project ) kwanzia system itakavoanza kutengenezwa hadi mwisho bila malipo yoyote yale.

I am ready for it kama nikipewa nafasi,ni wazo zuri sana hasa ukizingatia ni vigumu kupata contact za viongozi wa chama and the like,hii itasaidia sana.
 
Hili wazo naliunga mkono 100%, mimi najitolea kudevelop hiyo system bila gharama yoyote.
Nimekuwa mkereketwa wa chadema hasa kipindi hiki cha uchaguzi
Ktk kipindi hiki cha uchaguzi baada ya kuridhika na sera zao.
Nataka nijiunge rasmi na chama and I will play a key role in building
Complex information systems kwa ajili ya chama. Naombeni maelekezo
Jinsi ya kujiunga na ikiwezekana kuonana na muhusika wa habari ktk chama
Ili kazi ianze mara moja. Huu utakuwa ndo mchango wangu ktk chama
 
Naunga mkono wazo hili kwa 100 per cent!Ni wazo makini sana. Lakini lifanywe kwa uangalifu mkubwa.

Caution: Hofu yangu ni kuwa lisije likawa ni wazo la UWT(Usalama wa Taifa)wanataka kujua majina ya wafuasi wa CHADEMA ili waanze kuwashughulikia kwa mbinu zao chafu???Maana najua UWT wana hasira na CHADEMA maana nusura juzi wamkoseshe Kiranja wao Urais.

Take care.
 
Bw. Makoye naomba nikutoe wasiwasi. Ukweli ni kuwa usalama wa taifa hawawezi kufanya hivyo hasa katika dunia ya sasa. Pili kama wako makini kuweza kufanya hivyo, basi haitakuwa na haja hata ya kutafuta jina lako kwenye database ya chma. As long as unasapot CHADEMA, wanaweza kukugundua wakitaka, lakini mi naona hakuna watakachoweza kufanya, by the way watendaji wengi wa UWT ni wakereketwa wa CHADEMA...

Mi naunga wazo hilo mkono, naamini kama ni resources zipo, kilichobaki ni uongozi kufanya organization...
 
Ndugu Wana JF,

Napenda kutoa pendekezo kwa uongozi wa Chadema kuanzisha Database ya computer itayotunza kumbukumbu muhimu za wanachama wake kama vile Majina kamili, Anwani za mwanachama, Number ya Simu,Email, Number ya Kadi ya kujiandikisha kupiga kura, sehemu aliyojiandikisha kupiga kura, Elimu ya mwanachama, Shughuri za uzalishaji za mwanachama, na data zingine muhimu.

Chadema wakiweza kuwa na database yenye information muhimu ya wanachama wake, itaweza kufaidika sana na mambo yafuatayo:

1.Itarahisisha mawasiliano na wanachama wake on regural basis through email,sms, barua au leaflets, hata pale wanapohitaji kupata maoni ya wanachama moja kwa moja kuhusu sera au mabadiliko flani, itarahisisha mawasiliano

2.Chadema itaweza kujua mtaji wao wa kisiasa ni kiasi gani na unaongezeka kwa kasi gani na itaweza kujiwekea malengo ambayo kutakuwa na chombo cha kupima kama wanachama wanaongezeka au la, kwa mfano: Sidhani kama chadema wana data za uhakika kujua operation sangara ilifanikiwa ku sajili wanachama wangapi

3. Kwa kuwa na database ya wanachama itarahisisha kuwa rank wanachama ili baadhi ya wanachama waweze kupewa majukumu ya kuwaleea kisiasa baadhi ya wanachama wachanga walio maeneeo yao

4.Database ya wanachama itasaidia kuweza kupata na ku recruit potential Leaders ndani ya chama na wagombea wa nafasi mbali mbali wa uongozi pindi inapotokea fursa hiyo, itasaidia chama kujua wanachama wake wenye potentials na vigezo vya kukubalika na kuwaandaa kugombea nafasi za uongozi.

5.Database hii itaweza kutumiwa na kitengo cha mawasiliano ya chama kuwahamasisha wanachama kujitokeza kwa wingi wakati wa kupiga kura,

6. Database hii ya wanachama inaweza kutumika kama nyenzo ya kupata taarifa muhimu za hujuma kwa chama au scandals mbali mbali na kero za wananchi

7.Database ya wanachama itaweza kutambua ni wanachama wapi ni hai na wanalipia kadi na michango yao kwa chama, na kuweza kuwakumbusha wajibu wao kwa chama.

8.Database hii itaweza kuwaweka wanachama karibu zaidi na kuwapasha taarifa mara kwa mara kupitia personalized email zaoo za chama, kwa mfano kila mwanachama wa chadema anaweza pewa email adress yake ya chama example: vnyerere@chadema.com

9.Kuwa na Database ya chama itaifanya chadema ifanye research zake kwa urahisi zaidi na kwa uhalisia, kwa mfano kama chama kinataka kusimamisha mgombea flani katika jimbo flani itaweza kufanya study zake kwa kuwasiliana na wanachama wa jimbo hilo bila kutumia gharama kubwa ya kuwa ajili REDET au Synovate

10. Chadema ni chama cha kisasa hivyo kinatakiwa kurahisisha utendaji ya kazi zake kwa kuikumbatia technologia ya computer na kuwa na database ya wanachama.

Ndugu wana JF, Chadema ina vijana wengi wasomi na wanavipaji na ubunifu wa ku design software imara itakayoweza kutumiwa na chama hivyo viongozi wetu watoe Tangazo hapa JF kuna wazalendo wanaweza kujitolea ku design sofware na hiyo database kwa manufaa ya chama kwa kujitolea au kwa ujira mdogo sana, kwani hii leo tukiwauliza uongozi wa chadema wanajua idadi halisi ya wanachama wake ambao ndio mtaji wa kisiasa, Nadhani kuna utata mkubwa, tena inawezekana Chadema wakawa na wanachama wengi kuliko ccm lakini bado uongozi haujajua jinsi ya kuwaweka wanachama karibu na chama na wakawa involved on the process.

Napenda kuwakilisha wazo langu wazalendo.

Nimesoma. Nimekubali. Wataalamu tupo.

Sasa hivi hakuna jambo linaweza kufanyika kwa ufanisi bila technology.
 
Naunga mkono wazo hili kwa 100 per cent!Ni wazo makini sana. Lakini lifanywe kwa uangalifu mkubwa.

Caution: Hofu yangu ni kuwa lisije likawa ni wazo la UWT(Usalama wa Taifa)wanataka kujua majina ya wafuasi wa CHADEMA ili waanze kuwashughulikia kwa mbinu zao chafu???Maana najua UWT wana hasira na CHADEMA maana nusura juzi wamkoseshe Kiranja wao Urais.

Take care.

Hao mavuvuzela wa UWT wanajua nini? Hao kazi yao 'kupulizwa tu'

Kama wanaubavu watoe picha ya kifafa ya kiranja wao kwenye YouTube

Last edited by a moderator:
Dah,mkuu una mawazo yanayo reflect jina lako!
Binafsi nakubaliana na mawazo yako kwa 100% na kama watakua tayari kuchukua idea hii mimi ni nasoma B.sc in comp. science UDSM niko tayari kufanya kazi (kama project ) kwanzia system itakavoanza kutengenezwa hadi mwisho bila malipo yoyote yale.

I am ready for it kama nikipewa nafasi,ni wazo zuri sana hasa ukizingatia ni vigumu kupata contact za viongozi wa chama and the like,hii itasaidia sana
.

mtu kama huyu apewe contact haraka kwa anyejua mawasiliano na hao viongozi ili kazi ianze mara moja.
 
Mimi Pia naunga mkono kwa kwa 100%.
Mie Pia ni Computer Engineer, najitolea kushirikiana na wezangu waliojitolea kutengeneza hii database. Tunasubiri maelekezo ya uongozi.
 
watu watatu tayari tumejitolea hapa ka-udelevop system hii,naamini hata kama hakuna mmoja kati yetu atakaye ombwa kufanya kazi hiyo wazo hili ni zuri na wasilitupe viongozi wa chadema.

Tena ingekua vyema ikaanza mapema mwakani kama sio mwaka huu
 
Mna mawazo mazuri wana Chadema lakini lazima muweke watu proffesionals ku manage hizo database hili sio swala la ushabiki!

Mwisho wa siku msipokuwa makini utasikia hizo information zenu ambazo nyingine nyeti mtakuta watu wanafungia maandazi.

Good Idea
 
Back
Top Bottom