R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,578
MENEJIMENTI mpya ya Kampuni ya Uwekezaji ya NICOL imekanusha madai ya Felix Mosha ya kuendelea kujinadi kuwa bado ni mwenyekiti halali wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa mwishoni mwa wiki na Kaimu meneja wa NICOL, Kinoni Adam Wamunza, iliwathibitishia wanahisa, na umma kwa ujumla, kuwa taarifa hiyo ya Mosha ni hadaa.
Alidai lengo la Mosha ni kujisafisha baada ya kesi aliyofungua katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kutupwa nje, na mahakama kumwamuru alipe gharama za uendeshaji wa kesi hiyo.
Hii ni mara ya pili kesi aliyofungua Mosha inatupwa nje na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania.
Hivi karibuni, Mosha aliwaambia waandishi wa habari kuwa yeye bado ni Mwenyekiti wa NICOL, na atabaki Mwenyekiti hadi hapo mahakama itakapotoa uamuzi wa kesi (ambayo hakuitaja) aliyofungua Mahakama Kuu.
Katika mkutano huo, Mosha alidai pia kuwa kwa wadhifa wake huo aliwahakikishia wanahisa kuwa amana zao zimekua kutoka sh bilioni 8.5 hadi sh bilioni 65 kutokana na uwekezaji katika hisa za NMB.
Hata hivyo, Wamunza amedai katika taarifa yake kuwa Mosha aliongoza NICOL kwa zaidi ya miaka 10 na katika kipindi hicho, ilifika wakati alipuuza kufuata masharti ya usajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), na akawa anaiongoza NICOL kama kampuni binafsi.
"Mahesabu ya kampuni hayakuwa yanatayarishwa na kukaguliwa katika muda muafaka. Mahesabu ya NICOL yaliyokaguliwa ni ya mwaka 2008. Aidha, alisimamia uwekezaji katika makampuni ambayo yaliwekwa chini ya ufilisi kipindi kifupi baada ya NICOL kuwekeza katika makampuni hayo," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Alisema baada ya kuona Mosha anapuuza mara kwa mara maagizo yao, taasisi za udhibiti wa makampuni yaliyosajiliwa katika soko la mitaji; yaani, Msajili wa Makampuni (BRELA), Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA), Soko la Mitaji la Dar es Salaam (DSE) na Mamlaka ya Masoko na Mitaji (CMSA), zililazimika kuingilia kati kwa pamoja na kuwataka wanahisa wachukue hatua stahiki kubadili uongozi wa NICOL uliokuwepo ambao ulionekana kushindwa kutekeleza majukumu yao.
Taarifa hiyo ilieleza kwa kuwa hilo halikufanyika, CMSA ililazimika kuchukua hatua kadhaa za ziada, ikiwa ni pamoja na kuisimamisha bodi na uongozi wa NICOL na Mosha alikaidi kutekeleza maagizo na maelekezo ya taasisi za udhibiti.
"Baada ya miezi tisa kupita Mosha alipoanza kuathiriwa na hatua za ziada zilizochukuliwa na CMSA, ndipo alifungua kesi Mahakama Kuu kwa madhumuni ya kupinga maamuzi ya kisheria ya vyombo hivyo, na vilevile kujikinga yeye binafsi," alisema Wamunza.
Alisema kutokana na kutoridhishwa na hali iliyokuwepo ya migogoro ambayo ilikuwa inaathiri vibaya utendaji wa NICOL, baadhi ya wanahisa walifungua kesi katika Mahakama ya Biashara, Na. 4 ya 2012, wakaomba mahakama iruhusu mkutano wa wanahisa ufanyike kwa madhumuni ya kubadili uongozi wa NICOL.
Wamunza alieleza mahakama iliridhia ombi la wanahisa na ilitoa amri kuwa ateuliwe ‘Interim Manager' ambaye atachukua uongozi wa NICOL kwa muda kwa madhumuni ya kushughulikia mabadiliko ya kudumu katika uongozi wa NICOL.
"Amri hii ya mahakama mpaka sasa haijatenguliwa, wala hakuna zuio lolote la utekelezaji wake. Mkutano wa dharura wa wanahisa wa NICOL uliitishwa Aprili 14, mwaka 2012, kwa mujibu wa amri hiyo ya mahakama, ambapo wanahisa waliazimia, kati ya mengine, kumuondoa Mosha kutoka uenyekiti wa NICOL, na bodi yake ilivunjwa," ilieleza taarifa hiyo.
Katika mkutano wao wanahisa vilevile waliteua bodi mpya, ambayo sasa ndiyo inatambuliwa kisheria kama alivyohakiki Msajili wa Makampuni (BRELA) kutokana na kumbukumbu za masijala.