Uongozi ni nini?


C

COKINTA

Member
Joined
Jan 26, 2010
Messages
9
Likes
0
Points
0
C

COKINTA

Member
Joined Jan 26, 2010
9 0 0
Tumekuwa na mijadala mingi sana kuhusu viongozi wetu, wanavyoenenda na wanavyoongoza taifa letu na hata asasi mbalimbali katika jamii. Ninachojiuliza je wanajua hata maana ya kuwa kiongozi?? Kwani wengi wao wanaonekana kuwa dhaifu sana katika majukumu ya kiongozi na hata tabia za kiongozi. Wengi wa viongozi tulio nao kwao uongozi ni kushika nafasi ya madaraka na si kubeba wajibu na majukumu, na ku-align tabia na mwenendo wao kama watu waliobeba dhamana ya wananchi. Ninahisi ni wakati muafaka kwa great thinkers tutoe makala kuhusu maana ya uongozi na majukumu yanayoendana na mtu anapopewa nafasi ya uongozi na si watu kufurahia nafasi za uongozi na marupurupu bila kuwajika kama viongozi, hasa tunapoelekea kipindi cha uchaguzi mkuu 2010.
 

Forum statistics

Threads 1,251,889
Members 481,937
Posts 29,789,360