Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Uongozi ni sehemu ya mahusiano ya watu. Huwezi kuwa kiongozi mzuri kama huna maarifa katika mahusiano ya watu. Hiki ni kionjo muhimu sana katika uongozi. Watu wengi wanapungukiwa nacho. Ili uwe kiongozi unahitaji sana imani ya watu kwako. Wakuamini uko kwaajili yao na unauwezo wa kutatua changamoto wanazokabiliana nazo. Tofauti na mtawala ambaye mara zote anajiweka juu ya watu. Lakini kiongozi ni sehemu ya watu ambao kwa pamoja wanafanya kazi kutatua changamoto zinazowakabili.
Mtawala yuko kwaajili ya manufaa yake, manufaa ya jamii kwa ujumla kwake sio ya msingi sana kuliko manufaa binafsi. Utajiri kwake ni kitu cha kwanza, kujikusanyia kadiri ya uwezo wake kwaajili yake na kizazi chake kijacho. Mahusiano yake na jamii sio kitu muhimu sana kwake zaidi ya ''interest '' zake. Lakini kwa kiongozi interest za raia ndio namba moja.
Kwahiyo kiongozi hu order jamii yake na kuhakikisha mahusiano katika jamii yake yanaimarika na watu wanakuwa na malengo mamoja.Hujenga mifumo mizuri ya mashirikiano katika yale mambo yanayohusu jamii kwa ujumla.
Ni katika mashirikiano mabovu kwenye jamii ndio maana mambo hayaendi sawa. Wakati watu wanapokuwa hawana malengo sawa kwa mambo yanayohusu jamii kwa pamoja.
Watu wanapoacha kuwajibika kwa mambo yanayohusu jamii yao na maendeleo ya jamii yao kwa pamoja. Kutokuwa makini huku kumeharibu mambo mengi. Katika elimu na katika malezi ya watoto na mfumo wa jamii kwa ujumla.
Mfumo wa jamii umeharibika haufanyi kazi ipasavyo hakuna harmony. Watu watakapo weka interests za jamii mbele kuliko interest zao binafsi ni hatua kubwa za maendeleo.
Jamii ambayo kwamfano; imetenga viwanja vya michezo kwaajili ya watoto wao, wanamuona mtu anajenga na wao wanauongozi katika ngazi ya chini na kumuacha aendelee kujenga ni ya kuishangaa. Inaonyesha kutowajibika fulani.
Kwanza ni lazima tujenge familia zetu na kuziheshimu na kuzithamini na mahusiano yetu katika familia lakini pili ni lazima tujenge mahusiano yetu na majirani zetu kwakuwa huko chini ndio kunakojenga jamii hadi kuja kwenye taifa. Huku chini pakiimarika juu pataimarika. Kukiwepo na maadili, nidhamu na wajibu wa pamoja katika malengo tuliyojiwekea kwanini tusifike ?
Matatizo tuliyonayo sasa ambayo tunahangaika nayo na Magufuli anaangaika nayo ni matatizo ya kimaadili na kinidhamu ambayo mizizi yake iko chini. Na dawa yake sio nguvu peke yake bali kuunda upya mfumo wa kijamii na wa kimaadili. Tuna matatizo makubwa ya kimaadili katika taifa letu. Hii ni kazi ya familia na jamii kwa ujumla. Kuangalia mienendo na tabia za watoto wetu. Ni katika tabia zao baadae yetu itakuwa na mwanga. Tuna tatizo kubwa. Ambalo nguvu pekee haitoshi kulimaliza.
Huu ndio msingi imara ambao tunapaswa kuujenga ambao nina uhakika utadumu kwa muda mrefu zaidi. Na vizazi vyetu vitafurahia msingi huu. Ni jinsi gani tunawatayarisha vijana wetu kuingia kwenye utumishi wa umma kuanzia huko chini kwenye ngazi ya familia na mahusiano yetu katika jamii. Ni katika maadili yao katika hatua za awali kabisa kwenye ukuaji wao. Naomba tuliangalie hili. Tunajenga nyumba ambayo haina misingi imara.
Anachofanya Magufuli kuhusu ufisadi ni udhibiti wa kipindi kifupi tu. Ni muhimu kujenga tabia za watu wetu ili msingi wetu uwe imara. Ili mambo haya yasiwe yanajirudia rudia. Mabadiliko haya yanahitaji watu wote. Na yanahitaji kujitambua kwa watu wetu kwa taifa lao. Elimu ya watoto wetu na makuzi yao ni muhimu sana. Jamii imeharibika na inahitaji great social reform. Taifa linapaswa kubadilika .
Naamini kabisa nilichoandika hapa ndio tiba ya kudumu kwa matatizo ambayo yanatukabili kwa sasa ambayo watu wanayapigia kelele ya ufisadi na nidhamu. Ningependa watu tutafakari kuhusu hili ili tuje na mambo mengi zaidi ambayo yanaweza kulibadili taifa letu.