Uongo, Unafiki na Uzandiki wa CCM!


[h=2]Askofu Kakobe kuzungumzia muundo wa Muungano katika Neno la Pasaka 20.4.14[/h]
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa waumini wanaosali katika Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), linaloongozwa na Askofu Mkuu Zachary Kakobe, zinaeleza kwamba, Jumapili iliyopita katika Ibada Kuu ya Kanisa hilo, lililoko Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge, Dar-Es-Salaam, karibu na Mlimani City; Mzee wa Kanisa anayehusika na matangazo, alitangaza kwamba, katika Ibada Kuu ya Sikukuu ya Pasaka, Jumapili hii tarehe 20.4.2014, Askofu Kakobe atahubiri Neno la Mungu, ambalo pamoja na mambo mengine ya rohoni, litazungumzia pia juu ya mustakabali wa nchi yetu, hususan kuhusu Bunge Maalum la Katiba, linaloendelea na vikao vyake, mjini Dodoma. Hata hivyo, taarifa za uhakika zilizopatikana jana, kutoka kwa baadhi ya Viongozi wa Kanisa hilo, zinafafanua kwamba, Askofu Kakobe, atachukua muda mrefu zaidi katika mahubiri yake, kuzungumzia juu ya muundo wa Muungano unaoifaa nchi yetu.

Ibada Kuu ya Pasaka katika Kanisa hilo, itaanza saa 3 kamili asubuhi, na kumalizika saa 6.30 mchana. Hata hivyo, kwa kuzingatia Kanuni za Maadili ya Mavazi, za Kanisa hilo; Viongozi hao wa Kanisa, wamewakumbusha watu wote watakaohudhuria, kumheshimu Mungu kwa mavazi watakayoyavaa. Watakaovaa vimini, jeans, milegezo, na nywele bandia; hawataruhusiwa kuingia katika Nyumba hiyo ya Mungu. Vilevile, wanawake hawapaswi kuvaa suruali, na wanatakiwa kufunika vichwa vyao. Vivyo hivyo, wanaume hawakubaliki kuingia Kanisani humo, wakiwa wamevaa kofia.​
 
Mara zote mdomo hauna ushirikiano na maeneo mengine ya mwili. Shauri yako ukipata nafasi tena utakuja omba msamaha hapa.
kamwage hicho kifusi kama kimekuelemea naona unaleta longo longo!
 

hiyo picha ya prof issa shivji --------- ndiyo imenifurahisha!
 
Hakuna wanasiasa wanafiki Tanzania kama wale wanaotokana na CHADEMA, kila mara wamekuwa wakihubiri kile ambacho hawawezi kukitenda!
 
Kwa cc wazee wa bajet serikali 1 ndo itatupunguzia gharama na kwa kuwa CCM leo hii wamegundua ni gharama tunawaomba hivyo bac wapunguze gharama ktk uendeshaji wa miimili yote wabunge wapunguziwe gharama ya mishahara mpaka kufikia laki 300000 km ilivyo kwa walimu na magari ya kifahar wanayotumia wakubal kuyapiga mnada pindi wanapomaliza mchakato huu ili 2jue km kwel wameokoka na wako tayar kuwatumikia watz.
 
...ccm hawafanyi siasa,siku zote wamedumu na kufaidika na ulaghai wa kutumia ujinga wa wananchi. siku zao zinahesabika na mwisho wao upo karibu sana....
 
Mtaji wa ccm si ujinga wa wananchi kwani sasa wengi wameelimika bali mtaji wa ccm ni tume ya uchaguzi (isiyotaka kuboresha daftari)wanasheria(mahakama inayo tafsiri sheria itakavyo) na policcm na usalama wa mafisadi a.k.a. Usalama wa taifa (wanaoshindwa kushugulikia mafisadi )
Mtaji mkubwa ccm ni ujinga wa Wananchi.
 
Ndugu Asamwa, tunahitaji viongozi kama akina Jerry Rawlings wa Ghana.

Mkuu PauliMasao ni nini hasa unapenda kuhusu Jerry Rawlings?! Ni jinsi alivyoingia madarakani kwa kupindua serikali iliyokuwepo ama ni style yake ya uongozi?
 
Hakuna wanasiasa wanafiki Tanzania kama wale wanaotokana na CHADEMA, kila mara wamekuwa wakihubiri kile ambacho hawawezi kukitenda!

Jenga hoja, acha matusi-hayasaidii kitu. Je, ikiwa CCM mnatazama ughali wa serikali kwa kuangalia idadi ya serikali-kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2, je, hamuoni kwamba serikali 1 ni nafuu kuliko serikali 2? Kama ndivyo, kwanini sasa msiende kwenye serikali 1 badala ya serikali 2 (ambazo ni mzigo kwa mwananchi ukilinganisha na serikali 1)? Hapa ndipo unafiki wa CCM unapoonekana wazi. Kama sio wanafiki tuambieni jinsi serikali 2 zilivyo rahisi kuendesha (kigharama) kuliko serikali 1. Sio mnakaa kubwabwaja tu kama bata anayehara bila kutetea hoja iliyopo mezani kwa pointi zinazoeleweka.
 
Mimi nadhani angehubiri mfumo wa uendeshaji wa kanisa lake
 
Mimi nadhani angehubiri mfumo wa uendeshaji wa kanisa lake

alitakiwa aanze samuel 6 kwanza---angewaacha kadinali pengo na mufti simba wahubiri mifumo ya uendeshaji wa dini zao badala ya kwenda kuwarubuni akitaka waiunge mkono ccm ktk hoja ya serikali 3. na pia lukuvi angeacha kutumia mimbari ya kanisa kuwatukana waislamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…