Uongo mwingine wa lukuvi huu hapa.

Uongo mwingine wa lukuvi huu hapa.

Joined
Jun 20, 2009
Posts
45
Reaction score
225
Wakuu,
Nimejulishwa pia kwamba waziri Lukuvi alisema uongo mwingine mkubwa, jana tarehe 08 Nov 2013 bungeni, kwamba "kwenye mazungumzo ya vyama na serikali ati kuna wakati wajumbe wa vyama(TCD) walishindwa kuelewana na wakaomba faragha na ati wakapewa chumba maalum katika ofisi ya Waziri Mkuu na eti huko chumbani kuna wakati wajumbe wa vyama(TCD) walishindana kwa kupiga kura na wanne walikubaliana wawili wakakataa na eti yeye Lukuvi ana CD ya kikao hicho cha faragha"

UKWELI NI NINI.

Kama kweli Lukuvi kasema maneno hayo ni mwongo, tena mwongo wa ajabu kweli.

Mimi na Mnyika tuliongoza TC ya vyama, katika siku mbili za majadiliano haikuwahi kutokea tukaomba chumba ili tukubaliane jambo na wala hatukuwahi kwenda faragha na wala hakukuwahi kuwa na jambo tunalobishania sisi kwa sisi kwani hoja zilizotupeleka mezani tayari zilishapitishwa na viongozi wakuu wa vyama vyetu.

Mfumo tuliotumia ni kwamba, tulifanya majadiliano siku ya kwanza, siku nzima! na ilipofika jioni masuala ambayo hatukukubaliana tukasema kila upande urudi kwa wakubwa. Sie TC ya vyama tukaondoka hadi ofisi ya BUNGE chumba cha kiongozi wa kambi ya upinzani, tukapanga "modalities" za kutumia keshoye na mambo yapi tuwajulishe viongozi wakuu ili watushauri, kikao hiki cha ofisi za bunge hakikuwa na mvutano wowote na kilikuwa na mashauriano mazuri na hitimisho la kila jambo bila mvutano.

Keshoye tulianza mazungumzo kama kawaida pale ofisi ya waziri Mkuu, pana mambo serikali ikakegeza msimamo na pana mambo wakasimamia wanayoyataka wao, tukakubaliana katika baadhi ya masuala na tukakubaliana kutokukubakuana kwa baadhi ya mengine, kikao kikafungwa, hii "day two" pia haikuwa na faragha yoyote ile tuliyokaa, iwe pale kwenye ukumbi wa mikutano au katika chumba.

Kama kweli Lukuvi kasema maneno hayo basi Tanzania ina kazi kubwa sana hadi kuifikia demokrasia ya kweli.

Julius S. Mtatiro - Johannesburg.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mtatiro bana, hivi haya yote ni kwasababu ametoa ile siri???

Any way siasa za tanzania zina wenyewe.
 
Mtatiro wy unatapatapa ivyo? Usibabaishwe na mbabaishaji LUKUVI,fanya kama unakimbizana na kichaa
 
sema wazi (zaidi ya jf) kama unajiamin na unaamin unayosema wewe ndio ukwel
 
Hio faragha na mbunge wa ismani ni kaburi la cuf na washirika wake
 
Anadanganya hivi kwa faida ya nani? Au ni vile watu wengine uongo ni asili yao tu...
 
Mod hebu fanyeni uhakiki kama J. Mtatiro ni Verified User kwani amejoin juzi, otherwise naungana na mawazo yake kupinga uzandiki wa mnadhimu wa serikali
 
Wakuu kama pia nasema uongo hapamnihukumu, lakini nina uhuru wa kueleza ukweli ninaoujua katika kila jambo, na siwezi kupangiwa nini cha kusema.

Mtatiro upo desperate kw kile alichokisema Lukuvi. Sisi tunaoona mbali tumeelewa alivyosema "naitoa hii siri, sikuwa nimepanga kuitoa" .

Sasa baada ya kutoa siri hata hujajibu aliyoyasema bungeni na wewe unakuja na vipost kutusahaulisha. Strategy za kitoto sn.
 
Huwa napata Shida sana na uelewa Wang juu ya kazi za Lukuvi. Hivi ndio bright minister kuliko wote? Yeye ndio anajua majibu ya mawaziri wengine mpaka awasemee hata wakiwa ktk Mezani
Msimamo wa serikali kwanini autoe wakati waziri Mkuu yupo?
 
Uongo ni asili ya mtu lakini kwa upande wa Lukuvi anasema CD yenye kuonesha jinsi kikao kilivyofanyika..
 
Funguka zaidi Mkuu ikibidi hata kuwaweka kwenye kitimoto hao wajumbe wengine wanne. Lukuvi ni mmoja aliyehusika katika ile kauli ya Kikwete ya "nimeambiwa, nimeelezwa na nimefahamishwa" ambayo ilikuwa ni uongo mtupu!!! Kama una ushahidi zaidi funguka Mkuu.

Wakuu kama pia nasema uongo hapamnihukumu, lakini nina uhuru wa kueleza ukweli ninaoujua katika kila jambo, na siwezi kupangiwa nini cha kusema.
 
Wakuu,
Nimejulishwa pia kwamba waziri Lukuvi alisema uongo mwingine mkubwa, jana tarehe 08 Nov 2013 bungeni, kwamba "kwenye mazungumzo ya vyama na serikali ati kuna wakati wajumbe wa vyama(TCD) walishindwa kuelewana na wakaomba faragha na ati wakapewa chumba maalum katika ofisi ya Waziri Mkuu na eti huko chumbani kuna wakati wajumbe wa vyama(TCD) walishindana kwa kupiga kura na wanne walikubaliana wawili wakakataa na eti yeye Lukuvi ana CD ya kikao hicho cha faragha"

UKWELI NI NINI.

Kama kweli Lukuvi kasema maneno hayo ni mwongo, tena mwongo wa ajabu kweli.

Mimi na Mnyika tuliongoza TC ya vyama, katika siku mbili za majadiliano haikuwahi kutokea tukaomba chumba ili tukubaliane jambo na wala hatukuwahi kwenda faragha na wala hakukuwahi kuwa na jambo tunalobishania sisi kwa sisi kwani hoja zilizotupeleka mezani tayari zilishapitishwa na viongozi wakuu wa vyama vyetu.

Mfumo tuliotumia ni kwamba, tulifanya majadiliano siku ya kwanza, siku nzima! na ilipofika jioni masuala ambayo hatukukubaliana tukasema kila upande urudi kwa wakubwa. Sie TC ya vyama tukaondoka hadi ofisi ya BUNGE chumba cha kiongozi wa kambi ya upinzani, tukapanga "modalities" za kutumia keshoye na mambo yapi tuwajulishe viongozi wakuu ili watushauri, kikao hiki cha ofisi za bunge hakikuwa na mvutano wowote na kilikuwa na mashauriano mazuri na hitimisho la kila jambo bila mvutano.

Keshoye tulianza mazungumzo kama kawaida pale ofisi ya waziri Mkuu, pana mambo serikali ikakegeza msimamo na pana mambo wakasimamia wanayoyataka wao, tukakubaliana katika baadhi ya masuala na tukakubaliana kutokukubakuana kwa baadhi ya mengine, kikao kikafungwa, hii "day two" pia haikuwa na faragha yoyote ile tuliyokaa, iwe pale kwenye ukumbi wa mikutano au katika chumba.

Kama kweli Lukuvi kasema maneno hayo basi Tanzania ina kazi kubwa sana hadi kuifikia demokrasia ya kweli.

Julius S. Mtatiro - Johannesburg.[/Q
lukuvi is among the people who are in the list of kainerubaga msemakweli of shody degree and diplomas holder kwa hiyo kama aliweza kudanganya umma kuhusu elimu yake je haya mengine atashindwa
 
CCM kama chama pinzanina nyie akina Mtatiro, msitegemee watatoa kauli zitakazopelekea nyie kuungana.

They will always find some gaps ili wajenge kutokuaminiana ninyi kwa ninyi. Lazima muwe makini.
 
Wakuu kama pia nasema uongo hapamnihukumu, lakini nina uhuru wa kueleza ukweli ninaoujua katika kila jambo, na siwezi kupangiwa nini cha kusema.

Mbona povu linakutoka hivo?
Kaa chini tulia eleza umma ni kweli mlikuwa faragha na Wiliam lukuvi?
 
Last edited by a moderator:
CCM kama chama pinzanina nyie akina Mtatiro, msitegemee watatoa kauli zitakazopelekea nyie kuungana.

They will always find some gaps ili wajenge kutokuaminiana ninyi kwa ninyi. Lazima muwe makini.

Mtatiro wewe ndio muongo na lichama lako la kidini lenye uponda ndani yake!
 
Back
Top Bottom