Uongo huharibu ndoa

fimboyaasali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
8,415
7,968
Mkiwa kwenye ndoa uwe mwanaume au mwanamke, acheni uongo, msidanganyane.

Ongeeni ukweli tu, wote muwe wa kweli miongoni mwenu na hata kwa watu wengine msiongope, mtaharibu ndoa yenu!
 
IMG_1225.jpg
 
mkiwa kwenye ndoa,uwe mwanaume au mwanamke,acheni uongo,msidanganyane.ongeeni ukweli tu,wote muwe wa kweli miongoni mwenu na hata kwa watu wengine msiongope,mtaharibu ndoa yenu
Pokea kombe lako. Umesema ukweli mtupu. Ni bora hata kama umekosea jambo, useme ukweli kuliko kudanganya. Unaweza kudanganya hata mara mia moa na usijulikane lakini siku utakapojulikana uongo wako wa siku moja tu, unaharibu credibily yako yote na mwenza wako anaanza kufukua yale ya nyuma. Nasema hivi nikiwa na first hand experince. Ex wangu alikuwa na degree ya uongo, mwanzoni sikumjua lakini nilipokuja kugundua uongo wa siku moja tu, nilifuatilia na kujua ambayo sikupaswa kuyajua. Yaani nikiandika kuhusu uongo wake watu watashangaa jinsi kulivyo na watu ma-specialist wa uongo. eg. imagine unaambiwa gas imeisha, anaitwa bodaboda, anakuja kuchukuwa mtungi kwenda kuwanunulia mtungi mwingine, anaondoka na mtungi, anazunguka mitaa miwili na kurudi na ule ule mtungi, unaambiwa gharama ya boda na gas ni kiasi fulani, unalipa. Kilichotokea? Gas haikuwa imeisha, ilikuwa nyingi kabisa ila umepigwa! Bodaboda na mama walishapanga!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom