Uonevu wamkera Jaji Mkuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uonevu wamkera Jaji Mkuu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by ngoshwe, Jun 8, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Agustino Ramadhani

  --

  JAJI Mkuu wa Tanzania, Agustino Ramadhani, amesema tatizo la kusuasua kwa uendeshaji wa kesi za jinai ambalo linahusisha mhimili wa mahakama na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hayaleti picha nzuri katika Wizara ya Katiba na Sheria.


  Jaji Ramadhani, aliyasema hayo kupitia hotuba yake ya kumkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, wakati akifungua kikao cha Majaji wa Mahakama za Rufaa, Mahakama Kuu Tanzania Bara na Zanzibar kilichofanyika Hoteli ya Ngurdoto, mkoani Arusha hivi karibuni na Tanzania Daima kupata nakala ya hotuba yake.


  Alisema matatizo ya ofisi hiyo, yamesababisha lawama nzito kwa mhimili wa mahakama, kitendo ambacho hakipaswa kuanikwa hadharani ama kupitia vyombo vya habari.


  Akitoa mfano, Jaji Ramadhan alisema anakumbuka vyema jinsi hali ya kutoelewana iliyowahi kutokea kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi, na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hosea, kuhusu kesi za Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA), wakati zikiwe kwenye mchakato wa kupelekwa mahakamani.


  "Lakini siyo tu kwa mahakama, haki za binadamu zinasiginwa na mhimili wa mahakama unafanywa mbuzi wa kafara," alisema Jaji Ramadhan.


  Akitoa mfano wa raia 36 waliokamatwa wakivua samaki katika ukanda wa Bahari ya Hindi, ambao wamepachikwa jina la "Samaki wa Magufuli", alisema walistahili kufunguliwa mashtaka Mahakama Kuu na kwamba ushauri ulitolewa juu ya jambo hilo na mtaalam wa sheria za Maritime, Kapteni Ibrahim Bendera ulipuuzwa.


  "Suala hili, lilipofunguliwa rasmi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi 23, 2009 hadi lilivyohamishiwa Mahakama Kuu mwaka huu, muda umepotea bure kwa ukaidi," alisema Jaji Ramadhan.


  "…Mwaka mzima washtakiwa wako rumande, wananyimwa dhamana mpaka mshtakiwa mmoja raia wa Kenya alifia gerezani hivi karibuni. Balozi wa China hapa nchini, alikuja kuniona juu ya wananchi wake kuwekwa ndani kipindi chote hiki, lakini jambo la kusikitisha ni kwamba chombo chetu hakiioni hali hii," alisema Jaji Ramadhan.


  Alisema kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, kodi za Watanzania, zimetumiwa kuwalisha raia hao wa kigeni na kusema kuwa hiyo siyo haki kwa wananchi.


  "Hivi haitoshi kumshtaki nahodha wa meli, ambayo imekamatwa na kuwaachia hao watu wengine waende zao? Nimeongea na DPP –Feleshi- na kuumuliza kama hawezi kuwafutia mashtaka hao wengine. Kubwa nililolipata ni kuwa anayemiliki meli hajulikani, lakini nahodha kashikwa tatizo liko wapi?" aliuliza Jaji Ramadhan.


  Alitoa mfano wa pili kuwa ni iliyokuwa kesi na.9/2009 iliyofunguliwa Mahakama ya Wilaya Septemba 15, 2009 dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki Kuu (BoT), Simon Jengo, Naibu Mkurugenzi wa Fedha za Nje, Kisima Mkango, na Mkurugenzi wa Huduma za Benki Kuu, Ally Bakari, na Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Huduma ya Sheria, Bosco Kimela, wanaotetewa na mawakili Mabere Marando na Richard Rweyongeza.


  Alisema hati ya mashtaka ya kesi hiyo ilitiwa saini Februari, 2009 na miezi nane yaani Septemba 15 mwaka huo, ndipo watuhumiwa walikamatwa na kufikishwa mahakamani.


  Alisema kila kesi inapotajwa katika mahakama ya Wilaya ya Ilala wimbo umekuwa ni ule ule wa upelelezi bado.


  "Suala muhimu ni kwa nini mashtaka yaliandikwa Februari, halafu washtakiwa hao wakakamatwa na kufikishwa mahakamani Septemba na upelelezi uwe bado haujakamilika?" alihoji Jaji Mkuu.


  Alisema ilipofika Mei 7 mwaka huu, kesi hiyo ilifutwa na mahakama baada ya kupokea hati ya DPP iliyoiarifu mahakama hiyo iifute kesi hiyo kwa sababu DPP hana nia ya kuendelea na kesi na baada ya muda mfupi DPP akawafungulia washtakiwa kesi nyingine Na.359/2010 dhidi ya watuhumiwa watatu na wakawa wanakabiliwa na mashtaka matatu ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma.


  "Mheshiiwa Waziri Chikawe, huku ni kutumia vibaya madaraka ya kukamata na kufungua mashtaka ambayo yatamnyima mtuhumiwa haki ya dhamana. Je, huku si kukomoana?" aliuliza Jaji Ramadhan.


  "Tukumbuke tuwatendee wenzetu kama vile tunavyotaka nasi tutatendewe, sidhani kama kuna yeyote humu ndani au ofisi ya DPP ambao wangependa wenyewe au jamaa zao kurundikwa rumande namna hii, kuna kila sababu ya kuondokana na hali hii," alisisitiza Jaji Ramadhani.
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana kabisa na maoni hayo, lakini kwenye kila uvunjwaji wa haki kuna remedy na redress, katika tort kuna vitu vinaitwa malicious prosecution na false imprisonment. Kama ni hivyo na ni dhahiri kuwa watu wanaletwa mahakamani bila ushahidi na sababu kwa nini mahakamama baada ya kuwaachia isiwashauri watu waliofungwa kwa uonevu wafungue madai dhidi ya serikali au yoyote alitewafunga?

  Hiyo haipo kwenye kesi hizo tuu kuna kesi nyingi za mauaji za kubambikiza. Mtu anakaa rumande miaka nane au zaidi akiletwa mahakani anaachiliwa DPP hana nia ya kuendelea na kesi, kwa nini watu hao wasiidai serikali, just imagine 8 years in jail halafu unaambiwa hakuna ushahidi.

  Mahakama nazo inabidi ziote meno, mtu anashikwa na msokoto wa bangi jela miezi sita, huu ni upuuzi, mtu anaosha gari pasipo ruhusiwa anafungwa miezi minne, wasomali wanaenda south Africa wanakamatwa wanakaa rumande wiki. Yote hii i gharama ya mlipa kodi anayepata hasara ni serikali .
   
 3. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nafurahi kwamba amesema mheshimiwa mkubwa sana kama huyo. Lakini ngoja kidogo, huyu anayesema maneno hayo utadhani ni mlala hoi wa kijiji cha mbali sana Tanganyika ambaye hajui hata Kariakoo iko wapi katika ramani ya DSM. Si ni subordinate wake wanaofanya madudu hayo? Anashindwa vipi kuwarekebisha katika taratibu za kazi za kila siku akapanga job description za watu wote walioko chini yake na kusimamia madudu hayo hayapewi nafasi?

  Wait a minute, hivi Chief medical Officer akianza kulalamika kwamba madaktari na manesi wanafanya ndivyo sivyo akiwashitakia kwa waziri wa afya, si anajionyesha kwamba yeye mwenyewe anao udhaifu katika mamlaka alizopewa? Hivi waziri wa kilimo anatakiwa kulazimika kuhakikisha mbolea inafika Ng'wagitolyo kwa wakati yeye binafsi ili Kilimo Kwanza kifanikiwe na sio maafisa mbalimbali walioko chini ya wizara hiyo?

  Mweeeee! Mwe! Sio changa la macho hilo? Mwe mwe mwe mwe mwe!
   
 4. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hapo ni CJ anamlalamikia waziri wake kuhusu udhaifu wa Ofisi ya Mwansheria Mkuu Idara ya DPP. Ni dhairi kuwa Chikawe anajua kwani nae ni Mwanasheria, ilimpasa CJ kumpiga beat la moja kwa moja Werema na Vijana wake akina Feleshi, na IGP Mwema ambao ndio shida kubwa katika kuchelewesha kesi, kubambika watu kesi nk.

  Hakuna ufanisi kabisa katika ofisi ya AG. Lakini iliipasa pia Idara ya Mahakama kutolalamika hewani kana kwamba wao hawapo chini ya Wizara mmoja wakashindwa kuwasiliana ndani kwa ndani..hapa wananchi wa kawaida hawaelewi Ramadhan anasema nini kama si kujaribu kujiosha kwa matatizo ambayo wao walipasa kuyavalia njuga kwa nguvu zote ili wananchi waone Mhimili huo ukitenda haki.

  Mahakama pia zimekuwa zikihusika kwa hali majo au nyingine kukiuka haki za raia kwa mfano kuendelea kuruhusu mtuhumiwa asote rumande hata kama DPP hana sababu za kushindwa kuendeleza kesi ikiwemom kuleta mashahidi mahakamani. DPP akiomba kesi ihairishwe,mara nyingi Mahakama zetu zinaridhia tu hata ikiwa muda unaotakiwa kisheria kwa kesi kuanzwa kusikiliza ukiwa umepita.
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Tulaumu sheria, sio mahakama, ona kifungu 225 cha kanuni za kuendesha kesi za jinai kinaruhusu baadhi ya kesi kufutwa kama ikikaa mwezi, siku 60 au siku 90 bila kusikilizwa na bila kuwa na kibali basi mahakama ina uwezo wa kufuta kesi hiyo lakini wakati huo huo sheria inaruhusu mshtakiwa kufuguliwa kesi ile ile upya, haileti maana kabisa.
   
Loading...